Kawambwa anaonewa

Kawambwa anaonewa

miemwenye

Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
31
Reaction score
0
Mipango inayoandaliwa na watu au taasisi yoyote ile kufanya maandamano ya kumng'oa Kawambwa na naibu wake Mulugo ni haramu na dhaifu. Sekta ya elimu ni pana sana na ufaulu wa mwanafunzi hautegemei kitu kimoja. Waziri sio lazima awe mtaalamu wa wizara anayoiongoza,nafasi yake ni ya kisiasa,yeye anasimamia utekelezajj wa ilani ya chama chake kuhusu suala alilopewa, mathalani waziri wa elimu anadhamana ya kusimamia elimu. Kufeli kwa wanafunzi kunatokana na motisha mdogo kwa walimu,baadhi ya walimu kutokuwa weledi kwenye masomo yao,muamko mdogo wa jamii na wazazi na wanafunzi wenyewe kutozingatia masomo. Aidha serikali imeshindwa kusimamia sekta ya elimu vizuri kwani ingekuwa muujiza kwa mwanafunzi asiejua kusoma afaulu mtihani wa kidato cha nne. Kawambwa yeye ameyakuta haya kwa watangulizi wake. Cha msingi hakuna anayeweza kumnyooshea mwenzake kidole,cha msingi ni sisi kama taifa kukaa pamoja na kutafuta suluhisho,wewe binafsi ulisaidiaje mwanafunzi asifeli? Tushughulike na mambo ya msingi (issues) na sio mtu,ni matumaini yangu jeshi la polisi litapiga marufuku maandamano haya na mwenye akili hawezi kwenda kuandamana hata kama maandamano haya ambayo mimi binafsi nayaona kuwa batili yataruhusiwa.

NAOMBA KUWASILISHA
 
Miemwenye - cha msingi! cha msingi! Wewe ndie umefilisika kabisa mawazo.

1. Kwanza, wewe sio msemaji wa wizara/waziri/malugo/kawambwa

2.Siamini kama suala la kuwajibika ni suala la mtu binafsi. hili ni suala la waziri mwenye dhamana ya Elimu ya watanzania ikiwa ni pamoja na kushauri kifanyike nini.

3. An act of omission or commission is all offences against citizens of the republic OR Irresponsibility or Incapacity to perform his duties or inefficiency in delivering. Yooote haya au mojawapo linapaswa kumfanya hata anyongwe kwa kitanzi.

4.Kawambwa atakosa ajira, hao waliofelishwa wanakosa MAISHA! Kama sio kawambwa basi wamtoe bosi wake kikwete (tunaweza ingia mtaani tukadai Regime CHANGE vile vile!

5.
 
kwahiyo kiongozi kwa mtazamo wako Kawambwa akiondoka watoto watafaulu? Maana yangu ni kuwa tuhangaike na mfumo na sio mtu.
 
km kawa hata mm nafikiri kufukuzwa kw kawambwa cyo njia sahihi ya kufanikisha ili watt wasfeli b'se kuna sabab nyingine ambazo zikirekebishwa mambo yatakuwa sawia
 
kwahiyo kiongozi kwa mtazamo wako Kawambwa akiondoka watoto watafaulu? Maana yangu ni kuwa tuhangaike na mfumo na sio mtu.

Ili kubadilisha mfumo wa elimu ni lazima kuwe na kiongozi katika wizara ya elimu ambae ataongoza mabadiliko ya mfumo ambao utatuletea tija katika elimu ya nchi yetu na kwa bahati mbaya mtu huyo hawezi kuwa Shukuru Kawambwa kwani hana uwezo huo; hivyo ni lazima tumuondoe ili kufanikisha azma ya kuwa na mfumo wa elimu wenye tija.
 
Ili tuendelee tunahitaji,Kiongozi bora,Hii maana matatizo yote ya walimu,shule,wanafunzi,Alikuwa hafaham?Na kama anafaham alichukua hatua gani?Na matatizo yote wanaolalamika,Walimu,Shule yameamuliwa vipi?Ni kwanini wananchi watake andama kuna tatizo gani""MPAKA SASA MUHESHI WAZIRI AMECHUKUA HATUA GANI,?
 
kwahiyo kiongozi kwa
mtazamo wako Kawambwa akiondoka watoto watafaulu? Maana yangu ni kuwa
tuhangaike na mfumo na sio mtu.

Mkuu,yeye kama waziri husika hakwepi kuwajibika,mbona kina mwakyembe na magufuli wameweza kuuweka sawa mfumo wa wizara zao na mambo swadakta,sasa yeye kipi kinamshinda,kiukweli jamaa hana uwezo wa kuperform ndo maana hata kushauri ama kuondoa uozo hawezi
 
kwahiyo kiongozi kwa
mtazamo wako Kawambwa akiondoka watoto watafaulu? Maana yangu ni kuwa
tuhangaike na mfumo na sio mtu.

Mkuu,haonewi,yeye ndio wa kuubadilisha huo mfumo,hauwezi kushushwa kama quran then tujikute umebadilika,jamaa kwa kuwa sio kichwa kama mwakyembe na magufuli ndo maana hawezi,wizara yake ni nyeti inatakiwa awekwe mtu timamu sio kilaza kama kawambwa
 
Miemwenye - cha msingi! cha msingi! Wewe ndie umefilisika kabisa mawazo.

1. Kwanza, wewe sio msemaji wa wizara/waziri/malugo/kawambwa

2.Siamini kama suala la kuwajibika ni suala la mtu binafsi. hili ni suala la waziri mwenye dhamana ya Elimu ya watanzania ikiwa ni pamoja na kushauri kifanyike nini.

3. An act of omission or commission is all offences against citizens of the republic OR Irresponsibility or Incapacity to perform his duties or inefficiency in delivering. Yooote haya au mojawapo linapaswa kumfanya hata anyongwe kwa kitanzi.

4.Kawambwa atakosa ajira, hao waliofelishwa wanakosa MAISHA! Kama sio kawambwa basi wamtoe bosi wake kikwete (tunaweza ingia mtaani tukadai Regime CHANGE vile vile!

5.

wewe ndo umefilisika mawazo na ubongo wako n mashudu kwa hyo kwa mtazamo wako kawambwa akiondoka wanafunzi ndo watafaulu??

Huyu jamaa nimemwelewa vzur ye anataka 2badilishe mfumo mzma wa elmu na wala c mtu upo hapo!
 
Mkuu,haonewi,yeye ndio wa kuubadilisha huo mfumo,hauwezi kushushwa kama quran then tujikute umebadilika,jamaa kwa kuwa sio kichwa kama mwakyembe na magufuli ndo maana hawezi,wizara yake ni nyeti inatakiwa awekwe mtu timamu sio kilaza kama kawambwa

sasa kama kawambwa n kilaza nani awekwe pale 2kueke wewe?
 
sasa kama kawambwa n kilaza nani awekwe pale 2kueke wewe?

Mkuu Mipale Steve amka bro,haiwezekani mtu afanye vibaya halafu kwa namna yoyote ile atetewe,kutakuwa hakuna maana kwa dhana ya uwajibikaji,naamini wapo wenye mawazo mazuri wangeweza kuisaidia Wizara hii,kwenye mapungufu wangesema na serikali kwa upande wake ingetekeleza yale aliyoyaona na taratibu mambo yangeanza kuwa mazuri,sasa yeye tokea aanze ameshauri nini cha maana ili kuwa na maboresho tunayoyatarajia kwa mustakabali wa nchi yetu tukufu??
 
Back
Top Bottom