Kauli ya vijana wengi wamejiajiri kwenye bodaboda ina usiasa mwingi ndani yake

Kauli ya vijana wengi wamejiajiri kwenye bodaboda ina usiasa mwingi ndani yake

Mbahili

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
281
Reaction score
525
Kuna kauli mpya mjini imezuka iliyoletwa na jamaa wetu wa ma'mbele, kuhusiana na vijana na bodaboda. Ningetumia fursa hii kuliomba Baraza la Kiswahili nchini (BAKITA), kukipa neno "Lema" kama neno jipya likimaanisha kisawe cha bodaboda. (Hapo tutasema mangi kaupiga mwingi). 😂😂 Utani Mangi usinimaindi wala nini.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Baada ya kusikikia vijana wengi wamejiajiri kwenye biashara ya bodaboda, basi kama nilivyofundishwa nilichukua kalamu na karatasi. Nikachagua sehemu mashuhuri panapoitwa vijiwe vya bodaboda, nilichagua vijiwe ishirinii zenye bodaboda zaidi ya 20.

Hivyo ukichukua 20*20 unapata 400, hivyo ni population nzuri kufanyia utafiti wetu. Kwa kila kijiwe nilichukua bodaboda kumi kufanyia utafiti. Hivyo 10*20 miambili sampo nzuri kwa kuanzia. Kwenye questionnaire yangu kulikuwa na sehemu A na sehemu B.

Sehemu A inajazwa na kijana mmiliki wa bodaboda. Kama dereva sio mmiliki wa bodaboda, basi amjazie bosi kama ana umri chini ya miaka 45.

Sehemu B, ilipaswa kujazwa endapo dereva hana umiliki wa chombo hicho. Ila kuna kipengele pia kama hana umiliki, basi anamkataba na chombo hicho (ma'nake bado si mmiliki).

Kiukweli utafiti ulienda vyema. Nilikuja na hitimisho kuwa kwa kila kijiwe watu zaidi ya 7...(7/10) hawana umiliki wa chombo, hivyo 0.7 hawana umiliki na chombo. 0.3 humiliki zaidi ya 0.2 wamemaliza mkataba na kupewa chombo.

Kwa upande mwingine section A. Mabosi wa vijana hawa zaidi ya 90%, ni zaidi ya miaka 45. Hivyo si vijana..

Hitimisho:
Vijana wengi wamejiajiri kwenye biashara ya bodaboda sio halisia bali vijana wengi wameajiriwa kws biashara bodaboda. Bado hawajajiajiri sababu biashara si zao, wana maboss zao. Na mwisho kabisa baada ya utafiti wangu nilikuja na uzi kuwa nataka ninunue bodaboda niwape vijana, walete mahesabu. Kama mlinifuatilia
 
Back
Top Bottom