PreGE2025 POTOSHI Kauli ya Rose Mayemba kuwa uwezo wa Mwenyekiti kuipeleka CHADEMA mbele umeisha ilimlenga Lissu

PreGE2025 POTOSHI Kauli ya Rose Mayemba kuwa uwezo wa Mwenyekiti kuipeleka CHADEMA mbele umeisha ilimlenga Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1752219744156.png
 
Tunachokijua
Rose Mayemba awali aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kabla ya uteuzi wake na wajumbe wengine kutenguliwa na Msajili wa vyama vya siasa, na kisha baadaye kuteuliwa tena kwa ajili ya kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Januari 19, 2025 Mayemba alipata nafasi ya kuzungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine alitumia nafasi hiyo kueleza changamoto alizokumbana nazo wakati wa usaili wa nafasi za Kamati Kuu ya CHADEMA uliofanyika Makao Makuu ya chama kikiwa ni kipindi cha uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho uliofanyika Januari 2025.

Ipo video iliyochapishwa katika mtandao wa Facebook ikimuonesha Rose Mayemba, akisema uwezo wa Mwenyekiti kuipeleka CHADEMA mbele umeisha, ikiambatanishwa na kichwa cha habari kikimhusisha Lissu kuwa "Lissu akataliwa"


Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search, pamoja na marejeo ya video umejiridhisha kuwa kipande hicho kimepotoshwa muktadha wake halisi kwani katika Hotuba yake Mayemba alikuwa akimzungumzia aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA wakati huo, Freeman Mbowe akimuhusisha na changamoto zilizojitokeza wakati wa Uchaguzi wa CHADEMA mkoa Njombe.

Video hiyo haina uhusiano na uenyekiti wa Lissu bali Mayemba alikuwa akikosoa utendaji wa Freeman Mbowe alipokuwa Mwenyekiti. Rejea video halisi hapa.

"Mambo haya yote ninayoyasema tulikuwa tukimtumia Mwenyekiti, kwanini Njombe haitaki Freeman Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti. Mambo yote tuliyokuwa tunazungumza hapa tulikuwa tukimtumia 'inbox' kama baba yetu."

"Tunamwambia mwenyekiti kuna hili linaendelea, katikati ya uchaguzi wa kwanza nilioshinda, meseji zilikuwa zinatumwa ukumbini zinasema 'mimi Freeman Mbowe' namuunga mkono yule mgombea mwenzangu' anatajwa 'naomba mumpigie kura tutampa ushirikiano' zile meseji tukiamini kwamba hii haiwezi kufanywa na Mwenyekiti. Zile meseji tulimyumia mwenyekiti, tukamtumia John Mrema, tukawatumia na viongozi wengine wa chama."

"Wengine wakasema tunalifuatilia, mpaka kesho halijawahi kuchukuliwa hatua. Tuliamini baada ya hayo yote kutokea jambo fulani lingetendeka kunusuru mkoa wa Njombe, haikutokea. Njombe wakasema uwezo wa mwenyekiti wa
kufikiri na kuipeleka CHADEMA mbele, umeisha, hata wanaomsaidia, walio Pembeni yake ni bahati mbaya hawataki kumwambia ukweli na wanashiriki kuharibu haki za watu huko chini"

View: https://youtu.be/pfMrZF7ISCc?si=uMDAQatyLfFIaYTY&t=356
​
Back
Top Bottom