Mipango inayoandaliwa na watu au taasisi yoyote ile kufanya maandamano ya kumng'oa Kawambwa na naibu wake Mulugo ni haramu na dhaifu. Sekta ya elimu ni pana sana na ufaulu wa mwanafunzi hautegemei kitu kimoja. Waziri sio lazima awe mtaalamu wa wizara anayoiongoza,nafasi yake ni ya kisiasa,yeye anasimamia utekelezajj wa ilani ya chama chake kuhusu suala alilopewa, mathalani waziri wa elimu anadhamana ya kusimamia elimu. Kufeli kwa wanafunzi kunatokana na motisha mdogo kwa walimu,baadhi ya walimu kutokuwa weledi kwenye masomo yao,muamko mdogo wa jamii na wazazi na wanafunzi wenyewe kutozingatia masomo. Aidha serikali imeshindwa kusimamia sekta ya elimu vizuri kwani ingekuwa muujiza kwa mwanafunzi asiejua kusoma afaulu mtihani wa kidato cha nne. Kawambwa yeye ameyakuta haya kwa watangulizi wake. Cha msingi hakuna anayeweza kumnyooshea mwenzake kidole,cha msingi ni sisi kama taifa kukaa pamoja na kutafuta suluhisho,wewe binafsi ulisaidiaje mwanafunzi asifeli? Tushughulike na mambo ya msingi (issues) na sio mtu,ni matumaini yangu jeshi la polisi litapiga marufuku maandamano haya na mwenye akili hawezi kwenda kuandamana hata kama maandamano haya ambayo mimi binafsi nayaona kuwa batili yataruhusiwa.
NAOMBA KUWASILISHA
NAOMBA KUWASILISHA