Uchaguzi 2020 Kawe kunani? Why is a hot cake? Wamejitokeza wagombea 176! What is so special ? Kuchinja watu 175 kubaki 1, is not a joke!.Je, atakuwa nani?

Mimi nashauri kila chama kitoe idadi na majina ya waliochukua form za kugombea kwa kila jimbo na kata kabla na baada ya kura za maoni Yani mchujo kafanyika.

Hii itakuwa Nzuri sana na Ndiyo modernization yenyewe!

Kina bwana Polepole Naomba ifanyieni kazi hii.
 
Gwajima ana nafasi kubwa ya kushinda. Nimeona mdogo wake Gwajima kachukua Kawe na yeye. Anamponda kaka yake balaa.
Gwajima hawezi kushinda kwani jimbo la Kawe zaidi ya asilimia 70 ni waislamu. Hata yeye hilo analijua na anajihangaisha tu!
 
Nenda kapambane, all the best.
 
Kawe kumelipuka kwa sababu ya mbunge aliyepita, naona alikuwa hatoshi na watu wamechoka ngonjera.
 
Gwajima hawezi kushinda kwani jimbo la Kawe zaidi ya asilimia 70 ni waislamu. Hata yeye hilo analijua na anajihangaisha tu!


Sasa hapo unatakakuleta agenda ya Udini ambayo haileti faida bali hasara tupu!

Kwani mbunge anachaguliwa kutoa mawaidha au kuwakilisha wananchi bungeni na kutunga sheria na kuisimamamia na kuishauri serikali kwenye maswala ya wananchi?!

Yani leo hii mfano agombee Shekhe Issa Ponda ambae watu wanajua kuwa ni mfuatiliaji wa mambo watu wamkatae kwa kuwa muislam na jimbo alogombea lina wakristo wengi?

Mgombea hata akiwa mpagani haijalishi cha msingi ni kujiridhisha uwezo wake wa kufanya kazi na kuleta matokeo chanya kwa manufaa ya wananchi wa jimbo na Taifa kwa ujumla.

Yani umenishangaza sana sikutegemea hata kidogo mtu aje na mawazo kama yako.
 
Gwajima hawezi kushinda kwani jimbo la Kawe zaidi ya asilimia 70 ni waislamu. Hata yeye hilo analijua na anajihangaisha tu!


Hizo taarifa za takwimu umezipata wapi?

Zina usahihi kiasi gani?

Kwa hiyo tuangalie kwenye Taifa letu dini gani wako wengi ndipo wale wenye dini yenye wengi wawe wanatoa Rais na wabunge au?

Aisee umenishangaza sana!


Mimi hata kama ni akigombea mbunge wa dini isiyo yangu sijali ili mradi atatimiza majukumu yake kwa ufanisi.

Tukatae udini
Tukatae ukabila
Tukatae itikadi

Tukatae kwa nguvu zote.
 
Kwa idadi hiyo ya wagombea hapo kawe atakayepita anatosha kuwa hata mkuu wa nchi kama akipatikana kwa sifa,vigezo na weledi.

Lakini suala la wagombea binafsi linaumuhimu sana kwa sasa.

Sijajua kwa nini linapingwa,maana ligesaidia sana kuipunguzia serikali gharama za ruzuku.
 
Gwajima ana ugomvi mkubwa sana na waislamu na yeye ndiye aliyeuanzisha. Sijaandika hapa kwa bahati mbaya na ndiyo maana sijamtaja mtu mwingine zaidi ya Gwajima.
 
HAPANA. Yupo Moshi anakula u DC

Kippi hayupo Moshi na juzi Mama Mgwira kamuapisha DC Mpya kuchukua nafasi ya Kippi

Yule Mzee aliyevaa masuti mekundu alikua CCM ana miaka 55 analipwa laki 6 eti

JPM bwana🤣🤣
 
Nimeshakujibu kwenye post yako nyingine.
 
Gwajima hawezi kushinda kwani jimbo la Kawe zaidi ya asilimia 70 ni waislamu. Hata yeye hilo analijua na anajihangaisha tu!


Kuna mataifa yako kwenye G20 kwa maendeleo ya sayansi na viwanda na wala hawana dini zozote [emoji108][emoji108]

Yani ukiwambia Habari ya kwamba kuna Mungu na kutakuwa na Kiyama ya wafu wala hawatakuelewa sana sana watakuona chizi!

Sasa kama dini inamsaidia mtu kupata maendeleo Ulaya kiuchumi si wangekuwa maskini wakutupa?

Sisi hizi dini zilizofanywa kuletwa zinamchango gani katika kuleta maendeleo?

Kufanya kazi kwa bidii na maarifa ndiko kunakoleta maendeleo endelevu bila kujali dini ya mtu [emoji108][emoji108][emoji108]

Eti mtu mvivu hataki kuamka alfajiri kwenda kufanya kazi halafu anaamini umaskini ni mapenzi ya Mungu [emoji4][emoji4] Jamani inashangaza sana!

Mungu huyo huyo ameagiza watu wafanye kazi , kazi hufanyi halafu umaskini ukikukabili umasema ni mapenzi ya Mungu?!
 
Umewaza nini mzee,maana sio sababu ya lawama unazotaka kuandaa dhidi ya watia nia.

Huo ni udikteta wa kung'ang'ania yale unayoamini.
 
Gwajima ana ugomvi mkubwa sana na waislamu na yeye ndiye aliyeuanzisha. Sijaandika hapa kwa bahati mbaya na ndiyo maana sijamtaja mtu mwingine zaidi ya Gwajima.


Ugomvi gani ?

Hebu elezea hapa tuweze kufahamu.

Vinginevyo utachukuliwa kuwa mtu unayetaka kuleta fitina na uzushi ili kumfarakanisha Gwajima na watu hao unaotaja kitu ambacho hakitaweza kumkwisha Gwajima.
 
Ugomvi gani ?

Hebu elezea hapa tuweze kufahamu.

Vinginevyo utachukuliwa kuwa mtu unayetaka kuleta fitina na uzushi ili kumfarakanisha Gwajima na watu hao unaotaja kitu ambacho hakitaweza kumkwisha Gwajima.
Alisema atazigeuza madrasa zote ziwe Sunday school! Tena aliongea hivyo madhabahuni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…