Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Wanakawe wote kwa umoja wetu bila kujadi itikadi zetu tujitokeze kwa wingi wetu tarehe 28.10.2020 tuendelee na sauti adimu ya Zege. Tunahitaji mtu wa kwenda kutusemea na siyo mtu wa kwenda kupiga meza.
Anayeitwa askofu hata kura za maoni alishika nafasi ya 3, maana yake hakubaliki hata ndani ya CCM.
Zipo sababu zaidi ya 200 za kumchagua Halima Mdee lakini hapa naweka baadhi yake 10 tu.
1. Ni mwanamke shupavu
Kwanza Halima ni mwanamke asiyeogopa,jasiri asiyeangalia uso wa mtu. Mfano wa kuigwa na jamii yote. Haisemei KAWE tu huyu ni mbunge wa taifa.
2. Halima Mdee ni msomi na mchapa kazi
Elimu ya Mdee ni ya sheria na siyo ya mambo ya kawaida kama ya yule jamaa. Anao uwezo mkubwa wa sheria na amekua mchango mkubwa katika miswaada mbali mbali ya kisheria inayoenda bungeni.
3. Ana maono
Halima Mdee amekua mbunge mwenye maoni katika kuibadili KAWE, amepita katika wakati mgumu sana wa kusimamishwa bunge kwa sababu ya misimamo yake isiyoyumba.
4. Halima Mdee siyo mbaguzi
Halima Mdee siyo mbaguzi wa Kabila,Rangi, dini wala kanda anakotoka mtu, huyu ni mwakilishi wa wananchi wote na amekua akiishi hivyo.
5. Msemakweli
Halima Mdee kwake nyeusi ni nyeusi tu haiwezi kubadilika ikawa nyeupe.Atakuambia ukweli bila kupepesa macho
6. Mzoefu katika siasa za Tanzania
Halima Mdee ni mzoefu sana katika siasa za Tanzania, ameingia bungeni tangu mdogo sana. Haendi kujaribu ubunge,huyu ni mwakilishi tayari.
7. Amekua msemaji wa wananchi
Wa wanakawe na taifa kwa ujumla. Halima Mdee amekua msemaji wa shida za wananchi na siyo mtu wa kupiga meza tu.
8. Mtetezi wa Mtoto wa Kike
Halima Mdee kama utakumbuka vizuri akiwa na kadhi kadhi ya kutiwa ndani na kupelekwa mahakamani akitetea haki ya mtoto wa kike kurudi shule akipata ujauzito. Hili suala lilichukuliwa simple sana hasa na watu wa CCM lakini wengi walikua wakimfuata Halima Mdee nyuma ya pazia awatetee.
9. Anajiamini sana
Halima Mdee ni aina ya wanasiasa vijana wasiotumia. Anafanya kazi kwa kufuata anayoyaamini, hana usanii kama wengine.
10. Mwadilifu
Halima Mdee ni nembo ya wanawake waadilifu wasiokua na shaka. Hana kashfa za rushwa wala wala kutumia vibaya rasilimali za jimbo zikiwemo pesa za mfuko wa jimbo.
Kwa ujumla kumwelezea huyu dada hadi kumaliza utaweza kujaza kitabu kizima kumuandika. Huyu ndiye mwakilishi sahihi wa wananchi wa jimbo la KAWE.