Kauli ya "Tutafute Pesa" Ipuuzwe; Kwa Hatma njema Mtafute Mungu wako.

Kauli ya "Tutafute Pesa" Ipuuzwe; Kwa Hatma njema Mtafute Mungu wako.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
IPUUZE KAULI YA "TUTAFUTE PESA" KWA HATMA ILIYONJEMA BASI MTAFUTE MUNGU WAKO.

Anaandika, Robert Heriel
Yule Shahidi!

Andiko hili lisomwe na Vijana wote.
Usiwe mtumwa wa Pesa.
Usiihusudu hata Kama unaambiwa ni tamu. Kamwe usije kujidanganya. Hakuna Raha yoyote ya kuwa na pesa kama huna Mungu.

Hakuna Raha yoyote ya kuwa na elimu kubwa Kama huna Mungu. Waliosoma wataungana na Mimi.

Hakuna Raha yoyote ya kuwa na Mke/mume mzuri kama hauna Mungu. Wenye wenza wazuri tunalijua hili fika na ni mashahidi.

Kila kitu Duniani ni chakawaida isipokuwa Mungu. Utakiona cha thamani ukiwa haupo nacho, lakini ukiwa nacho huwa chakawaida. Kabisa!
Ila kuwa na Mungu huwezi kuona ni kawaida, utakuwa na furaha kuliko kawaida.

Vijana acheni kujihangaisha na kutafuta pesa, nisikilizeni Mimi Taikon, mara nyingi ukiona Jambo ninalisema ujue nimelipima, nilimelichunguza, siongei Kwa mihemko.. naongea Kwa uhalisia.

Mtafute Mungu wako, mpende, mthamini, sikiliza sheria zake, fuata maagizo yake alafu ukiishi maisha mabovu nakuruhusu uniite MBWA! Nakuruhusu unitukane tusi lolote.

Falsafa ya Yesu (moja ya wanafalsafa ninaopenda Falsafa zake) anakuambia; Kwanza utafuteni Ufalme wa Mungu, na haki yake, na mengine yote mtazidishiwa.

Vijana, jaribuni kunielewa.

Nimeona Vijana wengi wakihangaika na kulialia, wamechanganyikiwa.

Ukijifanya Mkaidi, basi sio ajabu haya yatakupata,
Dunia itakuacha Kwa kila kitu Kwa sababu unakimbizana nayo, utachelewa Maeneo mengi tena nyeti;
Utachelewa kuoa na kuolewa kisa kutafuta Pesa.
Utachelewa kujenga na kuwa na mji wako.
Utakuwa Under attacks Hali Internal & External Attacks. Ndipo mtu anakuwa na Msongo wa Mawazo,
Kukata tamaa, kuchanganyikiwa Kwa kuenda huku na huko kutafuta msaada mara Kwa wachungaji mara masheikhe mara Waganga. Hiyo ni Dalili ya kushambuliwa.

Kujiingiza kwenye Madawa au pombe,
Kukataliwa na Wakati, watu na mahali unapoishi.

Kuwa mwaminifu Kwa Mungu wako.
Hakuna sababu yoyote itakayokufanya usimuamini Mungu aliyekuumba na kuumba huu ulimwengu.

Kumbuka Mungu ndiye mwanzo hivyo atakusaidia kuanza Jambo lolote, naye ndiye mwisho atakusaidia kumaliza Jambo lolote utakalolianza.

Tafuta Mungu ili upate Pesa

Taikon leo sitaki kusema mengi.
Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Umasikini unadhalilisha mkuu asikuambie mtu....ukiwa msikitini ibadani umevaa kanzu yako ya kizamani halafu imechoka wakati huo wenzio wametupia kali za 70k-200k unahisi mnyonge na dhaifu (umasikini unauma kumoyoni ) ....hivyo hivyo ukiwa kanisani ibadani wenzio wametupia skuna kali halafu umevaa kiatu yako imeisha sori upande au imetoboka na umeirudishia sio siri unajihisi dhwaiful hali (umasikini unauma kumoyoni).....ni kweli uyanenayo lakini wacha watu watafute pesa.....
 
Hakuna aliye kama Mungu yeye yupo kabla ya nyakati na hakuna sehemu imetajwa mwanzo wake wala mwisho wake, hakuna aliye juu yake wala alie kando yake wala alie nyuma kiti chake cha enzi.

Lakini mfumo alio uweka yeye ndio unao tufanye tuwe kinyume na ulivyosema mleta mada.

Yeye alisema mwenye nacho ataongezewa na asie nacho atanyang'wa mpaka kile kidogo alicho nacho.
Japo kifalsafa au kiteolojia inaweza kutafrika kwa namna nyingi lakini ndugu tutafuteni pesa.

Hakuna ufahari wowote katika umaskini, hakuna furaha ,wala amani au jema lolote katika umaskini.

Asante kwa mada nzuri by the way.
 
Mara ya kwanza kushika kiasi kikubwa cha fedha, nikiwa mdogo , ilikuwa Ni Laki 5 but sikuwa na furaha

Nikajaribu kutembea na kila aina ya wanawake , labda ningeiyona furaha but ikawa ndo zaidi najiongezea maumivu.

Nikajaribu kuchanganya pombe na wanawake , hii ndo kabisa , ili taka kunipelekea kujiua

So nikaanza kwenda maombi( kanisani ) , kufunga na kukesha hapa ndipo nikaanza kuiona furaha ya kweli kutoka moyoni - sana nikijawa roho mtakatifu
 
Katika kumtafuta Mungu ukifika huko makanisani ni kutoa pesa kwenda mbele.

Siku hizi adi wana namba za kulipa na kutoa kwa simu.

Tafuta pesa itafute furaha maliza maisha zikwa
 
Na huu ndio ukweli wa maisha atakae pinga na apinge
 
Back
Top Bottom