Kazi muhimu ya Tundu Lissu ni kujenga Umoja na mshikamano ndani ya Chadema. Nini kifanyike?

Kazi muhimu ya Tundu Lissu ni kujenga Umoja na mshikamano ndani ya Chadema. Nini kifanyike?

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
829
Reaction score
1,120
Ni ukweli ndani ya chadema wanachama wamegawanyika mapande ya kiuchaguzi na kampeni. Ninatoa ushauri rahisi wa kutibu majeraha bila nguvu kubwa kama ifuatavyo:

1. Kushughulikia saikolojia ya kushindwa na kushinda kwa wanachama kwa kuonyesha wazi kuwa ushindi ni wa chadema yote na yeye Lissu ni kiongozi wa kila mtu bila kubagua upande wowote

2. Aepuke machawa kwa pande zote mbili. Haitampa uhalisia wa mambo ndani ya chama.

3. upendo kwa wote usiokuwa na chembe ya unafiki hususani kwa upande ulioshindwa ili kuwaondolea hofu ya kunyimwa haki au kulipizwa kisasi.

4.Ushirikishwaji katika maamuzi na kupata ushauri bila kujali nani alikuwa upande upi. uchaguzi umeisha, inawezekana washauri walio wazuri kabisa wengine akawapata upande wa pili, atoe fursa ya umahili wao. Hii itapandisha imani kwa utawala na uongozi mpya

4.Kuwaita na kuongea na timu za makampeni meneja wa pande zote mbili ili kuvunja kambi zao rasmi kama bado zipo kimya kimya na kuunga mkono utawala mpya.

5.Timu au Tume iundwe yenye watu mahili itayopita mikoani kukusanya maoni ya namna ya kuondoa majeruhi yaliyotokea na kufanya upatanishi.

6.kusikiliza rufaa zote za uchaguzi kwa uadilifu na kuzitolea maamuzi

7. uteuzi wa wajumbe wa sekretariati yenye mchanganyiko na yenye weledi na isiyo akisi mapande ya kampeni au upendeleo.

8. Mwenyekiti kutoa hotuba rasmi ya upatanishi na upendo wakati ataoona inafaa.
Mkutano wa Retreat kwa kamati kuu agenda kuu iwe ni pamoja na kujenga umoja ndani ya chama.

9. Kutorusu mwanachama kuendeleza chuki baada ya uchaguzi au kuweka mazingira ya kubagaza uongozi uliopo

10. Mambo yote yaliyotokea yachukuliwe kuwa ni sababu ya mazingira ya uchaguzi tu na hayakuwa na nia mbaya ya kumbomoa mtu au chama. Huo ndio uwe ni msimamo wa chama- FALSAFA YA STRONGER TOGETHER ikamilishwe ndani ya siku 100 ya uongozi.
 
Hana mpango huo, saivi yupo honey moon

Wanaharakati wanamwambia fukuza wote ubaki na wanaharakati wenzako😂👇
 

Attachments

  • Screenshot_20250125-135359.png
    Screenshot_20250125-135359.png
    576.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom