Kauli ya Rais wa TLS kuhusu kufunga kanisa la Gwajima

Kauli ya Rais wa TLS kuhusu kufunga kanisa la Gwajima

Kitchener

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
13,833
Reaction score
27,753
NINA LAANI NA KUKEMEA UNYANYASAJI NA SHAMBULIO LA KIIMANI LINALOFANYWA DHIDI YA WAUMINI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA.Ni Vema Viongozi wa Serikali wakatambua kwamba

1.Nikiambiwa nichague kati ya Yesu na Tanganyika nitachagua Yesu.

2.Nikiambiwa nichague kati ya Yesu na Ukimya munao uita amani na Imani yangu katika Msalaba narudia tena nitachagua Imani yangu katika Msalaba.

3.Nikiambiwa nichague kuheshimu amri haramu na Biblia nitasimama na Biblia.

4.Nikiambiwa kutii amri inayonikataza kuhubiri na Kumuabudu Mungu wangu nitachagua kumuabudu Mungu hata ikilazimu Mauti.

Serikali kwa Makusudi au kwa kudhani inajilinda kudhibiti ukosoaji inashambulia Ukristo kwa kudhani inamkomesha Askofu Gwajima kwa kosa la kukemea utekaji na Watekaji.

Katika hili Mimi Binafsi nasimama kuhesabiwa na ninatafakari na kuwa tayari kusimama upande wa Kristo bila hofu.

Hili ni Shambulio dhidi ya Imani wala siyo shambulio dhidi ya Dini ,Shehebu au Bishop.Gwajima.

Ufungiwaji wa Kanisa hili ulifanyika

1.Kinyume cha Sheria

2.Kinyume cha Katiba ya Nchi

3.Kinyume cha Haki ya Msingi ya Kusikilizwa.

4. Maneno na Kauli alizozitoa Bishop Gwajima ni za kweli na hazikuvunja sheria zozote na ninarejea kwamba

YEYOTE ANAYE MSHAMBULIA MTU ANAYEPINGA UTEKAJI NA UPOTEZWAJI WA WATU NI AMA MTEKAJI,WAKALA WA UTEKAJI AU MNUFAIKA WA UTEKAJI.KANISA LINATAKIWA KUTAFAKARI SHAMBULIO HILI DHIDI YA IMANI
 
Tanzania ina vichekesho sana. Kama mawakili wasomi wanaamua kumchagua mtu ambaye dishi limeyumba, unaweza kuwategemea walete hayo mabadiliko kweli?
 
kichaa cha mwabukusi hapo ni nini kwa maneno hayo?
 
"Nikiambiwa nichague kati ya Yesu na Tanganyika nitachagua Yesu."
AKIMAANISHA, nikiamua kuchagua dunia au kuabudu Mungu, nitatanguliza haki ya kuabudu Mungu aliyeumba Tanganyika. ni msisitizo tu wa umuhimu wa kuepuka kunyima watu haki ya kuabudu kwa sababu tu wamekosoa serikali.
 
AKIMAANISHA, nikiamua kuchagua dunia au kuabudu Mungu, nitatanguliza haki ya kuabudu Mungu aliyeumba Tanganyika. ni msisitizo tu wa umuhimu wa kuepuka kunyima watu haki ya kuabudu kwa sababu tu wamekosoa serikali.
Asante sana kwa ufafanuzi zaidi
 
kuna siku haya yote yatapita.
 
Back
Top Bottom