Kauli za sasa za Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuhusu CORONA zimeshaanza Kuzua 'taharuki' nchini, hivyo ama adhibitiwe au ajiuzuru upesi

Ulitaka awasilishe kwa njia gani? Maana naona ...ueleweki watu wanapaswa kuambiwa ukweli..local transmission inaenda kuchukua nafasi ni jambo zuri / isipokuwa mapopoma wetu watz wanaogopa kifo sana.
Mkuu huyo ni nyumbu! Hata angeongea tofauti angeloloma!!
 
Corona itadhibiti wingi wa watu duniani, Afrika, na Tanzania!

Kama watu 2000 wanakufa kwa siku, basi kwa wiki tunaweza kusafisha sana nchi!

Dunia inapaswa kuwa katika uwiano baina ya viumbe hai na maliasili!

Corona will do the trick! Watu milioni sitini wote mnataka kwenda wapi!? Vitoto vinazaliwa asubuhi, mchana na jioni! Rundo la watoto wanatotolewa kwa siku!

Tunalalamika maji hakuna, umeme mchache, misitu inakwisha, ardhi zinagombaniwa, chakula kinaisha, ajira zinaisha, wanyama wanakufa na kukimbia makazi, joto na msongamano!

Clearly, the earth has been outweighed and overpowered by the insanely growing population!

Kwa kweli tupungue tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kama nyinyi ndio mnawatia hofu wengine,kama unaogopa sana lala kwako mpaka mwaka itakapoisha covid 19.tuacheni wenye njaa tuingie barabarani tupige kazi.maisha yetu yenyewe ni covid 19.usingojee karantini yakuambiwa jiweke mwenyewe kama kibunda unacho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulitaka adanganye?? Week mbili zijazo tutaju mbivu na mbichi. God bless Tanzania
 
Huu ndio ukweli halisi ambao wavuta bangi wa lumumba hawataki kuusikia
 
Ili tuwe na uhakika bila shaka shaka au uvumi, wachache kati yetu humu JF tujitolee tuvuke mpaka kwenda Kenya. Tutakapopimwa tulete majibu hapa kama tayari tunasambaza Korona ama la.

Tusikimbilie sana kumlaumu Umy Mwalimu kabla hatujajiridhisha.
 
Ulitaka aseme Gentamycine inatibu C19 ndio umuamini kuwa anajenga a Tahadhari kwa Wananchi???
 
Mimi bado naheshimu msimamo wa Rais Magufuli isipokuwa pale wizarani palipaswa kuwa na kiongozi anayeelewa nini maana ya msimamo huu.
Maana yake ni kuwa "tumewatoa kafara nyinyi wachache hapo wizarani muhangaike kwa ajili ya taifa zima".
Kama nchi haiwezi kuwa locked down then waziri wa afya na task force yake yote walipaswa kujua wana kazi nzito sana ya kuhakikisha scale ya maambukizi haiongezeki na uwezo huo ulikuwepo bila shaka,kasoro kubwa tu ilikuwa kuendelea kuruhusu wageni,kutofunga mipaka,na kutokufanya mass testing na uharaka wa kukimbizana na contact tracing na uwezo wa kuishawishi jamii kuona corona ugonjwa wa kawaida na watu kujitokeza kupima,hasa hasa Dar es salaam na care mbovu kwa wale victims na suspects.jinsi wanavyohandle watu,hata mie ningekuja nao pale airport ningewapiga chenga nisiende kwenye hizo "concentration camp" zao zinazolipiwa,bora nikajifungie mahali peke yangu nife kuliko dhahama ile!Sasa ile karantini mtu unaeza kwenda mzima ugonjwa ukaupatia pale pale na ukafa kwa handling yao tu ilivyo.
Natamani ningekuwa karibu na Rais Magufuli nimshauri amtoe huko ughaibuni na kumrudisha wizarani dr.Mpoki Ulisubisya na January Makamba awe naibu wake.
 
Tulitakiwa kujifungia Ndani wenyewe siyo mpaka tufungiwe!
Tushambiwa tuepuke misongamano watu bado wabishi
Tumeletewa level siti wabongo tunalalamika
Mfano Ukienda kko ni business as usual
Muda utaongea..... Any way sir God atuepushe tu na balaaa la mlipuko

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kuna Hoja Kubwa na ya Msingi nimeiona ndani ya Uwasilishaji wako huu japo umeandika kwa Hisia Kali sana zenye Hasira / Jazba.
 
Nilishangaa sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hili umemuonea waziri ummy mwalimu, waziri kasema ukweli mtupu, kitendo cha watu kutoka Tanzania Na kwenda kukutwa Na maambukizi Kenya inaonesha uhalisia Wa tatizo.
 
Mtamlaumu dada ummy bure tu jamani. Ingawa siwapendi ccm lakini dada ummy anajitahidi kwa kiasi chake sema mikono yake ni kama imefungwa. Anaambiwa cha Kusema ilihali mambo ni mabaya. Na yeye kama mwanamke mwenye huruma analiona hilo na ukimuangalia usoni waona kabisa linamsuta but afanyeje sasa!! Ndo amri ishatoka.
Kosa la kwanza ni kuruhusu mikusanyiko ya dini iendelee (hili lilikuwa ni kosa kubwa kutokea kwa nchi hii)
La pili pamoja na huko makansani kuwa na watu wenye maPHD lakini wameshindwa kuzitumia wao kama wao kuwaokoa waumini wao it means SADAKA aka pesa inakuwa na uzito kuliko uhai wa waumini.
Shoo yeye kaamua kunawa kama pilato na zile taratibu alizotoa juzi ingawa bado zitasaidia kwa % chache tu.
Wenzetu zenji kidogo wako serious nasikia kuna misikiti imefunga kabisa.
"USIMJARIBU BWANA MUNGU WAKO"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hili umemuonea waziri ummy mwalimu, waziri kasema ukweli mtupu, kitendo cha watu kutoka Tanzania Na kwenda kukutwa Na maambukizi Kenya inaonesha uhalisia Wa tatizo.

Hivi angesema tokea mwanzo kabisa juu ya hali hii mbaya ya hili Janga la COVID-19 leo hii wenye Kuona mbali Kifikra ( Great Thinkers ) tungeshtuka, tungeogopa na hadi kuhoji hivi?
 

Kwahiyo tunamuonea kwa Kututisha Kwake Jana kuwa huenda kuanzia Wiki ijayo Maiti zikawa nyingi nchini kutokana na kwamba sasa kunaenda kuwa na ' Community Transmission ' tofauti na ilivyokuwa hapo awali? Huyu Waziri wenu amefeli na kila Siku tu Kauli zake zinapishana na Kutuchanganya wengi. Nashangaa kuona wapo Watu wanaomsapoti wakati kwa Mapungufu yake ya Kiutendaji hata Wao wanaweza ' Kupukutika ' Kwa Kufa kama siyo Kufariki kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…