Hivi huyu mdau
CONTROLA kuna uzi nilifungua juu ya kufungua kampunj ya kusafirisha unga to UK jamaa akazingua hakutoa wazo lake madini yake, na ninamjua ana madini mazuri sana, ngoja aje hapa nimlime faini
Mkuu naukumbuka ule uzi na ninakumbuka kila kitu ila kama unakumbuka nilisema jibu la swali lako sio fupi nikasema nitafungua thread kwasababu
si wewe tu unaetafa fanya viile nikawa nimesema nifungue thread kisha ndani ya thread nijibu swali lako kwa undani na zaidi niweke na vingine ambavyo hata
hukua unavijua (mbinu/maujanja ya ku surrvive/nk) sio kwamba nilikaa kimya makusudi mkuu,hata thread huwa nafungua nikiwa free kbsa kbsa na akili ipo
ktk hilo jambo ndio mana nakua natoa vitu vingi,yani mimi ukiona nimefungua thread naongelea kitu ujue (jana au leo) nimetoka kifanya hicho kitu ktk uhalisia
ukiona naongelea mbinu za kufanya biashara flani ujue nipo nafanya hicho kitu siwezi ongelea biashara ambayo siifanyi,mbinu ambayo siifanyi,chochote ambacho
sijawahi waza hata kukifanya eti nafungua thread au nina njaa sijala siku mbili Halafu nafungua thread nafundisha watu
jinsi ya kuishinda Njaa hapana sipo hivyo mkuu wangu hiyo FAINI naomba ipige STOP kdg kwasababu siku nitakapo fungua thread khs
lile swala utaelewa hata ni kwann nilikua kimya muda mrefu,la mwisho mkuu unapofungua thread au simulia kitu basi ni lazima UWE NA TAARIFA ZOTE muhimu
kisha ndio unakuja simulia au andika ukiwa na uhakika na unachokiandika hivyo mkuu tuvumiliane tu mkuu wangu Siwezi ficha kizuri kilicho ndani yangu hata siku 1
kama kipo nitakitoa tu kila mtu akipate maana ktk watu siogopi wapa fursa ni WABONGO siogopi hata kidogo kumwambiia MTANZANIA nimepita njia flani nimeona PESA KWENYE BOX
sema kesho nataka nikazifate,najua mtanzania ni mtu wa dharau na kupuuza,Hiyo ndio sababu nikiwa namwaga mchele humu JF naumwaga mzima mzima maana najua walaji ni wachache
wengi husoma na kuyaacha humu humu kwahyo sijakusahau chief,ahadi ni deni na lazima nilipe hilo Deni.