nguvu ya buku
Senior Member
- Jul 15, 2025
- 168
- 549
Producer: Upo aje bro, uko tayari?
Msanii: Ah niko full kabisa, lakini kuna kipengere, hapa sina cash ila kuna mchongo nausikilizia ntakulipa Alhamis.
Producer: wala usihofu, Najua unahaso, tunasaidiana na we do it for the game, laza michano kwenye beat.
Msanii: Sawa ndugu, Mic test, one two three... Eeh, nipe beat mwanangu,
BEAT LINAANZA
Wananita milionea, si mchezo si ndoto,
Jicho nyanya nimelegea, sina presha na arosto.
Ngoma zangu ni moto, studio inanukia,
Studio sina malipo, beat napewa naipumulia.
Maproducer wananikubali, nawakuza majina,
Heshima ya tai, namimina vina.
Milioni kwenye mfuko, ni kawaida si bahati,
Suruali imebeba mzigo, sihitaji kubeti.
Wananita legendari, maneno si hadithi,
Kwenye game ni kamati, wananipa kiti.
Nipo juu kama dari, siangalii chini,
zima biti, nishamaliza verse bila senti