Katika hali inayoonekana kuelekea kushindwa kwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chadema, Halima Mdee wafuasi wa chama hicho wamejitengenezea karatasi za kupigia kura zilizotiwa alama ya vema kwa wagombea CCM na kudai eti wamekamata kura hizo za wizi.
Katika video hiyo ya uzushi waliyoisambaza katika mitandao ya kijamii, wanaonekana wafuasi wa Chadema wakilalamika eti kura hizo zimekutwa ndani ya begi la kijana mmoja zikiwa tayari zimempigia kura wagombea wa CCM tena wakiwa na askari.
Swali la kujiuliza; ni kwanini Chadema waliamua kuchoma moto kura hizo badala ta kuhifadhi kama ushahidi? Tafsiri ya jambo hilo ni dogo sana wala halihitaji elimu ya darasani kwamba ni uzushi uliotukuka ambao wamezoea kuutumia na kuudanganya umma ili kupata huruma ya Watanzania kwamba wasiposhinda ionekane waliibiwa.
Basi tufanye ni kura zilizoibwa kweli, swali; kwanini walizichoma wakati ni ushahidi wangeufikisha kwa vyombo husika ili mhusika achukuliwe hatua?
Chadema wako katika hali ya kukata tamaa kwani hawakutegemea watu kujitokeza kwenye uchaguzi huku wale waliokuwa wakijaa katika mikutano wakila kona huku mgombea wa CCM, Askofu Josephat Gwajima akielekea kushinda.
Kwanza wamevunja sheria kwa kukaa kituoni baada ya kupiga kura halafu wanajisingizia uongo.
Chadema watulie dawa iwaingie wasubiri kura zihesabiwe na wakubali matokeo wala wasijaribu kuleta vurugu na kutafuta huruma za Watanzania waonekane walionewa.