Kauli za Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makalla, zinakiuka Haki za msingi za Binadamu

Hali ya uchumi ni ngumu sana.

Hao panya road wameona uhalifu ndio suluhisho la kujipatia kipato.

Wakipora wanasaidia na familia zao.

Hili tatizo lina mizizi mirefu sana.

Halitamalizwa kwa kauli tu.
 
Mpuuzi mmoja wewe...ngoja yaje yakufike ndio utajua
 
Alitakiwa kusema wakaangaliwe mochwari
 
Ndiyo upumbavu walionao hao, yani tangu mauaji yaanze kule Chanika, yakaja Kawe na kwingine kote huko wamekaa kimya tu, vyombo vya ulinzi na usalama vinataka vianze taratibu zake, wanaanza kuhemukwa.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Mpuuzi mmoja wewe...ngoja yaje yakufike ndio utajua
Asubiri siku avamiwe, apigwe, aibiwe, mke wake abakwe mbele yake na yeye alawitiwe mbele ya mke wake halafu arudi hapa JamiiForums na tantalila za haki za binadamu.

Wote tunatambua umuhimu mkubwa wa haki za binadamu lakini kuna wakati tukizitanguliza sana mbele Nchi haitafaa kuongoza.
 
Ni kwanini Jeshi letu la Polisi, pamoja na nguvu Kazi waliyo nayo na vifaa vya kisasa vya kutambua wahalifu, washindwe kuwatambua hao vijana wadogo, ambao wanatumia silaha za jadi, kama mapanga pekee?
Hilo hilo jeshi ndo tumesikia watu wamefia mikononi mwao bila kutoa maelezo. Je, hata mkuu wa mkoa akisema wawachukue vijana walio mitaani yawezekana wakawachukua walio majumbani kwa amri ya watu wasiojulikana.

Nchi hii ina drama nyingi na siasa nyingi na maneno ya kulindana bila sababu. Neno la bado tunashughulika ni wimbo mzuri unaotupeleka kulala kama watoto.
 
Makala kwa kauli hii amezingua anasahau yeye ni wa wote wahalifu na Wema, He is Comforter in Chief at Region level kauli tata kama izo niku create tension zisizo na Msingi, Hakuna anae afika na Mambo yanayofanywa na Panyaroad ila Asingeongea ivo public na aiende security organs zake Secretly na atoe hayo maelezo makali kabisa, Ku publicly issue kama hio kuna leta maneno mengi ila pia makala sio Mahakama aache kila mtu afanye kazi yake
 
Hao mapanya road wakikamatwa eneo la tukio wapigwe na kuinamishwa wangese sana hao madogo.
Wanataka vya bure si ndio wacha wapigwe kenge hao.
 
Mkuu labda kama hujakutana na hao panya road. Nipo hapa nauguza majeraha na nimechukulia vitu. Acha washughulikiwe.
 
Kwani hao panyaroad wanafata haki za binadam,mbona wakati wanafanya ushenz hao watu wa haki za binadam hawasemi kitu
Kuna mambo ukitaka kudeal nayo
Lazima udeal kikauzu

Ova
Huyo labda kama hajakutana na hao panya road. Nipo hapa nauguza majeraha na nimechukuliwa vitu. Acha washughulikiwe.
 
Kuna aliyesema msaliti apigwe shaba na jioni yake Tundu akapigwa chuma tena aliyesema ni mkuu wa mihimili yote, so haki za binadamu zipo kwenye makaratasi tu.
 
Haki za binadamu ni kwa ajili ya binadamu pekee.
Ukishakengeuka unajivua ubinadamu; hivyo utashughulikiwa kwa namna stahiki kuendana na identity mpya uliyojivika.
Ni wakati muafaka kuwaasa vijana kuzingatia maskani, vijiwe, na wenzao wanaoshirikiana nao kijamii. Nyakati kama hizi ni rahisi wasiokuwamo na waliomo kutotofautishwa.
 
Ni kwanini Jeshi letu la Polisi, pamoja na nguvu Kazi waliyo nayo na vifaa vya kisasa vya kutambua wahalifu, washindwe kuwatambua hao vijana wadogo, ambao wanatumia silaha za jadi, kama mapanga pekee?
Hao vijana wanatoka sayari ya Mars?

Jamii ya kihalifu huzalisha jamii ya kihalifu.

Tuanze kutatua machangamoto ya malezi na shule za watoto wa Taifa hili hautakaa usikie panyaroad.

Polisi wenyewe wameajiri wahalifu kibao humo ndani ndo maana kila kukicha utasikia majanga juu ya majanga dhidi ya raia.

Kiongozi kama Makala hawanaga mikakati ya kuzuia ama kudhibiti uhalifu zaidi ya matumizi ya nguvu, ubabe na kuvunja haki za binadamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…