Kazi za ovyo kwenye nchi hii

Kazi za ovyo kwenye nchi hii

MAWEED

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
3,550
Reaction score
12,239
Assalaam aleykum,

Wanajamvi leo acha tuongee ukweli hata kama tutakwazana ila tutajua tu. Kuna kazi ukikubali kufanya au kuajiriwa ni mateso/za hovyo na huwezi kutoboa labda uende kinyume na sheria, hakuna marupurupu, mishahara midogo na mazingira ya kazi yamekaa kimtego mtego sana.

1. ASKARI POLISI

i. Magereza.
ii. Trafiki

2. WALIMU (kufundisha)

Hizi kazi watumishi wake wamejaa njaa, dhiki, ulafi na shida tupu.

3.
4.
5.
 
Huwezi kuniamrisha paka we...ndo mnavotakiwa kujibiwa
Moderator inabidi muwe mnavifungia vithread vya hovyo hovyo kama hivi maana vinatujazia servers zetu za JF.

Hawa vibaka waliopata ajira Jw na wenzao wa PT akina mkorinto waende wakabishane huko Facebook maana hapa inaonekana haraka haraka huyu dada MAWEED ameshakalishwa na matraffic huko
 
2.WALIMU(kufundisha)
Hizi kazi watumishi wake wamejaa njaa,dhiki,ulafi na shida tupu...😆😆😆😆
 
Ukiwa mmiliki wa gari utaona kazi ya mpiga debe ni kazi mbaya na utamuona mpiga debe ni kama mtu asie na malengo na maisha yake, Ila kwake yeye hiyo ndo kazi inayompa heshima na anailisha familia yake na kaepuka na aibu za kuanika shida zake mbele za watu.

Ndo maana dunia hii mtu hutakiwi kudharau kazi unayoifanya hata kama wanao kuzunguka wanaidharau maana ukiiacha kazi kwaajili ya watu wanaidharau hao walioidharau kazi yako hawatakupa hela ya kusogeza maisha yako
 
Kuajiriwa kiujumla hakulipi hata kama mshahara wako ni 12 mil

Unapoajiriwa ina maana mwajiri wako kanunua muda wako,hivyo kufanya mambo yako ni ngumu utaishia tu kwenye huo mshahara wake
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Endelea kuota ,,, yani mtu akupe 12M kwa mwezi kwa kukaa kwenye laptop tu na full ac!

Halafu useme utashindwa kufanya mambo yako? Kama hio hela unaiona ndogo watu na elimu zao wasingeroga kupata ubunge.
 
Back
Top Bottom