Sio kila hustle wife ajue eti kisa mnapendana. Kuna misala mingi kama mwanaume unatakiwa usimame mwenyewe tu mradi wao wasilale njaa.
Kusema kila kitu sio uanaume. Binafsi nilipataga msala job wife alijua nipo likizo ndio baadae nikamwambia nimesimamishwa kazi.
Hata baadae nilipotimuliwa alijua ni kwa sababu niliyokua nimemwambia kumbe sababu ni nyingine kabisa ambayo alikuja kuijua kama 4yrs later wakati maisha yalishasonga kivingine.
Alijua baada ya kufungua makabrasha yangu kwenye briefcase alishangaa sana kujua kumbe nilikua na msala mkubwa kiasi kile na niliwezaje kupretend niko normal. Ulikua msala mzito wa kula mvua za kutosha ila niliupangua kivyangu na hadi leo akiniangalia hanimalizi