Kazi zenye changamoto ya kutoboa

Wote watatoboa muda ukifika mkuu, hiyo ni njia tu ya kuanzia kuna sehemu wanakwenda. Hawatakaa hapo milele. Hakuna aliye fanikiwa aliye anzia pazuri, wote walianzia chini. Huyo bodaboda kuna siku atafungua show room ya bodaboda. Wape muda, hata muuza karanga mpe muda. Biashara yeyote ni majaribio yanayo mpa mtu uzoefu wa kujua jinsi pesa inavyo zunguka.
 
duh mkuu umeandika kwa uchungu sana. anyway, kazi ndiyo hutupa heshima. tufanye kazi kwa ujenzi wa taifa.
 
Kwa wale wanaotoka maeneo yenye viwanda,madini uwa wanachukua mgao wao wa kimtindo achilia mbali 10% ya mauziano ya ardhi pamoja na magumashi yao ya ku backdate ardhi za watu kisha kuuza kwa wengine.
 
Kwa wale wanaotoka maeneo yenye viwanda,madini uwa wanachukua mgao wao wa kimtindo achilia mbali 10% ya mauziano ya ardhi pamoja na magumashi yao ya ku backdate ardhi za watu kisha kuuza kwa wengine.
Wenyeviti wa mtaa
 
Kingine ni kwamba watu wanafanya kazi sio kuwa matajiri bali ni ili waweze kusurvive na kuweza kulipa kodi, kula na kuvaa na kama wana familia ili watoto wale, wavae nguo na wapate nauli za mwenda shule za serikali. Pia waweze kumudu matibabu ya kawaida.

Tena wana maisha ya furaha na umri mrefu kuliko matajiri.

Watu kama hao wakikosa hiyo kazi maisha yanakuwa magumu zaidi na wanaweza kuiba, kufanya uhalifu, kujiuza kwa wanawake, au hata kufa kwa njaa au magonjwa ya msongo wa mawazo. Hivyo, pamoja na kwamba hawatatoboa ila kufanya kazi ni lazima. Na ndio maana umesema katika andiko lako kuwa kazi za viwandani huwakuta watu nje wanagombania kuingia na wasipochaguliwa hurudi nyumbani au kijiweni.
 
Bado kuna vijiji ujafika uangalie wafanyabiashara vijijini walivyo na maisha kuliko hao uliowataja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…