Kazi za BOT zilizopitia utumishi walisema wanataka watu wa Upper Second, First Class tu. Mbona na sisi wenye Lower Second system ilituruhusu kuomba?

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,275
Reaction score
3,316
Hali zenu wandugu?

Kuna tangazo la kazi za BOT zilitangazwa na Ajira portal,lile tangazo lilisema wanatakiwa kuapply watu wenye upper and first class pekee, ila cha kushangaza mfumo uliruhusu mtu yeyote mwenye degree tajwa aombe.

Hivi tunaweza kuitwa kweli kwenye usaili, na imekuaje mpaka ajira za BOT zinapitia utumishi wakati wao huwa wanaajiri wenyewe?

Asante
 
Kama zimepitia utumishi mnaweza kuitwa ilimradi mfumo umekukubali kuomba,maana utumishi ni zoazoa.
 
Usipoteze muda wako bure kama huna upper second class system yenyewe inaselect kila mtu mwenye degree husika ila gpa ukienda interview lazima watakagua tu. Hata kama wakikuruhusu ufanye usaili ikipita lazima muajiri akague kama umekidhi vigezo.
2021 System iliniselect tutorial assistant required Gpa ilikuwa 3.8 mimi nilikuwa na 3.5 nikafukuzwa wakati wa interview
 
Wewe unafikri kuomba ndo kupata kazi, vyeti vyako vitakaguliwa kwenye hatua za usaili zote mpaka utakapopeleka barua ya utambulisho kutoka utumishi bado utakaguliwa vyeti hivyo hata kama wakikuita kwenye interview usijisumbue kwenda mkuu
 
Hata TRA zamani walikua wanachukua only first and second class pekee,ila siku hizi wanachukua hata pass ilimradi ufaulu interview.
So huenda na hao BOT wamebadilika.
 
Hali zenu wandugu?
Kuna tangazo la kazi za BOT zilitangazwa na Ajira portal,lile tangazo lilisema wanatakiwa kuapply watu wenye upper and first class pekee, ila cha kushangaza mfumo uliruhusu mtu yeyote mwenye degree tajwa aombe.

Hivi tunaweza kuitwa kweli kwenye usaili, na imekuaje mpaka ajira za BOT zinapitia utumishi wakati wao huwa wanaajiri wenyewe?

Asante
Kuomba ni initial step. Kwenye mchujo ndio wata apply wanachokitaka
 
Majina Yametoka vp wamekuita?

Hali zenu wandugu?

Kuna tangazo la kazi za BOT zilitangazwa na Ajira portal,lile tangazo lilisema wanatakiwa kuapply watu wenye upper and first class pekee, ila cha kushangaza mfumo uliruhusu mtu yeyote mwenye degree tajwa aombe.

Hivi tunaweza kuitwa kweli kwenye usaili, na imekuaje mpaka ajira za BOT zinapitia utumishi wakati wao huwa wanaajiri wenyewe?

Asante
 
Kuna mdogo wangu aliitwa interview ya assistant lecture Mzumbe.

Yeye undergraduate alikuwa na GPA 3.7 ila alikuwa na masters yenye GPA kubwa. Na alikuwa ana uzoefu wa miaka mitano. Maana alikuwa anafundisha private university moja maarufu

Kabla ya interview ya Mzumbe wakakagua vyeti. Walipoona GPA yake ya degree ya kwanza ilivyo wakamfukuza kwenye interview.
 
Hali zenu wandugu?

Kuna tangazo la kazi za BOT zilitangazwa na Ajira portal,lile tangazo lilisema wanatakiwa kuapply watu wenye upper and first class pekee, ila cha kushangaza mfumo uliruhusu mtu yeyote mwenye degree tajwa aombe.

Hivi tunaweza kuitwa kweli kwenye usaili, na imekuaje mpaka ajira za BOT zinapitia utumishi wakati wao huwa wanaajiri wenyewe?

Asante
Subiri tu pale sehemu inayoandika shortlist itakupa jibu kamili. Ila uhakika ni kwamba hautotoboa
 
Back
Top Bottom