Kazi ya kununua ilo

Kazi ya kununua ilo

banalunda

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
231
Reaction score
67
Wanajamvi habari za majukumu? Kuna jamaa yangu mmoja ana bachelor, ameepata jamaa mmjoja anayefanya kazi ILO akamwambia kuwa kuna nafasi ya kazi kwenye upande wa administrative ila anatakiwa ainunue kwa 1M the wasaini mkataba wa kazi then aanze kazi. Hebu niambieni mnalionaje hili....
 
Mwambie ajihadhari na Matapeli. Na kama deal iko straight mwambie asilaze damu, mjini mipango...
 
Kuna sehemu za kununua kazi sio uko,tena kwa pesa ndogo kama iyo.
 
waandikishiane as ana mkopesha ili once akikosa hiyo kazi amdai.
 
Jamii forum watu wanafiki mno mmezidi unafiki!!
Hivi ule ufisadi mnaouona ni ule wa rostam, EL na Ridhiwani, ila nyie kwenda kutoa Rushwa mnashauriana na kuona ni haki yenu, hivi angekuwa EL, or Ridhiwani au Rostam mngekomaa nae mkimuita fisadi ila nyie sawa tu haina shida..........Wanafiki wakubwa nyie...............................................................................................................................
Wewe jamaa uliyeanzusha hii thread mnakifi mkubwa tena fisadi, sisi tunapambana na udhalimu na ufisadi wewe unataka tukusapoti.Kafie mbali fisadi mkubwa wewe na huyo ndugu yako
 
Ajihadhari kabisa kwa hilo vinginevyo changa la macho. Sijawahi sikia kwenye UN agency yoyote kuna kitu kama hicho. Watu matapeli sana siku hizi!!
 
ukishatoa hiyo rushwa kisha utirudishaje?
watanzania mwogopeni Mungu.rushwa ni dhambi tena adui wa maendeleo.
ukishapata kazi kwa rushwa nawe utatoa kazi kwa rushwa.kisha utaendelea kupanda mbegu hiyo kwa wengine.
wewe ni mtu wa kuogopwa kama ukoma.rushwa sio jambo la kujadili ni la kuepukwa na kukimbiwa mara moja.
ushauri wangu;mreport kwa takukuru na watakupa mbinu ya kumtia hatiani.
 
Anaingizwa mjini huyo. UN agencies kama ILO si kama serikali ya you know who! Just go the right way bwana! Hiyo nguvu aliyotumia kutafuta njia za panya aitie katika kutafuta kazi za halali ambazo hata akipata atatulia tuli si kuwa anashtuka shtuka kila saa. TOBA!:shut-mouth:
 
Anaingizwa mjini huyo. UN agencies kama ILO si kama serikali ya you know who! Just go the right way bwana! Hiyo nguvu aliyotumia kutafuta njia za panya aitie katika kutafuta kazi za halali ambazo hata akipata atatulia tuli si kuwa anashtuka shtuka kila saa. TOBA!:shut-mouth:



Kuna wahaya pale ILO wanauza kazi za Reseach assistant kama njugu!..mnaobisha hamuwajui vizuri mnadhani wanaofanya pale ni wazungu? zinauzwa sana tu ila ndio hivyo kazi zenyewe za mikataba mifupi hazilipi!
 
Kununua kazi, na wewe unakubali? ama kweli, imefikia hapo? ngoja nichekeche kidogo, nitarudi!
 
Back
Top Bottom