Trump anamshambulia Zelenskyy kwa kukaa madarakani kidikteta. Ukraine ilitakiwa kuwa na uchaguzi 2024 lakini haukuitishwa kwa vile bado iko kwenye State of Emergency iliyopitishwa na bunge mwaka 2022 na kuendelezwa (extended) hadi 2025 kwa sababu ya vita.
Trump haoni shida kabisa kwa Putin kuwa madarakani tangu 2000 hadi leo. Tangu mwishoni mwa utawala wa B Clinton kisha GW Bush, kisha B Obama, kisha D Trump 1.0, kisha J Biden, na sasa D Trump 2.0.
Kifupi, D Trump na MAGA wameona Putin ni mzungu na mkristo mwenzao mwenye itikadi za kihafidhina kama wao (pia wote hawapendi demokrasia). Hivyo, wanaamini Urusi haitakiwi kabisa kuwa adui wa Marekani. Tatizo lao ni hawa wanaoitwa LIBERALS huko Ulaya. Hata Hitler alikuwa bora zaidi kwa mtazamo wao.
Hata Afrika ya Kusini wameikatia misaada kwa kuchukua baadhi ya mashamba ya wazungu.
This is very interesting. Mchezo umebadilika.
Sasa nafuatilia kuona kama kweli USA itabadili kabisa itikadi na mkakati wake mkuu wa enzi za vita baridi (Cold War) wa kupambana na nchi za kikomunisti kama adui wake mkuu na kugeukia nchi zisizo za kikristo, za kiliberali, zisizowapa wazungu hadhi kubwa na kuruhusu fursa kubwa za kiuchumi kwa matajiri wa US na washirika wao.