Kauli za Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makalla, zinakiuka Haki za msingi za Binadamu

Ila madogo acha washikishwe adabu, maana ndo tunaitwa wanaume wa Dar.
Hata wakishikishwa ukuta bado wanaume wa dar watabaki wanaume wa dar.Wala chips,soseji,miguu ya kuku na shingo na utumbo wa kuku.Mnasubiri watoto wadogo washikishwe adabu na polisi.Kazi na nguvu zenu zilikwina?
 
Hao vijana wanatoka sayari ya Mars?

Jamii ya kihalifu huzalisha jamii ya kihalifu...
Ndiyo maana nikasema hao Polisi wanapashwa kufanya Kazi kwa kufuata Weledi.

Kupokea maelekezo toka juu, ambayo wanajua yanakiuka sheria, itakuja kula kwao!
 
Ni kwanini Jeshi letu la Polisi, pamoja na nguvu Kazi waliyo nayo na vifaa vya kisasa vya kutambua wahalifu, washindwe kuwatambua hao vijana wadogo, ambao wanatumia silaha za jadi, kama mapanga pekee?
Wana intelijensia ya kudhibiti wapinzani tu sio wahalifu
 
Mimi naona kuna umuhimu kuanzisha kikosi kazi kitengo maalumu cha muda wote kuzibiti magenge kama haya sio dar tu magenge haya ya kialifu yapo mikoa yote
Ina maana huwaamini polisi mpaka uanzishe vikosi mbadala?...
 
Mimi nionavyo mkuu wa mkoa yuko sahihi, Sasa unavyotaka wewe Ikiwa mwanao kapotea hajarudi nyumbani siku moja au mbili simu humpati sasa ufanye nini kama sï kwenda kuripoti polisi au kwenda kutafuta hospitali kama unatafauti na mkuu wa mkoa tuambie tu.
 
Makala na Mwigulu wametokana na mold moja. Akili zao zipo kimehemko na sifa.

Makalla miaka yake yote ya ukuu wa mkoa hana la maana lolote alilo accomplish zaidi ya matamko tata.

Hili swala la panya road lilipaswa liwe historia lakini imekuwa kama vile panya road wameizidi nguvu serikali yote. Halafu anatokea mpuuzi mmoja kutoa vikauli kila kukicha lakini matokeo hatuyaoni.
 
Kwahiyo ni Haki za binadamu kuwa mhalifu aliyebeba silaha na zana za maangamizi na anayeua watu Ili aibe, asakwe na akatwe kwa kupetiwa petiwa?!
 
Na wewe utuambie kama ni sahihi kwa wazazi wa Dar es salaam kuwaacha watoto wao bila malezi mazuri na kutuzalishia kundi la watukutu linalopora na kuua raia jijini ?
 
Najua ulichokisema ni sahihi kabisa.

Nilichomwelewa Mkuu wa Mkoa wa Dar, ni kuwa huyo mwanangu, nisipomwona, nijue kuwa atakuwa "kashughulikiwa" na Polisi, na hivyo nikamtazame "mortuary" kwa kuwa atakuwa keshapoteza uhai!

Ndiyo maana nikasema, hao Polisi kwanini wajipe, mamlaka ya kuondoa uhai wa raia wenzao, wakati kuna mhimili wa Mahakama, uliopewa jukumu la kusikiliza ushahidi, hadi kumtia hatiani mtuhumiwa?
 
Ulitaka asemeje?
Una watoto waovu inaelekea!
 
Ni kwanini Jeshi letu la Polisi, pamoja na nguvu Kazi waliyo nayo na vifaa vya kisasa vya kutambua wahalifu, washindwe kuwatambua hao vijana wadogo, ambao wanatumia silaha za jadi, kama mapanga pekee?
SASA kawe Ndio viongozi wanakaa na kuna kambi za jeshi na wameenda kufanya matukio ni hatari sana
 
Hao vijana wa panya road hawakuleta mbwembwe awamu ya Tano walijua wanacheza na kifo Sasa ivi wanapetiwa patiwa na mamlaka na nyinyi haki za binadamu,natamani siku wakubane kwenye Kona na Panga la kukukata bega kisha ulete haki za binadamu,tuchangie.
 
Ulimakafu
 
Hao vijana wa panya road hawakuleta mbwembwe awamu ya Tano walijua wanacheza na kifo Sasa ivi wanapetiwa patiwa na mamlaka na nyinyi haki za binadamu,natamani siku wakubane kwenye Kona na Panga la kukukata bega kisha ulete haki za binadamu,tuchangie.
Tatizo mkuu wa nchi wa sasa haijui vizuri hii nchi. Anadhani JPM alikuwa katili ilihali alijitahidi kukomesha uhalifu na wahalifu kwa kushirikiana na kamanda Siro!
Raia wema tuliishi kwa amani.

Sasa mama yeye anadhani Tz ni kama ulaya, polisi wawabembeleze wahalifu.😲🤔 Hawajui vizuri wahalifu wa tanganyika. Ukiwachekea utaambulia mabua!

Sasa hivi mauaji kila mahali. Mara wivu wa mapenzi, wizi nk. Tofauti na awamu iliyopita. Wengi waliopotea walikuwa wahalifu. Leo hii raia wema ndio wanapotezewa uhai na wahalifu tena hadharani kwa kukatwa mapanga. Ama kwa hakika tutamkumbuka sana hayati JPM! RIP
 
Mkuu wa mkoa yupo sahihi kabisaaaa, akimaanisha kwamba usipo muona kijana/binti yako wahi hayo majengo tajwa, kama ni amedhurika na panya road basi wahi utamkuta ICU, kama ni panya road bas wahi kumtazama kituo cha polisi haraka sana. Nanyie wanaume wa dar achen uvivu na ushoga mnashindwa kabisa na vitoto 40!!!?? Hivi kuna ugumu gani kam wanaume marijari kabisa kila mtaa wakatoka wanaume 20 tu wa kutembeza mkong'oto mtukufu pindi vijana hawa wakitimba mtaani kwenu!? ni swala la kusema wamefika tuwashughurikie na mkaachana na dhana kutafuta vichochoro vyenye upenyo vya kuchoropokea pindi vitoto vikitimba. Km mnabisha tukopesheni hao panyabuku hata mia tu waje hapa Kyela mjini tuwape somo la kulia bila kutoa machozi bali manundu

Sent from my OPPO A57 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…