Kazi[Careers] zenye future na maslahi mazuri Tanzania

Kazi[Careers] zenye future na maslahi mazuri Tanzania

University of dar es salaam.
Mkuu nimefuatilia hizo professional mbili za afya ulizoweka,moja ni IT na nyingine ni economics ila tu kwenye mambo ya hospital.....am medical personnel,nina talent and am so good...kuniambia leo hii nikasome IT au economics hell no,siko interested....Nadhan talent ziheshimike,imagine wazazi wake Kibatala wangemshawishi asomee uhasibu au wazazi wa Maxence melo wangeforce kuwa Bwana afya....Nashukuru kwa heads up lakini vipaji viheshimiwe na kila taaluma ina umuhimu wake...Ukisema usome kwa kufuata mafanikio yapo wapi utaishia kukimbiza mafanikio maisha yako yote,ukisoma kufuata unachoweza na kukipenda mafanikio yatakukimbilia.
 
Gen Lu Bu wengi hawaangali hicho wanachotaka ni wewe kujifunza kwa vitendo zaidi hands on experience,bongo unakuta mtu ana bachelor ya IT lakini ni mweupe
Vizuri, Katika kuelewa taaluma fulani inahitaji kuwa na msingi wa taaluma hiyo. Sasa katika kusomea hivi vyeti haitakua na ugumu wa kuelewa yanayofundishwa sababu ya kukosa msingi wa IT?. Nifahamishe zaidi ninahitaji kumshauri mtu juu ya hili.
 
  • Thanks
Reactions: Sax
Wewe mleta mada ni mpuuzi mmoja tu,, Hao watu umetaja hapo watakuwa wanakula hizo ict?

Kazi yenye future endelevu milele na milele ni Agricultural sciences. People must eat. Control food, control everyone. Popoma wewe
Ndio maana ulifeli shule. Husomi unadandia tu dudu. Wewe kwa kuwa huna akili huwezi kuelewa chochote hapo. Utabaki maskini. Tanzania mnalima nyie? Hizo kwanza dunia nzima unafanya kazi kwa taarifa yako. We unauwezo wa kulima? Unajua kulima au unabwata tu.? Akili kubwa haziitaji kutumia nguvu nyie kalimeni tutakupa. Alafu skuingine uache kudandia vitu usichoelewa. Kinyeo wewe.
 
Huwe
Mkuu nimefuatilia hizo professional mbili za afya ulizoweka,moja ni IT na nyingine ni economics ila tu kwenye mambo ya hospital.SIWEZI KUSOMA HUO UPUPU....am medical personnel,nina talent and am so good...kuniambia leo hii nikasome IT au economics hell no,siko interested....Nadhan talent ziheshimike,imagine wazazi wake Kibatala wangemshawishi asomee uhasibu au wazazi wa Maxence melo wangeforce kuwa Bwana afya....Nashukuru kwa heads up lakini vipaji viheshimiwe na kila taaluma ina umuhimu wake...Ukisema usome kwa kufuata mafanikio yapo wapi utaishia kukimbiza mafanikio maisha yako yote,ukisoma kufuata unachoweza na kukipenda mafanikio yatakukimbilia.
Unaziita UPUPU? Sasa upupu ni hiyo njia ndefu unayopita. Unatumia nguvu nyingi kuwa wa kawaida. Ni matumizi mabaya ya ubongo. Hizo profession hutokesha kazini, hutorukiwa na damu au usaa. Hutogombana na wananchi kirahisi. Hutopoteza muda mwingi sehemu moja, ni suala la akili tu.
 
Huwe

Unaziita UPUPU? Sasa upupu ni hiyo njia ndefu unayopita. Unatumia nguvu nyingi kuwa wa kawaida. Ni matumizi mabaya ya ubongo. Hizo profession hutokesha kazini, hutorukiwa na damu au usaa. Hutogombana na wananchi kirahisi. Hutopoteza muda mwingi sehemu moja, ni suala la akili tu.
Samahani mkuu sikupaswa kuita taaluma ya watu wengine upupu,mengineyo tukubali kutokubaliana.
 
Vitu vya kuzingatia;
•Unapendelea nini (Passion/Interest)
•Unaujuzi gani (Skills/knowledge)
•Utapataje pesa (Market demand)
 
Katika karne hii ya 21, kijana mwenye maarifa na maono atakuwa anafahamu kuwa bila kuchagua career sahihi maisha yatakuwa magumu.

Ninaposema taaluma au Careers nzuri, maslahi japo ndio la kwanza lakini pia kuna kitu kinaitwa quality of life au tuseme work-life balance.

Yani unaweza kufanya kazi inayokulipa karibu 5m kwa mwezi lakini inakutumia zaidi ya masaa 10 kwa siku wa zaidi ya siku 5 au 6 kwa wiki.

Hapo maana halisi ya kuishi inakuwa haina maana kama kazi unayofanya itakutenganisha na ndugu jamaa na marafiki na pia mambo ambayo unayapenda nje ya kazi.

Tofauti na mtu anayelipwa laki 8 lakini anafanya masaa 8 kwa siku 5 au pungufu.

Kwa hivi sasa, kazi ambazo ni nzuri zimekuwa 'overlooked' kwasababu ya mazoea, yani tumezoea udaktari, uanasheria, uhandisi nk ndio zinaonekana kazi. Lakini muda wa dhana hizo umeshapita.

Ulimwengu wa sasa unahama sana kwenye kazi za kutumia nguvu na kuwekeza vilivyo kwenye teknolojia, hivyo kazi zinazolipa au zitakazokwenda kulipa zitajikita zaidi kwenye hilo.

Yani wale wanaotumia akili kuliko nguvu ndio watakaoshinda mpambano wa soko la ajira, ama kwa kuajiriwa au kujiajiri.

Sasa, hizi ni baadhi tu ya Careers au sekta ambazo binafsi ningeshauri vijana waziangalie kwa jicho la tatu.

1. Information security, cyber security.
2. Data Scientist.
3. Software developer.
4. Digital marketing.
5. Biomedical engineering.
6. Actuarial mathematics.
7. Health economist.
8. Financial Management.
9. ICT.
10. Health informatics.

Nyingine mtaongeza.

Hizo ni baadhi tu ya fields na Careers ambazo kwa sasa na baadae zitakwamua sana vijana. Na ukiangalia nyingi hapo utaona ni kazi ambazo hazitakuharibia work-life balance huku ukiweka mkwanja mzuri mfukoni.

Achana na kazi ambazo unatumia nguvu nyingi kupata mafanikio average , kama udaktari ,ualimu nk ambao wanazidiwa na ata na traffic police.

Sio kwamba hakuna madaktari au waalimu wenye succes ila its not order of the day.

Kumbuka, efficiency=load/effort. Na zote unaweza kujiajiri.

Sio Unasoma saana, vitu vigumuu kazi ngumu alafu unakuwa bado an average Joe.

Kijana, kupanga ni kuchagua.
Kijana unaongea nadharia sana,kama unafanya kazi saa 8,harafu unalipwa laki 8,huo muda mwingine utakuwa unafanya nini?kwa laki 8,ununue kiwanja,ujenge,ulipe Kodi,usomeshe,itakuchukua miaka mingapi?hata hao wapendwa wako uliokuwa unapata muda wa kukaa nao,kwa laki 8hiyo unafikiri utaweza kuwapa maisha Bora?mtoto asome feza,awe na toys kibao,mama awe na kausafiri?!
Ni Bora ulipwe M5,lakini utumike kwa saa 12,lakini investment utakayokuwa unafanya kwako na kwa wategemezi wako ni kubwa na Bora sana kuliko ya Yule mwenye laki8!!
Kwa laki 8,utakaa muda mrefu kabla hujaanza kukaa kwako,na kumbuka maisha hayaishii kwako,waza kizazi chako Cha tatu,kwa laki 8,utajenga link,utanunua gari lini,utawekeza lini!huwezi kujilinganisha na mtu anyepokea 5M ila tu "anatumika"sana.
Ni vzr vijana wasome kozi mbali mbali,hizo za IT,maana ndio ulimwengu unapoelekea,na kusoma uhandisi hakukuzuii kuwa Software engineer,wapo watu ninaowafahamu walisoma mechanical engineering,lakini sasa hv wanagonga Coding,hayo mambo ya artificial intelligence,balaa,
Kuna kampuni moja inaitwa,World mobile,network planner wake,amesoma Civil engineering!!kila kitu kinawezekana,mitahala ingebadlishwa,Ili kijana akiwa chuoni,asome kozi hata mbili ikibidi,au abadilishe juu kwa juu,
Ila kuacha 5M ukapokee laki 8,kisa saa za kufanya kazi kwenye 5M ni nyingi,hiyo sio busara bwashee,fika migodini siku moja,uone watu wanavyopiga kazi ngumu,lakini cheki pia na ukwasi walionao!!!.Kaka mkubwa,nimemaliza
 
Vizuri, Katika kuelewa taaluma fulani inahitaji kuwa na msingi wa taaluma hiyo. Sasa katika kusomea hivi vyeti haitakua na ugumu wa kuelewa yanayofundishwa sababu ya kukosa msingi wa IT?. Nifahamishe zaidi ninahitaji kumshauri mtu juu ya hili.
Cha kwanza kabisa ujue unataka nini?itakupa mwelekeo wa kusomea nini? na kwa upande wa IT ni pana sana kuna software development,web development,software engineering,network engineering or development,automation,DevOps engineering,data science,AI,machine learning,cybersecurity,cloud computing N.k
->IT inahitaji kujituma sana,kusoma kwa bidii (long life learner),kuwa up to date na taarifa au software,team work, n.k
->kama ananafasi aende darasi ila kutokwenda darasani sio kikwazo cha kutofikia malengo platform zipo nyingi za kutrain foundation kwa junior with hands on experience (project) mf.freecodecamp.org,guru99.com n.k
 
Msisahau sekta ya Wanyamapori na maliasili zake,zinalipa sana tena sana nadhani ni sekta ambayo imeajiri vijana wengi wa Kitanzania kuliko sekta yoyote kwa ninavyofikiria mimi,sekta hizi ni kama Tanapa,Ncaa,Tawa, TFS (misitu),ambazo ndo chanzo pia cha makampuni ya kitalii,mahoteli n.k ambayo pia yameajiri watu wengi na salary na marupurupu ni matamu ambayo yanamfanya mtumishi hasitamani kuacha kazi.
Na walio wengi wamepata elimu ya kawaida sana aidha baada ya kumaliza o'level,six na kuongezea Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Mwanza au MWEKA Moshi au Taaluma kama hiyohiyo au Utabibu wa Wanyamapori toka SUA.
Sekta binafsi unakuta dereva/tourguide kapiga Pasiansi au MWEKA halafu kapiga lugha za ziada mf,Kijurumani,Kijapani,Kichina n.k,kajipatia leseni sahihi toka VETA/NIT nakwambia mtu huyo mwenye PhD hamfikii kwa maisha bora.
So msiwaze kusoma sana ndo kutoboaa wazee.Goodmorning
Ni kweli kutoboa siyo elimu kubwa, nikipato unachoingiza kinakuwezesha vipi hata kazi ya ualimu kama hukusomea kijiji unatoboa, tatizo wengi wanawaza vipato vikubwa Ili kuwalipa wanakijiji waliowasomesha Sasa hapo kipato kitatosha vipi?
 
Hapo namba nne (Software Development) unajikanganya na maelezo yako ya awali ya kwamba ufanye kazi na upate muda wa kuishi.

Software development is time sucker and very tedious job though it's paid.

Upande mwingine umekua bias sana most of mentioned job hapo ni from ICT Industry ni kweli tupo kwenye mapinduzi ya TEHAMA ila still zipo kazi watu wanakula kwa ubua na wana-make lots of cash kutegemea na taasisi anayofanyia mtu.

Kitu muhimu katika vyote ni kuwa na professional certification kwa namna moja ama nyingine zina-boost kipato.

For me I'll go for Auditing field as one of the best job ambayo unakula kwa ubua ila uwe certified kwanza.

Then Risk management halafu ikifuatia na IT - Security (Cyber Security)

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Mmenikumbusha enzi zile za B Com kila mtu na mishahara ya Vodacom na minara ya mobitel.
Wapo wapi siku hizi.?
Ukigundua kipaji mapema ukawa na nidham unatoboa
 
Vipi kuhusu hii bachelor of biotechnology and laboratory science wakuu
 
SUA na UDSM wanatoa programme za: B.Sc. in Biotechnology and Laboratory Sciences (SUA) na B.Sc. in Molecular Biology and Biotechnology (UDSM). Chuo cha DIT kinatoa Diploma ya Biotechnology.

UDOM wanatoa B.Sc. in Biotechnology and Bioinformatics #ni programme mpya pale UDOM ambayo imechukua intake ya kwanza mwaka (2021).



Mtazamo wangu:



1. Kwa kuangalia trend ya hizi programme mbili za UDSM na SUA hapa Tanzania, Biotechnology ni programme nzuri. Programme hizi zinakupa knowledge na skills zitakazokuwezesha kufanya manipulation ya biological processes mbalimbali katika viumbe hai vidogo kama vile bacteria, virus na fungi ili kutengeneza products ambazo zina manufaa kwa viumbe hai, au kutibu magonjwa mbalimbali, n.k



Kwa lugha nyepesi...huku utajifunza kiundani yale mambo ya Genetic engineering uliyojifunza Advance School kwenye biology. Pia utapata maarifa mtambuka (general knowledge) ya sayansi nyinginezo zinazohusiana na Biotechnology. Kwa lugha nyingine hawa watu wanaitwa "wataalamu wa sayansi za vinasaba".



2. Programme hizi zitakupa ujuzi wa kukusaidia kufanya kazi kwenye taasisi, miradi na mashirika mbalimbali ya tafiti za afya ya binadamu, mifugo, mimea na hata zile zinazohusu viumbe waishio kwenye maji. Kwa Tanzania, baadhi ya sehemu hizo ni kama: IHI, KCRI, NIMR, MITU, TARI, TAWIRI, MDH, ICAP, GCLA, na mengineyo.



Pia ujuzi wa biotechnology unaweza kukusaidia kufanya kazi kwenye viwanda vya chanjo kama vile Hester Biosciences na TVI kwa hapa Bongo. Pia unaweza kupata ujuzi utakaokusaidia kwenda kufanya kazi za udhibiti ubora kwenye sehemu kama vile TBS, TMDA pamoja na viwanda vya vyakula, vinywaji, n.k. Vilevile unaweza kuwa mhadhiri kwenye vyuo vikuu kwa masomo kama: Biochemistry and Molecular Biology, Microbiology, Immunology, Parasitology, n.k



Hizo ni baadhi baadhi ya sehemu maarufu unazoweza kufanya kazi. Pia zipo sehemu nyingine nyingi ambazo sijazitaja.



3. Changamoto kubwa iliyopo ni kwamba teknolojia hii ni kubwa na kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania matumizi ya teknolojia hii ni madogo kutokana na sababu za kiuchumi kwakuwa kufanya shughuli zinazohusu Biotechnology inahitaji gharama kubwa. Hivyo basi graduates wa programme ya Biotechnology na zinazofanana na hizo wanajikuta wanajaa mtaani kwa kukosa ajira zilizo rasmi.

Kujiajiri katika fani hii inawezekana ila kuna changamoto zake ikiwemo uhitaji wa mitaji mikubwa.

Ila issue ya tatizo la ajira kwa nchi zetu ni tatizo kwa fani nyingi na sio Biotechnology pekee.



Kutokana na ukweli wa kwamba Biotechnology inahusisha masomo mengi ambayo yanahusiana na afya ya binadamu basi graduates wa programme hii wamekuwa wakipambana kutafuta nafasi za kufanya kazi katika hospitali mbalimbali kwakuwa sehemu zinazofanya shughuli za Biotechnology sio nyingi hapa Tanzania ukilinganisha na idadi ya wahitimu. Hili ni tatizo kwakuwa wataalamu hawa wa biotechnology ni kweli wanaweza kufanya kazi za maabara za hospitali lakini hawaruhusiwi kisheria kufanya kazi hiyo.



4. Dunia kwa sasa inakabiliwa na majanga makubwa kama vile COVID-19 na Monkey Pox Virus, climate change, n.k ambayo yanaweza kutatuliwa kiurahisi kwa kutumia utaalamu wa biotechnology. Hivyo basi tunategemea siku za mbeleni nchi zetu zitaona umuhimu wa kuweka nguvu kwenye fani hii na basi sehemu za kufanya ujuzi huu zitaongezeka na tatizo la ajira kwa wataalamu wa biotechnology litapungua (haliwezi kuisha).



5. UDOM wameongeza component moja ya tofauti na UDSM na SUA kwenye programme ya Biotechnology iitwayo "Bioinformatics".

Bioinformatics inahusisha matumizi ya biology, statistics na computer science katika kuchakata data mbalimbali zitokazo maabara zinazohusiana na vinasaba. Bioinformatics ni part nzuri ya Biotechnology na wataalamu wa Bioinformatics ni wachache hapa nchini. Uhitaji wake kwa sasa unaweza usiwe mkubwa sana hapa nchini lakini tunatarajia siku za mbeleni uhitaji utakuwa mkubwa hapa nchini na duniani kote. Unaweza ukaamua kusoma zaidi issues za Bioinformatics kwenye level ya Masters na PhD.



Curriculum za Biotechnology kwa SUA na UDSM zinayo component ya Bioinformatics lakini curriculum ya UDOM imeenda ndani zaidi kwenye issues za Bioinformatics hivyo basi tunatarajia wahitimu wa UDOM kuwa na ujuzi zaidi kwenye Bioinformatics kuliko hawa wa UDSM na SUA. Ila ili uweze kuielewa Bioinformatics vizuri anza kujenga mapenzi na maswala ya programming kwenye computer, hesabu kidogo especially eneo la statistics na biology kwa sana.



SUMMARY:

Biotechnology ni choice nzuri kama una malengo ya kuja kuwa researcher/mtafiti au mtaalamu kwenye maswala ya vinasaba vya binadamu, wanyama, mimea na viumbe wengine. Zipo opportunities pia za kufanya kazi sehemu nyinginezo ambazo hazihusiki na mambo ya vinasaba kama nilivyotaja huko juu; viwanda vya vyakula, TMDA, n.k



Swala la ajira ni changamoto kidogo kwenye Biotechnology lakini hata fani nyingine kama udaktari zina changamoto hiyo kwa sasa.

Kama mtu ataamua kuingia kwenye fani hiyo basi asome kwa bidii ili kupata ujuzi vizuri. Kufaulu vizuri na kuwa na cheti kizuri ni muhimu kwenye issues za competition. Kujiongeza kwa kutafuta connections za watu ambao wapo kwenye fani hii kwa muda mrefu ni jambo la busara pia. Na pia kumtanguliza Mungu katika safari yako ya fani ya Biotechnology ni muhimu zaidi. Ukizingatia hayo basi Biotechnology itakupeleka sehemu nzuri sana kimaisha.



+++ Biotechnology sio programme ngumu kama watu wengi wanavyotishia. Ila inakuwa rahisi pale unapojifunza kuipenda. Fursa zipo pia kama utakuwa mpambanaji
Vipi kuhusu hii bachelor of biotechnology and laboratory science wakuu

(au ukiwa na connection 🌚)



#PASSION IS KEY



~ Biotechnologist
 
Kuna free Funded scholarship ya Axl(software development), itamfaa yoyote anaetaka kuingia kwenye ict. Duration ni mwaka mmoja na ukimaliza io... .. utakua umekwivaa
hii kitu mwenye uhitaj anaipataje mkuu
 
Back
Top Bottom