mtu ambaye si mwanasheria anakuwa mwanasheria mkuu, eh eh eh!!
Icho chuo kweli ni kipya, yaani hata mahakama haikutambui kama afisa katika ngazi yoyote ya sheria.
Kwa kuwa uko first year unaingia II nakushauri wewe wala usiwe na kiherehere kwenye maamuzi, wakiita kikao cha uogozi wewe nenda, saini kula allowance, lala mbele...
Usichukulie mzaha kusaini document za kisheria, ikumbukwe vyuo vyote uanzishwa chini ya sheria ivyo ukijiita mwanasheria mkuu siku taasisi yenu imepelekwa mahakamani kwa shauri lolote liwalo/ Mungu epusha ...itatakiwa documents na kama utakutwa umesaini kama mwanasheria wa taasisi wakati wewe sio mwanasheria, na mbaya zaidi izi serikali za wanafunzi zina mihuri, na umechongewa muhuri umesaini 'Mwanasheria' duuhh mziki wake hautatosha... utatakiwa kudhibitisha profession yako na itakutia hatiani.
Kwa kuwa mwaka wa kwanza nategema hauwezi kuwa legal consultant ivo usitoe maoni kama mwanasheria wa taasisi, wewe fanya majukumu utakayopewa na katiba ya serikali ya wanafunzi kama yapo, na kila serikali ya wanafunzi lazima isajili katiba ivyo pitia uko utajua majukumu yako.
Samahani kama ntakuwa nimekuudhi au kukosea popote!!