Ndugu wana bodi: Habari ya leo:
Wakati kampeni za uchaguzi wa Tanzania zikiendelea kote nchini nimeona nitoe angalizo kwa wananchi wa Tanzania kwanini Tundu Lissu hafai kuchaguliwa:
1. Akiwa katika Bunge la Katiba, Tundu Lissu alimtukana Baba wa Taifa na kusema kuwa aliishi kwa udanganyifu na uongo. Lakini baadae ameonekana akimsifia mwalimu Nyerere kwenye baadhi ya hotuba zake. Je, amesahau alichosema kuhusu mwalimu Nyerere?
2. Alinukunuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akidai kuwa Tanzania kuna COVID-19 na kwamba Serikali inaficha kuhusu hilo.
Na kwamba haiwezekani Kenya au Uganda kuwe na maambukizi ya virusi vya Corona Tanzania kusiwe na maambukizi.
Lakini ameonekana akiendesha mikutano ya kampeni bila kuvaa barakoa. Je, kwa sasa hakuna Corona kama alivyokuwa anadai au amesahau alichosema?
3. Jana alisema elimu ya Tanzania haina maarifa ya kumsaidia mwanafunzi anayemaliza katika vyuo vyetu. Je na yeye hana maarifa kwani alisoma katika vyuo vya Tanzania pamoja na mkewe?
4. Anasema hakuna demokrasi hapa kwetu Tanzania lakini ndugu huyu yupo CHADEMA na ameshindwa kumshawishi Mwenyekiti wake asiwe Mwenyekiti wa kudumu.
5. Alishiriki katika mkutano wa Mwembeyanga na kudai pamoja na wenzake kuwa Lowassa ni fisadi mkuu. Alibadilika tena na kumnadi LOWASSA kama mgombea urais kupitia CHADEMA. Je, alisahau waliyosema yeye na wenzake kule Mwembeyanga.
Hizi kauli tata za ndugu Tundu Lissu zinatupa wasiwasi na kwa watu makini hawezi kupigiwa kura kwani ana kauli tata.
Huyu hafai kuwa Rais wa Tanzania hata siku moja kwani ni kigeugeu au anasahau aliyoyasema.