Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kauli iliyotolewa na Mkuu wa wa Dar, Amos Makala, kwa wazazi wa watoto kuwa atakayemkosa mtoto wake nyumbani, basi anapaswa aende kituo cha Polisi au hospitali kwenda angalia kama yuko huko, ni kauli ya vitisho visivyokuwa na msingi na ni kauli ambayo inakiuka Haki za Binadamu.
Najua Mkuu wa Mkoa, ametoa kauli hiyo kuhusiana na kukerwa na vitendo vya vijana wadogo, wanaofahamika kwa jina la Panyaroad, kwa vitendo vyao vya kuvunja nyumba za wakazi wa jiji la Dar, kufanya wizi wa vitu mbalimbali, kujeruhi hadi kusababisha vifo, kama ilivyotokea hapo majuzi huko Kawe.
Lakini nijaribu kumuuliza Mkuu wa Mkoa wa Dar, hivi yeye anadhani kwa kutumia vitisho hivyo, ndiyo atakuwa amepata ufumbuzi wa vitendo hivyo vya Panyaroad?
Hivi anajua "impact" ya kuyatamka maneno hayo hadharani, akiwa ndiye Mwenyekiti, wa Kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa huo wa Dar?
Nimuulize tena Mkuu wa Mkoa, hivi anajua kwa kuyatamka hayo maneno, ni kama ametoa "blessings" zake kwa Polisi wetu, waweze kujeruhi na hata kuua hao wanaoitwa Panyaroad, bila kwanza kuwahoji na kupata ushahidi wa hao wahalifu?
Hivi yeye Mkuu wa Mkoa, anatambua kuwa kwa tamko hilo anakiuka misingi ya Haki za binadamu?
Ninaposema hivyo, siyo kuwa naunga mkono vitendo hivyo vya kinyama vya hao wanaojiita Panyaroad, la hasha, nia yangu ni kulitaka Jeshi la Polisi, litende Kazi zake kwa Weledi mkubwa, kwa kufuata sheria.
Polisi wetu wanafahamu kuwa Hawama mamlaka ya kuua raia yeyote bila msingi wowote.
Tunafahamu pia kuwa Katika nchi yetu, ni mhimili wa Mahakama pekee, uliopewa mamlaka ya kumtia hatiani raia yeyote na kutoa hukumu.
Nchi hii inaendeshwa kwa kufuata misingi ya kisheria.
Hivi anaweza kutuambia kwa kuyatamka hayo maneno, ni sheria gani inayomruhusu yeye kama Mkuu wa Mkoa, aliagize Jeshi lake la Polisi, litekeleze majukumu yake, pasipo kuzingatia sheria za nchi hii?
Kwa hiyo Mkuu wa Mkoa, Amos Makala, anapaswa aombe radhi kwa wakazi wa Mkoa wa Dar, kwa matamshi aliyoyatoa, ambayo ni kinyume cha utawala bora, unaozingatia sheria.