Kazi ya ulinzi ndugu zangu sio kazi wallah

Kazi ya ulinzi ndugu zangu sio kazi wallah

Acha tu mkuu,huwa nawahurumia sana watu wanaolala nje..kuna siku nilikua njombe ,nikapita mitaa flani nikaona watu wako nje wanalinda maduka huku wamewasha moto,nikajisemea hawa watu Mungu awalinde tu kwa lile baridi la njombe ni hatari kuwa nje usiku mzima.
Very sad ila ndiyo maisha
 
wakati nachukua basic ilikuwa 150 nilichukua 2m asaiv wamepandisha basic 220 Kwa hiyo unaweza kukopa mbaka kiufupi tulipewa wenye miaka kuanzia mitatu kama sijakosea ila walikuwa wanaangalia mshahara wako Kwa asaiv tangu upande mshahara wanakopesha mbaka m7 ila wana top up Kwa ambao hawajamaliza mikopo Kwa si tulio maliza hawakopeshi tena ila Kwa mlinzi wa kawaida ana top up mbaka m5_6
Nakushauri kwa mshahara huo usikope.mkopo wa zaidi ya miezi 36.
Maana utakatwa muda usiopunfua miez 108. Chukua mkopo wa miezi michache. Japo utapata hela kidogo lakini utakwepa riba kubwa
 
Madenge bana akinisaidia Shughuli pale Ofisini kwangu nampatia kaposho kulingana na tulichoingiza siku hiyo, Basi bana siku moja akaja niambia kaka ee nimepata kazi ya Ulinzi kwa Mwarabu Kirumba pale mshahara laki tatu, nikamwambia haina neno kaka kakomae maana hapa deiwaka siku nyingine tunatoka Patupu, akaenda wakawa wawili siku ya kwanza Fresh tu, ya pili Fresh tu dah zikapita kama siku sita hivi, Madenge anakwambia siku hiyo wametulia windo na Mwenzake wanakuja kustuka saa nne asubuhi wamezungukwa na Askali hawafaham walisinzia saa ngapi Vibaka waliwapiga dawa za usingizi wamechomoa chomoa kila kitu kwenye Magari tajili anataka alipwe vitu vyake ndio watu kuwaambia huu mtaa ulishashindikana kwa Vibaka hakuna mtu atakubali kulinda huku! Hawa jamaa wanapitia changamoto sana!!
 
Inategemea na kampuni unayofanyia Kuna kampuni kubwa kama GARDA WORLD, G4S ,security group SGA, SUMA JKT n.k Kuna rafiki zangu wanafanya kazi huko kitengo cha IT na wengine walinzi.

Walinzi unaozungumzia wewe ni wale wa kampuni kama MOKU ,KAMANDA SECURITY na zingine za wazawa.
Kwahiyo unataka kusema Suma Jkt ni kampuni kubwa ? 😆😆😆Mshahara laki 2 kavu ,si bora ungesemea SGA,GARDA NA G4S ambao international kimo cha basic 222k
 
Uzi wetu huu walalahoi. Inaleta faraja walalahoi wenye hali zinazofanana mmekaa pamoja mnapiga stori za kufarijiana.

Big up walalahoi wenzangu
 
Back
Top Bottom