Kazi imeanza Zelensky anataka kutolewa kafara

Kazi imeanza Zelensky anataka kutolewa kafara

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Hawa manyang'au wa U.S naona wameshamtumia Zelensky kama pampas sasa wanataka kumtupa.

Visingizio vimeanza za kuwinda kuondoshwa

Huyu Musk mtandao wake huu amekuwa akiutumia kuchochea tawala kadhaa kuondoshwa

Kazi kaianzisha Trump chawa Musk anaunga tela

View: https://x.com/realDonaldTrump/status/1892242622623699357?t=DFDdNH9XOKkzxW6slBh8eA&s=19

View: https://x.com/realDonaldTrump/status/1892397388595093561?t=Qiwya97C-41jPe0IKwMbqg&s=19

View: https://x.com/elonmusk/status/1892292753314181582?t=Z9sec4aEmqlFfLERxKPPhA&s=19
 
Marekani anatumia kila mbinu kujiondoa kwenye hivi vita bila kupata aibu kama aliyo ipata alipo kimbia Vietnam.
Wamesha ona hivi vita hawatoboi hata idumu miaka 70 ,haya maigizo yanayo endelea haya fanywi kwa bahati mbaya.
 
Kobaaz bana kwa kujifariji tu. Yani mnalazimishaga vitu ilmradi tu nafs zenu zipate faraja.

Nyau de adriz
 
Trump na huyo Elon wamezidisha dharau na kiburi Kwa umoja wa ulaya na Zelesky wamesahau kwamba wao wenyewe US Kila wanapotaka kupigiana lazima wawaombe umoja wa ulaya kuungana nao.
 
Kobaaz bana kwa kujifariji tu. Yani mnalazimishaga vitu ilmradi tu nafs zenu zipate faraja.

Nyau de adriz
Ww ndo unalazimisha furaha maana sasa hivi mna hali ngumu baada ya Trump kuwapelekea moto.
Tulipo kuwa tuna waambia Urusi ni dude kubwa mlikuwa mnakaza fuvu, sasa ona amewashinda kwenye uwanja wa vita na bado kwenye dipromasia yupo anawagaragaza.
 
Hawa manyang'au wa U.S naona wameshamtumia Zelensky kama pampas sasa wanataka kumtupa.

Visingizio vimeanza za kuwinda kuondoshwa

Huyu Musk mtandao wake huu amekuwa akiutumia kuchochea tawala kadhaa kuondoshwa

Kazi kaianzisha Trump chawa Musk anaunga tela

View: https://x.com/realDonaldTrump/status/1892242622623699357?t=DFDdNH9XOKkzxW6slBh8eA&s=19

View: https://x.com/realDonaldTrump/status/1892397388595093561?t=Qiwya97C-41jPe0IKwMbqg&s=19

View: https://x.com/elonmusk/status/1892292753314181582?t=Z9sec4aEmqlFfLERxKPPhA&s=19

Nchi ipo vitani unaanzaje kufanya uchaguzi? Yani wanaongea kile wanachojiskia.

Hapo Ukraine hana chake tena, US wanachofanya na haya matamko yao ni kuandaa wafu kisaikolojia.

Ulaya inabidi wajitafakari sana huyu US sio wa kumwamini ata hiyo NATO ukute ni kwaajili ya mikwara tu kikinuka US atawaangalia tu.
 
Trump anamshambulia Zelenskyy kwa kukaa madarakani kidikteta. Ukraine ilitakiwa kuwa na uchaguzi 2024 lakini haukuitishwa kwa vile bado iko kwenye State of Emergency iliyopitishwa na bunge mwaka 2022 na kuendelezwa (extended) hadi 2025 kwa sababu ya vita.

Trump haoni shida kabisa kwa Putin kuwa madarakani tangu 2000 hadi leo. Tangu mwishoni mwa utawala wa B Clinton kisha GW Bush, kisha B Obama, kisha D Trump 1.0, kisha J Biden, na sasa D Trump 2.0.

Kifupi, D Trump na MAGA wameona Putin ni mzungu na mkristo mwenzao mwenye itikadi za kihafidhina kama wao (pia wote hawapendi demokrasia). Hivyo, wanaamini Urusi haitakiwi kabisa kuwa adui wa Marekani. Tatizo lao ni hawa wanaoitwa LIBERALS huko Ulaya. Hata Hitler alikuwa bora zaidi kwa mtazamo wao.

Hata Afrika ya Kusini wameikatia misaada kwa kuchukua baadhi ya mashamba ya wazungu.

This is very interesting. Mchezo umebadilika.

Sasa nafuatilia kuona kama kweli USA itabadili kabisa itikadi na mkakati wake mkuu wa enzi za vita baridi (Cold War) wa kupambana na nchi za kikomunisti kama adui wake mkuu na kugeukia nchi zisizo za kikristo, za kiliberali, zisizowapa wazungu hadhi kubwa na kuruhusu fursa kubwa za kiuchumi kwa matajiri wa US na washirika wao.
 
Nchi ipo vitani unaanzaje kufanya uchaguzi? Yani wanaongea kile wanachojiskia.

Hapo Ukraine hana chake tena, US wanachofanya na haya matamko yao ni kuandaa wafu kisaikolojia.

Ulaya inabidi wajitafakari sana huyu US sio wa kumwamini ata hiyo NATO ukute ni kwaajili ya mikwara tu kikinuka US atawaangalia tu.
Mbona Urusi walifanya uchaguzi kipindi cha vita?
 
Back
Top Bottom