Ndugu Paskal, unastahili na unaimudu sana hiyo kazi. Pia maoni yangu ni kuwa ukichaguliwa hutakuwa mbunge wa RUBBER STAMP, utasimamia haki na utawatumikia wana Kawe bila ubaguzi na utaweza kuishauri serekali vizuri.Wanabodi,
Declaration of Interest.
Mimi Paskali Mayalla ni mkazi wa Kawe, nimezaliwa Kawe, nimesoma primary Kawe, nimesoma sekondari Kawe, nimehudhuria JKT kambi ya Mlalakuwa, nimesoma Chuo cha uandishi wa habari IJMC pale Makumbusho, nimeajiriwa TVT pale Bamaga, nimeoa Kawe, naishi Kawe, na sasa nimestaafu rasmi na kurejea nyumbani Kawe, hivyo mimi ni Kawe na Kawe ni mimi!.
Pazia la kujaza fomu za ubunge na udiwani za CCM limefungwa rasmi leo saa 11:00 jioni, jimbo la Kawe, wamejitokeza wagombea 176!, ambapo wagombea 175 watakatwa na atabaki mmoja. Kuchuja wagombea 176 ili kumpata mmoja, it's not a joke, na akipatikana huyo mgombea mmoja, he/she must be the best of the best.
Swali ni Kawe kunani hadi jimbo liwe hot cake namna hii?. Watu 176 kugombea nafasi moja!, this is not normal, haijapata kutokea!, what is so special about Kawe hadi wapigane vikumbo hivyo?!.
My Take.
Vikao vya maamuzi vya CCM, vitakuwa na kazi kubwa ya ziada ya kuchuja wagombea 176 ili kumpata mgombea mmoja bora, kuliko wote, na akipatikana, he/she will be the best of the best!.
Nashauri wale wagombea wengine 175 watakao chinjjwa, sasa ndio wawe wajumbe wa Kamati ya kujitolea ya ukombozi wa jimbo la Kawe.
Ili kuirahisishia kazi vikao vya mchujo, majina ya wagombea yakiwekwa hadharani, tusaidie kuwafanyia vetting by elimination wale tunaowajua kuwa sio ili jimbo la Kawe lipate Mbunge bora zaidi ya aliyepo.
Kwa vile mimi ni mkazi wa Kawe, na wana Kawe sio wale watu wa type ya t-shirt na kofia, na shibe ya siku moja, vikao vya uteuzi vya CCM vikifanya tena makosa yale yale ya kututeulia wagombea wenye majina makubwa lakini hawana uwezo wa kujieleza na hawana mvuto, wana Kawe kama kawaida yao...
Naomba nisimalizie.
CCM Oye!
Paskali
Kwa KUDRA ZA ALLAH SUBHANA WA TAALA Utachaguliwa na utakapopewa shahada ya mgombea wa CCM, bila unafiki wa kichama, sisi wana JF tutaka tukuapize hapa jukwani na utuapie kuwa utautumikia ubunge wako 1st kwa wana kawa 2nd Watanzania wote, na hutakuwa mpambe wa kijinga kama kina Bajaj, msukuma na wengineo.
Pia ni tegemeo langu kuwa utakitumikia chama chako vizuri sana na kutoa ushauri mzuri bila uoga wowote, NGUMI YA MSUKUMA HALISI HAIRUDI NYUMA.