Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Kwa hiyo huyo 'Daktari' Samia Suluhu Hassan anamzidi hata Yesu Kristo pamoja na manabii na mitume wote waliomtangulia na kuja nyuma yake ukiachia huyo 'Mtume'? Tunasubiri kusikia hiyo 'past tense' yako Bw. Kawaida. Kumbuka kuwa hata Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na yeye aliwahi kumwamrisha Mungu amshukuru Rais Magufuli eti kwa ile kazi nzuri aliyowafanyia Watanzania.
Mkuu wa Mkoa (RC) Aggrey Mwanri, ila alikuja kusema ile ilikuwa ni 'past participle tense' na haikuwa 'past perfect tense' . Lakini katika hekima yake isiyochunguzika, Mungu alimuita Magufuli na hakuna ajuaye kuwa kama alimuita ili kusudi akamshukuru kule 'mbinguni' au kama alimuita ili amuepushe na 'chawa' wasizidi kumpoteza kwa kumfanya akufuru apokee kufuru au kama aliruhusu watu 'waMmagufuli'! Hiyo itabaki kuwa siri ya Mungu mwenyewe (Kumbukumbu ya Torati 29:29).
Lakini nieambiwa kuwa yule RC sasa ni mmoja wa mabosi wako huko chanikiwiti kama Naibu Katibu Mkuu! Unaweza kumuuliza nini kilitokea baada ya yeye kutoa kauli ile maana ni mzoefu sana katika kupuliza 'saksaoni' katika bendi ya sifa. Ila ninyi huko endeleeni kumzunguka Rais Samia na kauli za kufuru, ila siku kikombe cha ghadhabu ya Mungu kikija kufurika, kitakuja kuwaangukieni nyote!