Kauli za sasa za Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuhusu CORONA zimeshaanza Kuzua 'taharuki' nchini, hivyo ama adhibitiwe au ajiuzuru upesi

Hizi ni ramli.
kwani huko ulaya na marekani walichukua siku ngapi na kuanza kufa?.
Hii ni wiki ya tatu.
JE UNA TAARIFA YA KIFO CHOCHOTE KILICHOSABABISHWA NA CORONA?
"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
mjingamimi,
Unataka uhakika gani mkuu....rate yako ya kupima vitusi ni ndogo sn so huwezi kuwa na rekodi sawa na wanaopima wananchi wao kwa kiwango kikubwa kwa siku....
Nyie endeleeni kujifariji kijingajinga
 
GENTAMYCINE,
Wewe ulivyo popoma badala ya kuelezea nini kifanyike baada ya tamko la waziri. Unaishi kulalama tu hapa.

Ok. Ulitaka mh Ummy abaki na taarifa ili kesho na kesho kutwa muanze kusema serikali inaficha taarifa. Nyumbu mnatakiwa kibadilika.

Serikali inachukua kila hatua ili kudhibiti ili janga halafu wewe unaleta midhaa hapa.
 
Mbona bwana trump aliwaambia raia wake wajiandae kwamaambukizi makubwa navifo nakweli baada yawiki mbili mbele maneno ya bwana trump yakatimia?

Sasa waziri wetu kakosea wapi? Katika kipindi kigumu ambacho Ummy mwalimu anapitia basi nikipindi hiki ambacho anatakiwa apewe moyo nafaraja sana.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa..... Mungu ibariki dunia nzima nawatu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiuhalisia sisi tuna maambukizi mengi kuliko majirani zetu

Kwa ' Body Language ' tu ya Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu na jinsi Seriakali ya China inavyopambana Kuisaidia Tanzania yenye Wagonjwa 25 tu mpaka sasa huku ikiiacha kama si Kuisusa nchi ya Kenya yenye Maambukizi zaidi ya 180 ya CORONA naweza Kukubaliana nawe kuwa hali ni mbaya na huenda kama alivyotutisha Waziri husika kuwa kuna ' Community Transmission ' inakuja muda wowote kuanzia sasa basi Biashara ya Majeneza na Sanda ikaanza kulipa mno hasa hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
 
Pengine waziri amechoka kufichaficha roho inamsuta inabidi atubie ukweli tujiandae kisaikolojia
 
kila mara nasema corona INAJIONYESHA YENYEWE..
Hata usipopima watu kama wapo wanaoumwa wataonekana..
JE wapo hao wanaonekana?.
WANA DALILI KUWA WANA CORONA?.
Korona haijifichi mzee.
Unataka uhakika gani mkuu....rate yako ya kupima vitusi ni ndogo sn so huwezi kuwa na rekodi sawa na wanaopima wananchi wao kwa kiwango kikubwa kwa siku....
Nyie endeleeni kujifariji kijingajinga

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Hizi ni ramli.
kwani huko ulaya na marekani walichukua siku ngapi na kuanza kufa?.
Hii ni wiki ya tatu.
JE UNA TAARIFA YA KIFO CHOCHOTE KILICHOSABABISHWA NA CORONA?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
Mkuu kukuelimisha ni sawa n kupka rangi hewa!!!
Nenda Muhimbili ujionee!
 
Kuchelewa kuwazuia Wachina na au kuwaweka karantini siku 14 kabla hawajaanza umachinga wao hapa Tz yaweza kutugharimu maisha ya WATZ wengi.

Wamefikia wangapi hadi jioni hii?

Kuna waliotangulia mbele za haki?
 
Hili swala ni zito zaidi ya tunavyo dhani. Mungu atunusuru tu maana huyu mama kabla ya tukio la kwanza kabisa la Isabella Arusha.. alisha sema hatuna uwezo wa kupambana na janga hilo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jidu La Mabambasi watu wanadhani wanaoshauri kinyume na serikali ni wasaliti ila wao wanaokubaliana na kila jambo la watawala ndiyo wazalendo!!
Mkuu mtu asiye elimika katika basic principles za hygine ni vigumu sana kumuelimisha ukubwani.
Watu hawaelewi.
Nakumbuka Miaka ya Mwalimu , Dr Leader Stirling aliposema ugonjwa wa kipindupindu unatokana na kula uchafu wako mwenyewe.
Waswahili pamoja na wanasiasa wa TANU miaka hiyo hapa walikuja juu kama moto wa nyika, wakisema mzungu kawatukana.

Dr Stirling alikuwa sawa kabisa kisayansi maana kipindupindu kinatokana na bacteria wa ecoli ambao hutokana na kinyesi cha binadamu.
Wangekuwa wameelimika wangejua jinsi ya kujikinga.
Hili gonjwa la corona tukisema linahitaji total lockdown, watu wanasema tunampinga mheshimiwa Magufuli.
Hivyo hakuna njia watu wapukutike tu ili tupate akili.
(Sahihisho: Dr Leader Stirling alikuwa daktari na waziri wa afya na SIYO Mzee Bryceson, kundradhi)
 
Hangaikeni wee ila tambueni hakuna mtu anayeweza kulinda uhai wake duniani. Hakuna aliye na mamla na uhai wake..Muda ukifika utakufa kama bado huwezi kufa kamwe!
.....Bwana asipoulinda mji waulindao wanakesha
Mkuu Mungu alikupa akili itumie,usiende kimbuzi mbuzi
 
Ni watanzania wangapi wapo mitandaoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…