Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Maandamano yanayoendelea kumshinikiza Rais William Ruto kuondoka ofisini yana tija kubwa kwa Kenya na fundisho kwa Serikali ya CCM kuelekea 2025.
Wanachokiandamia ni kukithiri kwa ufisadi na maisha ya anasa ya viongozi wao hasa wanasiasa.
Vijana hao wakiwa katika lindi la umasikini lakini viongozi wao wakiogolea kwenye fedha zao sawa na yule kigogo wa TRA aliyekutwa bilioni 7 nyumbani kwake.
Hakuna wanachokidai kisichokuwepo Tanzania. Kwa hakika waliotakiwa kuandamana kwa wingi wao ni vijana wa Tanzania. Laiti kama wangetumia wingi wao wa kwenye Simba na Yanga kudai haki yao inayoporwa na mafisadi hakika tungekuwa na mabadiliko chanya na ya haraka.
Ifike mahali sasa tuanze kuwachochea vijana hawa kuondoa woga kudai haki zao na kupambana na ufisadi na mafisadi. Tuwaambie wajifunze Kenya ambako naamini hali ikiendelea hivi sitoshangaa Rais Ruto akiomba hifadhi Magogoni.
Laiti nyumbu wangejua wao ni wengi kuliko simba mmoja kamwe wasingemuogopa Simba na badala yake wangemkabili, kumshambulia na kumtimua asimdhuru hata nyumbu mmoja.