Kazi[Careers] zenye future na maslahi mazuri Tanzania

Kazi[Careers] zenye future na maslahi mazuri Tanzania

Hizo fani ulizoandika hapo zote zinapatikana bongo?
Je kwa kijana anayemaliza kidato cha 4 afu yuko vizuri kitaaluma, unamshauri asome comb gani form 5?
Nivizuri useme yupo vizuri kwenye Saiyansi (Physics, Chemistry, Biology na Mathematics) au Yupo Vizuri kwenye Arts; yaani History, Kiswahili, English na Geography
Ukisema yupo vizuri tunategemea kwa saiyansi; hana pass chini ya C; na kwa arts hana pass chini ya B.
Kama amefauli yote vizuri; Aende PCM ambayo itampa fursa ya kusoma kozi zote tajwa hapo juu au PCB kama anapenda mambo ya uhai na mazingira)
Kama Arts asome HGE kwani Geography & English bado ina fursa japo sio nyingi kama saiyansi
 
Wewe mleta mada ni mpuuzi mmoja tu,, Hao watu umetaja hapo watakuwa wanakula hizo ict?

Kazi yenye future endelevu milele na milele ni Agricultural sciences. People must eat. Control food, control everyone. Popoma wewe
 
Kumbe kuna watu bado wana ndoto za kuajiriwa, careers na security na bado mnaamini uwepo wa neno "soko la ajira" kama kipindi kile shule ya msingi wakati watu wanaamini njia pekee ya kufikia mafanikio ni kuajiriwa au kufa masikini.

Lakini ndio vizuri sababu bila ya work force na employees basi itakuwa ngumu kufanikiwa sababu hautoweza kufanya kila kitu peke yako kazi nyingine zinahitaji wafanyakazi wengi na loyal, besides kila mtu akijiajiri na kuwa boss au CEO then nani atamuajiri, atafanya kazi na kumtumikia mwenzake?

Hivyo kufikiria ajira, career na job security ni kitu kizuri.
 
Mzaleee zimejaa online unasoma na kufanya mtihani online mf.microsoft excel expert ni around $150 na CompTA Network+ ni $381.N,k
->IT ni pana sana so inategemea na eneo unalotaka kujikita zaidi.
 
Msisahau sekta ya Wanyamapori na maliasili zake,zinalipa sana tena sana nadhani ni sekta ambayo imeajiri vijana wengi wa Kitanzania kuliko sekta yoyote kwa ninavyofikiria mimi,sekta hizi ni kama Tanapa,Ncaa,Tawa, TFS (misitu),ambazo ndo chanzo pia cha makampuni ya kitalii,mahoteli n.k ambayo pia yameajiri watu wengi na salary na marupurupu ni matamu ambayo yanamfanya mtumishi hasitamani kuacha kazi.
Na walio wengi wamepata elimu ya kawaida sana aidha baada ya kumaliza o'level,six na kuongezea Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Mwanza au MWEKA Moshi au Taaluma kama hiyohiyo au Utabibu wa Wanyamapori toka SUA.
Sekta binafsi unakuta dereva/tourguide kapiga Pasiansi au MWEKA halafu kapiga lugha za ziada mf,Kijurumani,Kijapani,Kichina n.k,kajipatia leseni sahihi toka VETA/NIT nakwambia mtu huyo mwenye PhD hamfikii kwa maisha bora.
So msiwaze kusoma sana ndo kutoboaa wazee.Goodmorning
 
Wewe mleta mada ni mpuuzi mmoja tu,, Hao watu umetaja hapo watakuwa wanakula hizo ict?

Kazi yenye future endelevu milele na milele ni Agricultural sciences. People must eat. Control food, control everyone. Popoma wewe
Kilimo duniani ila siyo Tanzania. Kilimo kwa Tz hakina tija kuanzia mazingira ya kujiajiri hadi kuajiriwa. Agricultural policy iliyopo ni ya kwenye makaratasi tuu
 
Back
Top Bottom