Uchaguzi 2020 Kawe ina heshima tayari, inahitaji maendeleo

Nani kakudanganya? Mnadhani hii nchi ni ya kwenu peke yenu?
Ni wazi kuwa Gwajima anakubali Asilimia zote Huyo Bibi atafute tu cha kufanya tukutane viti maalumu
IMG-20201008-WA0047.jpg
 
Wewe wamekunyima hata mmoja wa majaribio, huyo wa kumi amekubalika na bado anakubalika, baada ya mitano take inayokuja , atakuunga mkono iwapo utabadili mawazo na kuja chama Bora zaidi.
Chama bora ndo kipi hcho[emoji57][emoji57]
 
Sio siri kabisa. Gwajima hana maadili kabisa ya kuwa kiongozi wa jamii. Hata familia yake haiwezi. Amemvunjia heshima mkewe na watoto, jimbo ataliweza? Amevunjia heshima Kanisa lake sembuse jimbo?

Alimvunjia Kadinali pengo heshima na kumtukana, akawavunjia heshima Waislamu kwa kutamka kuwa ana maono ya kugeuza misikiti kuwa vituo vya Sunday school.

Hii ni kashfa kwa Waislamu ambayo haiwezi kufumbiwa macho. Nakubali kuwa Kawe inahitaji heshima kwa kuwa kunaishi waheshimiwa na Halima Mdee ndiye pekee amedhihirisha kubeba dhamana hiyo.

Halima ni msomi wa sheria. Halima ni mwanamke ambaye anapohutubia mwenye akili yeyote atakubaliana na mantiki ya hotuba yake. Huwezi kumdharau.

Amejitambulisha katika jamii kama mwanamke kiongozi shupavu na mtetezi hodari wa kile anachokiamini. Alisimamishwa ubunge kwa kama nusu ya muhula mzima eti kwa sababu ya kusema tu bunge ni dhaifu. Alipigwa na kuvunjwa mkono kwa maonevu tu na reaction yake ikawa, no fear, no hate.

Akiwa mbunge wa Kawe wana Kawe watazidi kuheshimika.
Ni kweli kuwa Kase kama ilivyo majimbo yote inahitaji maendeleo. Maendeleo hayeletwi na mbunge bali serikali.
Yan umekaa unaandika ujinga huu kweli huna akili
 
..Mawaziri wanaishi hukohuko halafu maendeleo hayapelekwi?

..hapo ccm walihujumu maendeleo ili waje wamlaumu Halima Mdee.

..Na waliokuwa wakimfukuza na kumfungia Halima asihudhurie vikao si Spika na wabunge wa ccm?

..Je, mawaziri na viongozi wa ccm ambao wanawakilishwa na Halima Mdee walimtetea mbunge wao asifungiwe kuhudhuria vikao?
Kama mtu hana adabu ufanyweje kwa ufupi yule mama hana adabu kabsa bungeni huwezi mtukana kiongozi wako na asikuchukulie hatua
 
KAWE INA HESHIMA TAYARI, INAHITAJI MAENDELEO

Je, ni kweli Kawe inahitaji heshima?

Jimbo la Kawe ni moja kati ya majimbo muhimu sana hapa Dar es Salaam.
Kule Masaki na Oysterbay wanakaa watu muhimu katika taifa. Mabalozi wengi wanakaa jimbo la Kawe.

Vitengo muhimu kwa ustawi wa nchi viko kwenye jimbo la Kawe.

Kwa upande wa makazi pia, maeneo ya Mbezi Beach, Mikocheni, Bunju, Goba, Salasala, Madale yote haya yamejaa watu wa maisha ya kati na juu ambao wana mchango mkubwa katika taifa hili. Haimaanishi watu wengine sio muhimu, kila mtu ni muhimu kwa kiwango chake kulingana na nafasi aliyopo.

Kwa mtazamo huu, jimbo la Kawe tayari lina heshima. Jimbo la Kawe halikutakiwa kuwa jimbo la watu wanaolalamika kwa kukosa huduma muhimu kama barabara za ndani, hospitali na maji. Kawe ina heshima ndio maana wakazi wa huko wamekuwa wastaarabu sana kipindi hiki chote cha miaka 10.

Kwa heshima iliyonayo jimbo la Kawe, mwakilishi wake angekuwa ameweka mbele maslahi ya jimbo lake kwa kutanguliza hoja za wananchi na sio kulalamika bungeni na kugoma.

Yaani baada ya miaka 10 Mdee ndo amejua kuwa Kawe inahitaji heshima?

Heshima gani wakati watu hawana maji kule Ndumbwi?

Heshima gani wakati madaraja hayajaisha huko Boko? Mbezi Beach na Mbezi juu imejaa barabara za vumbi? Heshima gani hiyo?

Heshima gani wakati fedha za mfuko wa jimbo zimetafunwa?

Heshima gani wakati mwakilishi aliyechaguliwa na watu wa Kawe anaongoza migomo bungeni?

Watu wa Kawe wana heshima, ila kwa aliyoyafanya Mdee kwa miaka 10 amewadharau sana.

Watu wa Kawe msirudie makosa haya.
Mmemstahi sana huyu Mdee kwa miaka hii 10.

Safari hii mchague Askofu Gwajima mtu makini anayejua wanachohitaji wananchi wa Kawe.

Ni wakati wa kuachana na longo longo na kuchagua mtu jasiri, hodari, mchapakazi na mpenda maendeleo atakayeishawishi serikali kuleta maendeleo kwenye jimbo la Kawe.

Wanakawe achaneni na Mdee, hajawaheshimu miaka 10 yote hii, ataweza kwa miaka hii mitano (5)?

Mchague Gwajima kwa maendeleo ya Kawe na Magufuli kwa Maendeleo ya Tanzania atunze heshima mliyonayo.

Salum Kipanga
Mbezi - Mtoni,

Jana nimehudhuria kampeni za Gwajima pale wanja wa magunia Msasani. Kwa kweli hata Gwajima hajui anaomba kazi gani. Halafu matusi hasa ya yule anaegombea udiwani nashindwa kuelewa hivi CCM imeishiwa na watu?
Mdee chapa kazi hawa ni wale wanaolipwa buku tano tano na CCM.
 
..serikali nzima na wakubwa wote nchi hii wanaishi jimbo la kawe.

..sasa ilikuwaje wasipeleke maendeleo huko? au walikuwa wakifanya hujuma?

..fedha za mfuko wa jimbo matumizi yake yanasimamiwa na mkurugenzi wa wilaya, ambaye ni mteule wa ccm.

..Tuikatae ccm kwa kulibagua kimaendeleo jimbo la kawe.

..Tumkatae Gwajima kwasababu ni TAPELI. Aliahidi kumfufua Amina Chifupa. Aliahidi kununua treni. Atimize ahadi hizo kwanza ndipo tuamini kwamba anaweza kutimiza ahadi za ubunge.
Ni nani muwakilishi wa wananchi kumbuka wananchi walimchagua ili awawakilishe kule bungeni lakin halima hajawahi kufanya hvyo zaid ya kutukana na kutetea chama chao hao mawaziri hawajachaguliwa na wananchi acha ufala wewe angefanya kazi yake kwa bidii zote
 
Jana nimehudhuria kampeni za Gwajima pale wanja wa magunia Msasani. Kwa kweli hata Gwajima hajui anaomba kazi gani. Halafu matusi hasa ya yule anaegombea udiwani nashindwa kuelewa hivi CCM imeishiwa na watu?
Mdee chapa kazi hawa ni wale wanaolipwa buku tano tano na CCM.
Hawana sera kabisa hawa wameishiwa pumzi
 
KAWE INA HESHIMA TAYARI, INAHITAJI MAENDELEO

Je, ni kweli Kawe inahitaji heshima?

Jimbo la Kawe ni moja kati ya majimbo muhimu sana hapa Dar es Salaam.
Kule Masaki na Oysterbay wanakaa watu muhimu katika taifa. Mabalozi wengi wanakaa jimbo la Kawe.

Vitengo muhimu kwa ustawi wa nchi viko kwenye jimbo la Kawe.

Kwa upande wa makazi pia, maeneo ya Mbezi Beach, Mikocheni, Bunju, Goba, Salasala, Madale yote haya yamejaa watu wa maisha ya kati na juu ambao wana mchango mkubwa katika taifa hili. Haimaanishi watu wengine sio muhimu, kila mtu ni muhimu kwa kiwango chake kulingana na nafasi aliyopo.

Kwa mtazamo huu, jimbo la Kawe tayari lina heshima. Jimbo la Kawe halikutakiwa kuwa jimbo la watu wanaolalamika kwa kukosa huduma muhimu kama barabara za ndani, hospitali na maji. Kawe ina heshima ndio maana wakazi wa huko wamekuwa wastaarabu sana kipindi hiki chote cha miaka 10.

Kwa heshima iliyonayo jimbo la Kawe, mwakilishi wake angekuwa ameweka mbele maslahi ya jimbo lake kwa kutanguliza hoja za wananchi na sio kulalamika bungeni na kugoma.

Yaani baada ya miaka 10 Mdee ndo amejua kuwa Kawe inahitaji heshima?

Heshima gani wakati watu hawana maji kule Ndumbwi?

Heshima gani wakati madaraja hayajaisha huko Boko? Mbezi Beach na Mbezi juu imejaa barabara za vumbi? Heshima gani hiyo?

Heshima gani wakati fedha za mfuko wa jimbo zimetafunwa?

Heshima gani wakati mwakilishi aliyechaguliwa na watu wa Kawe anaongoza migomo bungeni?

Watu wa Kawe wana heshima, ila kwa aliyoyafanya Mdee kwa miaka 10 amewadharau sana.

Watu wa Kawe msirudie makosa haya.
Mmemstahi sana huyu Mdee kwa miaka hii 10.

Safari hii mchague Askofu Gwajima mtu makini anayejua wanachohitaji wananchi wa Kawe.

Ni wakati wa kuachana na longo longo na kuchagua mtu jasiri, hodari, mchapakazi na mpenda maendeleo atakayeishawishi serikali kuleta maendeleo kwenye jimbo la Kawe.

Wanakawe achaneni na Mdee, hajawaheshimu miaka 10 yote hii, ataweza kwa miaka hii mitano (5)?

Mchague Gwajima kwa maendeleo ya Kawe na Magufuli kwa Maendeleo ya Tanzania atunze heshima mliyonayo.

Salum Kipanga
Mbezi - Mtoni,

Tunaenda na mwamba Iron Lady na siyo pornstar/cum bishop mzee wa pornhub...
1602166198942.png
 
Jana nimehudhuria kampeni za Gwajima pale wanja wa magunia Msasani. Kwa kweli hata Gwajima hajui anaomba kazi gani. Halafu matusi hasa ya yule anaegombea udiwani nashindwa kuelewa hivi CCM imeishiwa na watu?
Mdee chapa kazi hawa ni wale wanaolipwa buku tano tano na CCM.
Acha kabsa kupotosha Umma jana Gwajima alikuwepo Bonde la mpunga na wala hakuna mtu hata mmoja aliyetukana kwa vile mmezoea kutukana nyie chadema msifikiri ya wenzenu wako hvyo sema utawafanyia nin wananchi wako sio maneno ya kuwaponda wengine paka wewe
IMG-20201007-WA0107.jpg
 
Jana nilienda wanja wa magunia kumsikiliza Gwajima na mgombea udiwani pale Msasani.
Gwajima sijui hata anafahamu kazi anayoomba
Hahaha eti uwanja wa magunia wewe kweli akili zako ziko matakoni huwezi kumuelewa
IMG-20201006-WA0032.jpg
 
Lazima tumchague Gwajima maana wanaKawe tushachoka na kero tulizonazo kwa miaka mingi sasa imetosha tunataka maendeleo na mabadiliko

unaenda kulichagua jitu la ccm tena daaah ? aisee hii nchi ina ungese wa kiwango cha lami, yan mtu alikuwa anawazaba mitusi na kila kitu leo kawa mwema leo anaweza kuleta maendeleo aiseeeee
 
Ni nani muwakilishi wa wananchi kumbuka wananchi walimchagua ili awawakilishe kule bungeni lakin halima hajawahi kufanya hvyo zaid ya kutukana na kutetea chama chao hao mawaziri hawajachaguliwa na wananchi acha ufala wewe angefanya kazi yake kwa bidii zote

..Mawaziri kama Dr.Ndalichako, Dr.Makame Mbarawa, Dr.Philip Mpango, wote ni madiwani wa manispaa za Dsm.

..kama wanaruhusiwa kushiriki vikao vya madiwani, basi wanawajibika kuwasemea na kuwaletea maendeleo wananchi wa Kawe.

..kilichotokea hapo ni HUJUMA tu, na wananchi wanatakiwa wakatae uhuni huo.
 
Tulimchagua Halima hvyo angetuwakilisha alafu wewe unayeongea hvyo umesoma Ilan ya utekelezaji 2015-2020 hzo hela alitolea wapi ndo maana tunasema ameandika uongo mtupu akijifanya eti kawe inahitaj Heshima heshima Gani aliyoleta kawe
 
unaenda kulichagua jitu la ccm tena daaah ? aisee hii nchi ina ungese wa kiwango cha lami, yan mtu alikuwa anawazaba mitusi na kila kitu leo kawa mwema leo anaweza kuleta maendeleo aiseeeee
Ni wazi kuwa Halima hawez kutuwakilisha Bungeni hvyo hatuwezi kamwe kurudia matapishi sisi ndo wakazi wa kawe na hali zetu tunazijua ni bora mara kumi kumchagua Gwajima kuliko huyo domo zege
 
Tulimchagua Halima hvyo angetuwakilisha alafu wewe unayeongea hvyo umesoma Ilan ya utekelezaji 2015-2020 hzo hela alitolea wapi ndo maana tunasema ameandika uongo mtupu akijifanya eti kawe inahitaj Heshima heshima Gani aliyoleta kawe

..inaelekea hufahamu utaratibu wa matumizi ya fedha za mfuko wa maendeleo wa jimbo.

..mbunge na madiwani wanawajibika kuzipangia fedha matumizi kulingana na maombi ya wananchi na vipaumbele mbalimbali.

..baada ya kikao cha mbunge na madiwani kuamua fedha zitumike ktk mradi gani, au zigawiwe kwa kikundi gani, MKURUGENZI WA HALMASHAURI hutoa fedha hizo, na husimamia kuhakikisha zimetumika kwa malengo yaliyowekwa.

..Kwa hiyo kama fedha zimetumika vibaya, au hazikuwafikia walengwa, anayepaswa kulaumiwa ni MKURUGENZI na siyo mbunge. Utaratibu huo upo ktk majimbo yote hata yale yaliyochagua wabunge wa CCM.
 
Back
Top Bottom