Kazi ni Ile inayokuingizia Kipato. Mama au Baba wa nyumbani siô Kazi kwani Hakuna kipato kinachozalishwa.

Kazi ni Ile inayokuingizia Kipato. Mama au Baba wa nyumbani siô Kazi kwani Hakuna kipato kinachozalishwa.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
KAZI NI ILE INAYOKUINGIZIA KIPATO. MAMA AU BABA WA NYUMBANI SIÔ KAZI KWANI HAKUNA KIPATO KINACHOZALISHWA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Amri ya Mungu ya kufanya Kazi. Inahusu kufanya Kazi za uzalishaji Mali, kujipatia kipato ili uweze kuishi.
Yàani Mûngu anapokuambia Fanya Kazi anamaanisha Fanya uzalishaji ili uweze kuishi. Kwani Asiyefanya Kazi Kula na asile.

Amri ya Kazi Ipo Kwa Wanadamu wote. Wakike na wakiume. Kwèñye jamii nyingi hasa zile Ambazo zîpo gizani kûna kasumba mbaya kuwa Mwanaume ndiye anatakiwa kufanya Kazi. Ilhali ukweli na Haki NI kuwa Watu wôte wanalazimishwa kufanya Kazi Bila kujali jinsia zào. Kazi za uzalishaji Mali, mapato.

Kwa nini lazima ufanye Kazi hata kama wewe ni Mwanamke;
1. Wewe ni MTU, ili Kulinda Ûtu wako
Mtu Asiyefanya Kazi z uzalishaji lazima utu wake uathirike. Lazima anyanyasike Kwa sababu atakuwa tegemezi.
Unaposikia Wanawake wananyanyaswa Moja Kwa Moja lazima uelewa ni kwèñye jamii na wale Wanawake wasiofanya Kazi. Huwezi mnyanyasa MTU anayejitegemea.

Hivyo unafanya Kazi ili uheshimike kama MTU.
Asiyefanya Kazi Kwa namna yoyote lazima adharaulike Bila kujali NI Mwanaume au Mwanamke.

2. ILI UMUABUDU MUNGU WAKO.
Kama hufanyi Kazi Huwezi kuwa unaabudu. Mungu anataka Zaka na Sadaka. Na elewa Zaka ni sehemu ya Kumi ya mapato yako siô mapato ya Mumeo. Mapato ya Mtu Mwingine (akiwepo Mumeo) akikupa ukayapeleka Kwa Mungu hayo huchukuliwa kama Sadaka na sio Zaka.

Elewa Mungu anabariki Kazi za mikono yako. Hapa inamaanisha Kazi za uzalishaji wako ili akupe riziki.
Unafanya Kazi ili usiende Kwa Mungu Mikono mitupu.
Kuonyesha kuwa Mungu aliibariki Kazi ya Mikono yako.
Mwanaume naye akienda atatoa Kulingana na alivyobarikiwa.

Kûna MTU atasema Ukiolewa au ûkioa mnakuwa Mwili Mmoja. Siô kwèli.
Kwa Mungu kîla MTU hulipwa yeye kama yeye na siô kimafungu. Kwamba Mungu hawezi kukuadhibu Kwa Makosa ya Mumeo au Mkeo. Pia Mungu hawezi kukubariki Kwa matendo ya Mkeo au Mumeo hiyo haipo.

Kushika Amri za Mungu NI Kwa Mtu mmoja mmoja.

3. ILI KUWA NA HAKI YA KUMILIKI MALI.
Nje ya Urithi na zawadi ambazo utolewa Kwa utashi wa Mtu. Sehemu pekee àmbayo MTU anahaki ya KUMILIKI Mali NI Kwa kufanya Kazi.
Mali yoyote àmbayo hujaifanyia Kazi na kuitolea jasho na haitokani na kipato chako siô Haki yako kisheria.
Kama NI Mali za Wazazi wako hizô siô zako.
Kama NI Mali za Mumeo au Mkeo hizô siô zako linapokuja suala la HAKI.

Zitakuwa zako Kama mwenye Mali Kwa hiyari Yake akaamua kukupatia akiwa yupo hai(zawadi) au akiwa amekufa(Urithi).

Kwèñye Ndoa zinakuwa Mali Zenu Kwa Sababu ya Ndoa ila nje ya Ndoa kîla mmoja atapewa alichochuma. Na hiyo ndîo HAKI.

NI dhulma kutaka KUMILIKI Mali isiyoyako. NI dhulma kama zilivyo dhulma ñyiñgine.
Kûna Amri inasema usitamani Mali ya jirani yako.
Unapotengana na Mkeo au Mumeo Mali zote Ambazo hukuzichuma siô Mali zako NI Mali ya jirani yako. Usizitamani.
Hakuwa jirani Kwa sababu alikuwa Mumeo au Mkeo lakini nje ya Ndoa huyo NI jirani kama walivyojirani Wengine.

Sheria kandamizi, Sheria nyonyaji, Sheria dhulmati zilizotungwa na Watu wasio na uelewa na mambo ya Haki huweza kumpa umiliki wa Mali MTU asiyestahili.

Kwa ujumla MTU anafanya Kazi ili ajitegemee na asipate Laana y kumtegemea MTU Mwingine.

Kwèñye jamii yetu kûna kasumba mbaya kuwa Mwanamke kuwa Mama WA nyumbani NI Kazi Jambo ambalo NI dhana potofu.
Dhana hiyo imeundwa kimakusudi kwa lengo la kukandamiza Haki hasa Kazi za Wanawake kujitegemea na kuishi Maisha halisi kama Nature inavyotaka.
Baadhi ya Wanaume huitumia dhana hiyo kama silaha ya kumuangamiza Mwanamke ili awe tegemezi na kumfanya awe mtumwa milele. Wanaume wanaotaka kuabudiwa kama mîungu. Kwa sababu anayekulea na kukulisha NI kama mungu wako.

Kwa mfano NI jamii àmbayo Wanawake ni tegemezi àmbayo Wanawake huweza kuolewa kimafungu(wake wengi) lakini jamii ya Wanawake wanaojitegemea hiyo NI ngumu.
KUoa Wake wengi NI unyanyasaji Mkubwa ikiwa Itafanywa pasipo hiyari ya Mwanamke husika.
Na Mwanamke tegemezi Hana hiyari Kwa sababu siô Mtu na Hana UTU.

Kupika chàkula chako au kwaajili ya familia yako haipo kwèñye orodha ya Kazi Kwa sababu unajitumikia mwenyewe.
Huwezi kupata kipato Kwa kujitumikia wewe mwenyewe.

Kufanya Kazi maana yake kutumikia Wengine ili wakulipe.

Huwezi kujifulia nguo zako au kumfulia Mtoto wako mdogo alafu ukaiita Kazi ilhali unajitumikia mwenyewe.

Huwezi kujipikia au kusafisha Vyombo au Nyumba unayoishi ukasema unafanya Kazi ya uzalishaji labda úwe na upeo mdogo..

Unaweza kufanya miradi ya familia na ukazalisha kipato Kwa kuwauzia Wengine.
Mfano unafuga Kuku WA familia lakini unauza mayai na Kuku Kwa Watu. Hiyo inaitwa Kazi.

Unalima shamba lako Kisha mazao unauzia Watu Wengine. Unajipatia kipato. Hiyo NI Kazi.

Kusema kuita majukumu ya Nyumbani NI Kazi ni matumizi Mabaya ya msamiati.

Ndîo maana ukikua Hapo kwèñu kama Huna Kazi hata kama unajishughulisha kuosha Vyombo lazima uambiwe utafute Kazi ya kufanya

Yàani Kazi ya kukufanya uishi. KAZI ya kukupa mahitaji yako.

Ndoa siô Kazi. Kuolewa siô KAZI
Kuzaa siô KAZI.
Kulea siô Kazi labda kulea Watoto wasiowako Kwa mkataba WA malipo yàani kuwa Yaya(babysitter) hiyo itaitwa Kazi

Na Huwezi kutaka ulipwe Kwa kujitumikia wewe mwenyewe.
Mfano ati kusafisha nyumba unayoishi au kulea Watoto wako alafu utake kulipwa hiyo siô Kazi.
Kama Huwezi ajiri MTU akulelee Mtoto mumlipe wewe na Mumeo.

Kûna wale wanasema Wanaume wanaotafuta Wanawake wanaofanya Kazi wamebweteka, au wavivu au mario. Wengine wanafika Mbali zaidi kuwaita mashoga.

Lakini hiyo NI mihemko ya Watu weñye upeo mdogo.

Waislam, Wayahudi na Wakristo wanaotumia Biblia na Quran na Talmud hii NI orodha ya Manabii na mitume na watu weñye majina makubwa kukuliko ambao wake zào walikuwa wanafanya Kazi(yaani wazalishaji)

1. Mtume Muhammad
Huyu alimwoa Bi. Khadija, mfanyabiashara. Muhammad alishauri kijana WA kiislam aoe Mwanamke Kwa vigezo vitatu àmbavyo NI Dini yake, Uzuri wake na Mali. Sasa Mwanamke atakuwaje na Mali kama hafanyi Kazi

2. Suleiman
Ñdipo akaandika Mithali 31
3. Isaka aliyemwoa Rebecca aliyekuwa anachunga Mifugo ya Babaake.
4. Yakobo aliyemwoa Raheli na Recho. Yakobo alimkuta Raheli akiwa anachunga Mifugo
5. Musa aliyemwoa Sipora. Sipora alikuwa anachunga

Watu wafanye Kazi

Binti yako kama hutaki kuabudu Watu na unàtaka kumwabudu Mungu kikamilifu lazima ameivya kufanya Kazi uitekeleze.

Mwanaume anayekuzuia usifanye Kazi ya uzalishaji huku akikukwambia ufanye ujitumikie yàani ufanye majukumu ya kifamilia na kuziita NI Kazi ilhali hujui unaingiza kipato kiasi gani. Huyo hafai. Hana Upendo WA kwèli. Hana Haki na NI mlaghai. Anataka uvunje Amri ya kufanya Kazi àmbayo siô Amri tuliyopewa Sisi Wanaume pekee Bali NI Amri ya wôte.

Kûna hoja ya Mwanaume ndiye aliyeumbiwa Kula Kwa jasho.
NI Sahihi lakini hiyo siô hoja ya kumfanya mwanamke asifanye Kazi.
Mwanamke afanye Kazi za uzalishaji Ambazo hazitamfanya atoe jasho(yàani ahangaike kupita kiasi).
Kumbuka Kabla ya anguko, agizo la Mungu lilikuwa Kulima Bustani na Kûitunza, hiyo NI Kazi walipewa lakini Mungu hakuweka laana ya kudanya kazi hizo kwa jasho.

Hivyo ndivyo utakavyoishi Kwa HAKI na kuzifurahia Siku zako zote utakazoishi Hapa Duniani Binti yàngu.

Acha nipumzike sasa.
Ijumaa Kareem, ñawatakia maandalizi mema ya Sabato

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Sawa Sasa Ndugu Robert tafadhali uweke mtazamo wako kwenye maswali yangu...

1.Je Mwanaume akiwa Bachela kuna kazi gani anazifanya ambapo akioa anaacha.

2.Je, kufua na kupasi anakofanya Bachela, akipeleka nguo zake dry cleaner analipa ama halipi?

Je yule Dobi ule sio mshahara wake?

Na ukiacha kujipikia ukaenda lipia mgahawani, Je ule sio mshahara Kwa mwenye mgahawa?

3.Unapoajiri House boy/House girl ule mshahara unaomlipa mwisho wa mwezi ni wa kazi gani? Ni kitu Gani anazalisha?

4.Mke wa mtu tajiri mkubwa anafanya kazi Ili iweje?

5.Je, unajua kuachiwa uhuru Mwanamke ndiko kumesababisha mmomonyoko wa maadili tulionao sasa?

6.Ni kwamba Mama wa Nyumbani ni kazi SEMA haijawekwa kiwango Cha mshahara.

7.Je, Mwanaume anapoenda kununua kahaba akamlipa Je ule si mshahara japo hiyo ni kazi ya dhambi?

Mume anapomletea mke mavazi, chakula, malazi, kumtoa out na mengine Je huyo Mwanamke angekuwa anafanya kazi mshahara wake si angeutumia kwenye mambo hayohayo?

Niishie hapa kwa leo Ndugu Robert...
 
Sawa Sasa Ndugu Robert tafadhali uweke mtazamo wako kwenye maswali yangu...

1.Je Mwanaume akiwa Bachela kuna kazi gani anazifanya ambapo akioa anaacha.

Hakuna kazi anayoacha au unayoacha ukioa au ukiolewa kuhusu zile kazi ya kujitumikia
2.Je, kufua na kupasi anakofanya Bachela, akipeleka nguo zake dry cleaner analipa ama halipi?

Analipa.

Je yule Dobi ule sio mshahara wake?
Ni malipo yake
Na ukiacha kujipikia ukaenda lipia mgahawani, Je ule sio mshahara Kwa mwenye mgahawa?
Ni posho yake
3.Unapoajiri House boy/House girl ule mshahara unaomlipa mwisho wa mwezi ni wa kazi gani? Ni kitu Gani anazalisha?
Anatoa huduma ambayo haimhusu inakuhusu wewe uliyemuajiri ndio maana unamlipa.
4.Mke wa mtu tajiri mkubwa anafanya kazi Ili iweje?
Matajiri wote duniani wake zao wanafanya kazi au wanamiliki makampuni
5.Je, unajua kuachiwa uhuru Mwanamke ndiko kumesababisha mmomonyoko wa maadili tulionao sasa?
Hakuna kitu kinaitwa mmomonyoko wa maadili. Kilichopo ni kuingiliana kwa maadili baina ya tamaduni.
6.Ni kwamba Mama wa Nyumbani ni kazi SEMA haijawekwa kiwango Cha mshahara.

Mama wa nyumbani sio kazi.
Mtu hawezi kujitumikia akajilipa
7.Je, Mwanaume anapoenda kununua kahaba akamlipa Je ule si mshahara japo hiyo ni kazi ya dhambi?
Anamlipa kwa sababu sio Mali yake
Huwezi lipia kitu ambacho wewe ni mmiliki.

Mume anapomletea mke mavazi, chakula, malazi, kumtoa out na mengine Je huyo Mwanamke angekuwa anafanya kazi mshahara wake si angeutumia kwenye mambo hayohayo?
Kumnunulia Mke au mume zawadi haipo kama sehemu ya mshahara.
Niishie hapa kwa leo Ndugu Robert...
 
Wewe ukienda kazini mkeo kama huwa anashinda nyumbani hapiki?hakuandalii nguo?watoto je?akiacha vyote hivyo ikiwa ni mkeo ingekuwaje?dada wa kazi ehhh? Mungu alikuwa na akili kubwa kusema wanawake wabaki majumbani kufuatilia familia zao Sasa hivi Kila mwanamke anatoka.....ulawiti ubakaji umeongezeka wanawake wamevaa nafasi ya mwanaume...Mnyazi Mungu tunusuru
 
Haya mambo ya kukimbizana na Dunia ndiyo yametufikisha hapa.

Hoja ya msingi kwa mstakabali chanya ni heri kuwepo majukumu kwa wote ya kujipatia kipato, lakini yale ya mwanamke yawe na ukomo wa muda ili awajibike kuweka sawa mazingira ya familia na nyumbani.

Kwa tathimini isiyo rasmi, familia zenye kipato kikubwa ndizo zina wahanga wengi wa madawa ya kulevya, wasagaji na mashoga.
Ukifuatilia kwa kina hayo ni matokeo ya malezi mabovu kwa sababu ya ubize wa wazazi wao kutafuta pesa na kumuachia dada wa kazi jukumu la malezi.

Maisha siyo fedha tu, tuangalie namna bora ya kubalance pande zote.
 
Nadhani wanawake wana shida fulani isiyoonekana. Imagine mwanamke akiachiwa tu hata uchi barabarani anatembea. Nenda social media utajionea mambo wanayofanya.

Akiwa na uhuru wa kifedha ataanza kuishambulia nyumba yake mwenyewe aibomoe, then akiibomoa anaanza kulialia tena na kulaumu wanaume, hapo malezi yatakua changamoto usishangae watoto wengi wenye shida ya maadili wamelelewa na single mothers.

Samahani mleta mada nimetoka nje ya mada, Ila hili nalo naomba mkalitazame.
 
Robert naona hata hujanielewa inaonekana unajibu tu bila kusoma Nini nilimaanisha.
 
Hakuna kazi anayoacha au unayoacha ukioa au ukiolewa kuhusu zile kazi ya kujitumikia

Analipa.

Ni malipo yake

Ni posho yake

Anatoa huduma ambayo haimhusu inakuhusu wewe uliyemuajiri ndio maana unamlipa.

Matajiri wote duniani wake zao wanafanya kazi au wanamiliki makampuni

Hakuna kitu kinaitwa mmomonyoko wa maadili. Kilichopo ni kuingiliana kwa maadili baina ya tamaduni.

Mama wa nyumbani sio kazi.
Mtu hawezi kujitumikia akajilipa

Anamlipa kwa sababu sio Mali yake
Huwezi lipia kitu ambacho wewe ni mmiliki.

Kumnunulia Mke au mume zawadi haipo kama sehemu ya mshahara.
Unajua kuna vitu ndugu Robert viko wazi kabisakabisa.

Nimekuuliza ukiajiri mfanyakazi wa ndani....?

Mantiki ya swali langu umeipata?

Ngoja niende Moja Kwa Moja Sasa,

NI KWANINI MKITENGANA MAHAKAMA ITAGAWA ZILE MALI ASILIMIA (%) KWA MUME ASILIMIA (%) KWA MKE. AMA NIKUULIZE KWANINI ITAZIGAWA MALI MUME APATE NA MKE APATE HAIJALISHI MKE ALIKUWA MAMA WA NYUMBANI AU LA?
 
Unajua kuna vitu ndugu Robert viko wazi kabisakabisa.

Nimekuuliza ukiajiri mfanyakazi wa ndani....?
Ushasema mfanyakazi, unajua tofauti ya mfanyakazi na Mkeo au Mumeo?
Wewe unapofua nguo zako mwenyewe unakuwa mfanyakazi?
Mantiki ya swali langu umeipata?

Hapo hakuna mantiki Mkûu.
Labda unashindwa kuweka hoja yako vizuri ikaeleweka.

Ukijifulia nguo zako au ukimfulia Mtoto wako nguo Nani anakulipa?
Ngoja niende Moja Kwa Moja Sasa,

NI KWANINI MKITENGANA MAHAKAMA ITAGAWA ZILE MALI ASILIMIA (%) KWA MUME ASILIMIA (%) KWA MKE. AMA NIKUULIZE KWANINI ITAZIGAWA MALI MUME APATE NA MKE APATE HAIJALISHI MKE ALIKUWA MAMA WA NYUMBANI AU LA?

Ungesoma àndiko langu Kwa utulivu maswali yôte uliyouliza nimeyajibu kwèñye Posti.
 
Nadhani wanawake wana shida fulani isiyoonekana. Imagine mwanamke akiachiwa tu hata uchi barabarani anatembea. Nenda social media utajionea mambo wanayofanya.

Akiwa na uhuru wa kifedha ataanza kuishambulia nyumba yake mwenyewe aibomoe, then akiibomoa anaanza kulialia tena na kulaumu wanaume, hapo malezi yatakua changamoto usishangae watoto wengi wenye shida ya maadili wamelelewa na single mothers.

Samahani mleta mada nimetoka nje ya mada, Ila hili nalo naomba mkalitazame.

Matatizo ya Wanawake mengi yanatokana na jamii na jinsi mfumo ulivyowaandaa.

Hao wanaotembea uchi NI Kwa sababu waliandaliwa kuwa chombo cha burudani na starehe
 
Haya mambo ya kukimbizana na Dunia ndiyo yametufikisha hapa.

Hoja ya msingi kwa mstakabali chanya ni heri kuwepo majukumu kwa wote ya kujipatia kipato, lakini yale ya mwanamke yawe na ukomo wa muda ili awajibike kuweka sawa mazingira ya familia na nyumbani.
Ndio maana hatakiwi Kula Kwa jasho yàani kufanya Kazi Kwa kuhangaika sana kama sisi wanaume

Kwa tathimini isiyo rasmi, familia zenye kipato kikubwa ndizo zina wahanga wengi wa madawa ya kulevya, wasagaji na mashoga.
Ukifuatilia kwa kina hayo ni matokeo ya malezi mabovu kwa sababu ya ubize wa wazazi wao kutafuta pesa na kumuachia dada wa kazi jukumu la malezi.

Mkuu nenda Tandale, Manzese, Magomeni, mwananyamala, Mbagala huki ûkifika utabadili mtazamo wako. Mashoga, wasagaji, mateja, punda wapo Huko na wanatoka familia Maskini Kuliko matajiri
Maisha siyo fedha tu, tuangalie namna bora ya kubalance pande zote.
Ni kwèli
 
  • Thanks
Reactions: K11
Ushasema mfanyakazi, unajua tofauti ya mfanyakazi na Mkeo au Mumeo?
Wewe unapofua nguo zako mwenyewe unakuwa mfanyakazi?

Hapo hakuna mantiki Mkûu.
Labda unashindwa kuweka hoja yako vizuri ikaeleweka.

Ukijifulia nguo zako au ukimfulia Mtoto wako nguo Nani anakulipa?

Ungesoma àndiko langu Kwa utulivu maswali yôte uliyouliza nimeyajibu kwèñye Posti.
Kichwa Cha Uzi wako kimesema mama wa nyumbani sio kazi kwakuwa hakuna kinachozalishwa.

Nikakuuliza swali la Moja Kwa Moja kwanini siku mmetengana mahakama itamgawia mama wa nyumbani Mali ambazo wewe baba ulifikiri kichwani mwako ndiye umezichuma lakini mahakama ikakutangulia kiakili kukuelekeza kuwa zile Mali mama wa nyumbani ameshiriki Kwa asilimia sawa na wewe?

Kwanza jifunze KUJUA dhumuni/purpose ya ndoa ni Nini. Ndio utajua unavyopotosha jamii.
 
Wewe ukienda kazini mkeo kama huwa anashinda nyumbani hapiki?hakuandalii nguo?watoto je?akiacha vyote hivyo ikiwa ni mkeo ingekuwaje?dada wa kazi ehhh? Mungu alikuwa na akili kubwa kusema wanawake wabaki majumbani kufuatilia familia zao Sasa hivi Kila mwanamke anatoka.....ulawiti ubakaji umeongezeka wanawake wamevaa nafasi ya mwanaume...Mnyazi Mungu tunusuru

Nipatie àndiko Moja tuu linalosema Mwanamke akae nyumbani au awe Mama WA nyumbani. Kwa Dini yoyote Ile. Íwe Kristo, yahudi, Hindu, budha, uislam, au Dini zetu za jadi.

Nipatie Hilo àndiko ili wasomaji na wachangiaji Wengine wajifunze alafu Mimi nitakuletea Aya za kutosha na Amri za Mungu zinazotaka Watu wôte kufanya Kazi.
 
Kichwa Cha Uzi wako kimesema mama wa nyumbani sio kazi kwakuwa hakuna kinachozalishwa.

Nikakuuliza swali la Moja Kwa Moja kwanini siku mmetengana mahakama itamgawia mama wa nyumbani Mali ambazo wewe baba ulifikiri kichwani mwako ndiye umezichuma lakini mahakama ikakutangulia kiakili kukuelekeza kuwa zile Mali mama wa nyumbani ameshiriki Kwa asilimia sawa na wewe?

Hakuna hiyo Sheria Mahakamani kuwa Mke aliyekaa nyumbani kama golikipa ati apewe Mgao Sawa na Mume aliyekuwa anafanya Kazi. Hiyo Sheria haipo.
Labda Stori za vijiweni.

Na hata Kwa mfano ikiwekwa Sheria ya namna hiyo. Itakuwa Imekiuka Haki za Umiliki.
Kwa sababu hakuna sababu ya maana hata Moja ya kugawa mali ya Mume Kwa Mke Asiyefanya Kazi au kugawa Mali ya Mke Kwa Mume Asiyefanya Kazi Kwa kisingizio cha kulea Watoto AMBAO NI wenu wôte.

Kama NI ushauri WA kufanikiwa siô kîla Mwanaume anapata na kuchukua ushauri Kwa Mkewe, wàpo wanachukua ushauri Kwa Mama zào kuliko Wake zào, wàpo wanaochukua ushauri Kwa marafiki zào.

Kuhusu kulea Watoto, nikuhakikishie kuwa Siku hizi familia nyingi zenye mafanikio zina Mayaya, Housegirl na houseboy.

Kwanza jifunze KUJUA dhumuni/purpose ya ndoa ni Nini. Ndio utajua unavyopotosha jamii.

Kasome Mithali 31 utajua kusudi la Ndoa NI nini?
Kisha kasome Kutoka 20:8 utajua aliyeumbiwa Afanye Kazi NI Nani?
 
Hakuna hiyo Sheria Mahakamani kuwa Mke aliyekaa nyumbani kama golikipa ati apewe Mgao Sawa na Mume aliyekuwa anafanya Kazi. Hiyo Sheria haipo.
Labda Stori za vijiweni.

Na hata Kwa mfano ikiwekwa Sheria ya namna hiyo. Itakuwa Imekiuka Haki za Umiliki.
Kwa sababu hakuna sababu ya maana hata Moja ya kugawa mali ya Mume Kwa Mke Asiyefanya Kazi au kugawa Mali ya Mke Kwa Mume Asiyefanya Kazi Kwa kisingizio cha kulea Watoto AMBAO NI wenu wôte.

Kama NI ushauri WA kufanikiwa siô kîla Mwanaume anapata na kuchukua ushauri Kwa Mkewe, wàpo wanachukua ushauri Kwa Mama zào kuliko Wake zào, wàpo wanaochukua ushauri Kwa marafiki zào.

Kuhusu kulea Watoto, nikuhakikishie kuwa Siku hizi familia nyingi zenye mafanikio zina Mayaya, Housegirl na houseboy.

Kasome Mithali 31 utajua kusudi la Ndoa NI nini?
Kisha kasome Kutoka 20:8 utajua aliyeumbiwa Afanye Kazi NI Nani?
Ngoja kwanza, kwani unataka mke afanyie kazi Ili iweje?

Wewe umeshindwa kufanya kazi au?

Na bado Utaajiri house girl ikiwa mke wako atafanya kazi kama wewe?
 
Ngoja kwanza, kwani unataka mke afanyie kazi Ili iweje?

Wewe umeshindwa kufanya kazi au?

Na bado Utaajiri house girl ikiwa mke wako atafanya kazi kama wewe?

Mke ni binadamu na ni mtu ndio maana lazima afanye kazi.

Mke anafanya kazi kwaajili yake mwenyewe ili ajitegemee.

Upo Karne ya 21 Bado unauliza swali mwanamke afanye kazi ili iweje?
Hizo shule mlienda kusomea ujinga wa ajabu sana.

Uliza serikali kwa NINI inataka kumkomboa mwanamke kutoka kwenye wanaume wajinga
 
Wewe ukienda kazini mkeo kama huwa anashinda nyumbani hapiki?hakuandalii nguo?watoto je?akiacha vyote hivyo ikiwa ni mkeo ingekuwaje?dada wa kazi ehhh? Mungu alikuwa na akili kubwa kusema wanawake wabaki majumbani kufuatilia familia zao Sasa hivi Kila mwanamke anatoka.....ulawiti ubakaji umeongezeka wanawake wamevaa nafasi ya mwanaume...Mnyazi Mungu tunusuru
Wapi Mungu alisema wanawake wasifanye kazi mkuu au unaropoka usichokijua
 
Mke ni binadamu na ni mtu ndio maana lazima afanye kazi.

Mke anafanya kazi kwaajili yake mwenyewe ili ajitegemee.

Upo Karne ya 21 Bado unauliza swali mwanamke afanye kazi ili iweje?
Hizo shule mlienda kusomea ujinga wa ajabu sana.

Uliza serikali kwa NINI inataka kumkomboa mwanamke kutoka kwenye wanaume wajinga
Kwanza yakiwekwa matokeo yangu na Yako kuanzia primary Hadi chuo kikuu nauhakika hakuna mahali utanikaribia Kwa ufaulu.

Sitaki kuongea mengi.

Ni kwamba wewe hauna hela, na hoja zako hizi zinadhihirisha huna Hela na unakwepa jukumu la kumhudumia mke Kwa 100%. Mke ambaye manufacturer wetu kamuumba kama Kiumbe Cha kupokea tu, Leo unataka awe wa kutoa.

Unakoelekea utadai Wanawake wawe wanatoa MAHARI.

Tafuta Hela Robert uwe tajiri utakuja KUJUA Raha ya mama wa nyumbani.

Hakuna Mwanamke anayefanya kazi huko kazini akawa salama.
 
Mwanamke sio kiumbe Cha kupokea tu , Bali anapaswa ajitegemee. MTU asiyeweza kujitegemea Ni mtumwa. Na ndio wanasababisha umaskini katika nchi yetu. Je mwanamke asipoolewa atapokea wapi? Je mine wake akifa atapokea wapi?
 
Back
Top Bottom