Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
SIKU mbili baada ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni Papa Francis kumaliza ziara yake Barani Afrika: katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Sudan Kusini, wakuu wa nchi za Afrika Mashariki wamekutana Bunjumbura kujadili Hali ya mambo DRC hususan Mashariki mwa nchi hiyo ambako mapigano makali yanaendelea.
Pamoja na kwamba kikao hicho kimekuja Kwa kuchelewa mno maana wananchi katika eneo hilo ambao ni sehemu ya Afrika Mashariki wanateseka mno hasa kina mama na watoto wanaouliwa, kubakwa, kulawitiwa, kuchomewa nyumba zao na hata makaburi ya halaiki kadhaa yamegundulika. Zaidi ya watu milioni moja wameyakimbia makazi yao!
Akiwa mbele ya Papa Francis, Rais wa DRC Felix Tshekedi alimshitaki Paul Kagame kwamba ndiye ansyefadhili kikundi maarufu cha M23 ambacho kichwa ngumu kutesa watu miongoni mwa vikundi lukuki vya waasi.
Katika kikao hicho Cha wakuu wa nchi za EAC moja ya Azimio walilotoka nalo ni kuwataka wakuu wa Majeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana ndani ya siku saba kuona namna ya kumaliza Mgogoro huu wa DRC.
MY TAKE: Wakuu wa Majeshi wa EAC mkumbuke jambo moja muhimu kwamba Mkuu wa Majeshi ya Rwanda (mtuhumiwa) naye atashiriki Je, kama ni kweli nchi yake inafadhili wauaji wa M23 kusaka madini ya dhahabu atakubaliana na maamuzi yenu?
Pili, mjue kwamba M23 ni Wakongo wenye asili ya Rwanda kutoka kabila la Tutsi. Watu hawa waliingia nchini DRC zaidi ya miaka 60 iliyopita. Baadhi yao ni wakubwa mno katika vyombo vya ulinzi na usalama vya DRC na ndio maana kila mara Tshekedi alipojaribu kupangua Jeshi lake kuleta ufanisi amekuta akitwanga maji kwenye kinu.
Hawa M23 wanajenga hoja dhaifu kwamba ndugu zao (Watutsi) wa Kongo wanaonewa kisa tu wanaongea Kinyarwanda na si ki-Kongo au Kifaransa. Ujinga plus.
USHAURI: Mkisema nchi za EA zote zipeleke Majeshi mkumbuke mtasnichiwa na Majeshi ya Rwanda na Kongo wenyewe kimaslahi. Badala yake kazi hii ya kuwaua, kuwafyeka na kuwatokomeza magaidi wa M23 ipewe JWTZ peke Yao.
Uzoefu unaonesha kwamba 2014 JWTZ waliwatokomeza na mtakumbuka vita ya maneno kati ya Jakaya Kikwete na Paul Kagame ilianzia hapo. Kwamba Kagame alikasitika Kwa nini JWTZ wa Jakaya wayauwe M23 ni ushahidi mwingine kwamba Kagame anayo maslahi katika vita hii ya Mashariki mwa Kongo.
Nchi za EA wanachoweza kufanya ni kutoa michango ya fedha za kutosha kisha warudi majumbani wapumzike kazi wawaachie JWTZ waingie msituni. Naamini ni kazi ya siku chache sana. Achaneni na sijui vikosi vya kulinda amani na vikao vya kila mara mahotelini.
M23 si wa kubembeleza, si wa kufanya nao vikao. Ni JWTZ kuwatandika kikatili kutoka mbele Hadi nyuma. JWTZ hii kandarasi INAWAHUSU, ichukueni haraka kuwaokoa wenzetu. Nawasilisha!