Keenja na Binti yake Eliaisa

Cha maana pasi yake ya kusafiria imeshawekwa kapuni..sasa sheria ifuate mkondo wake..na kibaya zaidi vyombo vya habari vishajua kuwa kuna kaharufu ka mchezo mchafu..stay tuned

It is a pity Mjadala huu sikuuona on time!

Inawezekana wachangiaji tukawa hatuwatendei haki watanzania wenzetu kwa kutokufahamu! Kwanza ikumbukwe kuwa huyu mtoto wa Keenja ameshitakiwa akiwa anatekeleza wajibu wake kwa mwajiri wake, National Housing Cooperation (NHC)! Kimsingi angetakiwa alindwe na ajira yake kwa vile walimuondoa mpangaji wa NHC akiwa kazini. Mchina aliondolewa kwenye nyumba ya NHC baada ya kukiuka taratibu za upangaji. Aliondolewa kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kuhusisha ofisi ya serikali za mitaa na kumpa taarifa ya kimaandishi. Yeye (mchina) aliandaa orodha kubwa ya vitu alivyodai kupotea kutokana na zoezi hilo ambayo ilikuwa tofauti kabisa na ile iliyosimamiwa na NHC, Dalali na ofisi ya serikali ya mitaa! Aidha Dalali ndiye aliyehusika moja kwa moja ktk kufunga milango.

Mchina alifungua kesi ya madai dhidi ya NHC na dalali. Katika hali inayoweza kuchukuliwa kama ni lengo la kuwakomoa watendaji waliohusika, alifungua kesi ya wizi dhidi ya mfanyakazi wa NHC (ambaye ni Eliaisa Keenja) na dalali wa NHC kama individuals.

Mimi sio mwanasheria lakini nimeifuatilia kesi hii kwa ukaribu sana na kushangazwa na taswira inayojengwa dhidi ya watu wasio na hatia. Waandishi wa habari walioko JF watanisamehe lakini Mchina amekuwa akiwapa waandishi "her side of story" na wao kukimbilia kuandika magazetini bila ya kujali athari zake.

Hebu tujenge picha kuwa wewe katika kutimiza majukumu yako ya kawaida ukafunguliwa mashtaka ya kuiba mamilioni ya shilingi na kuwekwa rumande (by the way Eliaisa alishalala rumande siku za njuma ktk mashtaka haya haya!), ufiwe na mume wako halafu hapohapo uwekwe ndani! kama hiyo haitoshi unahukumiwa na umma kupitia magazeti na mtandao kama mwizi!

Siyaandiki haya kwa vile Eliaisa ni rafiki yangu bali ni sehemu ya habari ambayo hatuisikii. Tunachokisikia ndicho kinachotufanya tuyaseme tunayoyasema humu!

Vyombo vya habari vingeweza kufanya kazi nzuri zaidi hata kama MCHINA ni mshikaji wao!
 

Kumbe ukweli wenyewe ndio huu ?
Pole sana dada Eliaisa Keenja.
 


Kisutu court comes clean on Keenja's bail
DAILY NEWS
Faustine Kapama
Thursday,March 27, 2008 @19:01

...Giving clarification on the matter, Magistrate Mwangesi said that after cancellation of accused's bail, her father and advocate approached him for intervention. According to him, he told them that what was decided by the magistrate was legally a court's order and the available remedies were for them to go to the High Court to either appeal against the order or file revision proceedings.

When they went to the High Court, he said, Judge Kaijage called him to inquire about the case and asked him whether there was any necessity for the High Court to call for the court records for revision purposes. "I told him to wait to allow me to communicate with the trial magistrate to see whether or not she could exercise her powers to review her order, which is normal and legal procedure," he said.

The magistrate further said that the High Court would have called for the file had the trial magistrate stuck to her guns. However, he said, after communicating with her she agreed to consider the matter. "It was at that point when the judge directed the aggrieved party to go back to the magistrate to seek review of the orders given. So there was no directive to us on this point," Mr Mwangesi said.

Indeed, he said, the parties went back to magistrate Beda and submitted their application, alleging that the accused was mourning her husband who died recently. The magistrate granted their application and granted bail to the accused on conditions of securing two reliable sureties who signed bond of 20m/- each. She also ordered her to surrender any travel document to the court. Thereafter, the magistrate withdrew from presiding over the case. No reasons were advanced, as the magistrate declined to comment when reached.


Dume la Mbegu;
Unaongelea nyeti za kesi yenyewe na sababu za kuomba dhamana. Wengine tunaongelea mahakimu walivyo dhihaki haki na sheria kwa kuruhusu baba mtu kuingilia kesi na baadae msemaji wa serikali kupinda ukweli kuhusu utaratibu ulivyo.

Kufiwa na mume, ukauzu wa Mchina, utupu wa vyombo vya habari, na mwajiri asiyejali ni mambo ya kusikitisha lakini hayasemi lolote kuhusu utaratibu – au shaghala bagala – ililyotumika kutoa dhamana.

Baba mtu hakutakiwa kuongea na majaji Mahakama Kuu kwa sababu ni wakili tu anaweza kumuongelea mtuhumiwa. Mahakama kuu haikutakiwa kumtafuta hakimu kwa niaba ya mtuhumiwa halafu kumwambia binti Keenja haya rudi kule kwa hakimu kapeleke ombi lako, tumesha ongea nao. Tayari hapa kuna ushaweishi wa Mahakama kuu, ndio maana hakimu akakubali halafu akajitoa.

Mahakama Kuu haikutakiwa kumuuliza Hakimu ‘eti unaweza kupitia ule uamuzi wako tena.’ Mahakama kuu ikisha jiingiza tuu, hivi vitu vinatakiwa viwe kwenye maagizo rasmi ya Jaji kumuamuru hakimu apitie upya uamuzi wake. Sio kupigiana simu (hapa mawasiliano na maamuzi na kutengua maamuzi yalifanyika ndani ya masaa tu). Hivi ni vitu vya msingi mno, na majaji wanapovipinda wazi wazi ni dhihaka kwa sheria.

Ni kweli Hakimu anaweza kutengua uamuzi wake, lakini sio utaratibu kwa Jaji kujiingiza kinyemela nyemela huku akiepuka kuacha alama za vidole kwenye makaratasi au kwa kumtuma Mwangesi awasiliane na Hakimu. Wakili wa binti Keenja sio mjinga kumpeleka Mheshimiwa Keenja kwa majaji Mahakama Kuu kabla ya kuleta pingamizi kwa Hakimu. Huyu wakili kwani hajui kwamba angeweza kupinga kule kule kwa hakimu, utaratibu anaoungelea Mwangesi? Tafadhali!

Sasa kama binti Keenja keba hela au ni Mchina ndio fidhuli hayo yatajulikana mbele, lakini sio kuanza kudhihaki haki na sheria kwa vile mtuhumuwa babake Keenja

 
"Baba mtu hakutakiwa kuongea na majaji Mahakama Kuu kwa sababu ni wakili tu anaweza kumuongelea mtuhumiwa"

Kuhani Mkuu, sijui kama unauhakika kuwa wakili hakuwa sehemu ya jitihada hizo za kumpatia mteja wake dhamana na lets face it, wewe mtoto wako akitaka kuwekwa "ndani" kwa sababu yoyote ile utakaa nyumbani na kunywa kahawa ukipiga mluzi!? Umeshaenda mahakamani na kushuhudia idadi ya watu wanaoenda kusikiliza kesi zinazoendeshwa? Idadi kubwa ya watu hao wanakuwa wanaguswa kwa njia moja au nyingine: wengine wakitaka wapendwa wao washitakiwa waachiwe huru, n.k. Hivyo baba ya mtoto akiwa mlalahoi, tajiri, maarufu, kigogo, nk naye angependa kikombe cha moto kisimwangulie binti yake. Nampa BIG UP sana Keenja katika hili.

Mahakama kuu haikutakiwa kumtafuta hakimu kwa niaba ya mtuhumiwa

Nijuavyo mimi (Kuhani Mkuu unaweza kunisahihisha) hakimu alifuta dhamana kwa vile Mshitakiwa alishindwa kuhudhuria kesi. Kipindi cha nyuma mshitakiwa alikuwa ameomba ruhusa mahakamani ya kwenda kutibiwa kesi ikiwa inasikilizwa na hakimu wa awali, Mahai na ruhusa ilitolewa lakini bila kumbukumbu yoyote kuwekwa kwenye faili la mashitaka. Pia kesi ilisikilizwa siku ya mazishi ya mume wa mshitakiwa na mahakama ilijulishwa. Siku iliyofuata ya kusikilizwa kesi hakimu akaamua kufuta kesi bila ya ombi hilo kutoka upande wa mashitaka. Inawezekana ni ktk mazingira haya mahakama kuu ikaomba hakimu apitie upya uamuzi wake. Dhamana ni haki ya mshitakiwa.

Ni kweli Hakimu anaweza kutengua uamuzi wake
Yaa, anaweza ndio maana alifanya hivyo.

"Sasa kama binti Keenja keba hela au ni Mchina ndio fidhuli hayo yatajulikana mbele"

Ni kweli haya yatajulikana hapo baadae lakini hakimu wa awali , Mahai (kabla ya huyu aliyejitoa) alitaka udhibitisho kama Mchina amefungua kesi nyingine ya madai dhidi ya NHC ili afute kesi hii kwa vile haina legal right ya kuwepo kesi ya pili yenye watuhumiwa tofauti juu ya issue ile ile.

"sio kuanza kudhihaki haki na sheria kwa vile mtuhumuwa babake Keenja"

Nakuunga mkono, Kuhani katika hili lakini nani asiyejua juu ya ukweli kuwa magereza na mahabusu yamejaa watu wasio na hatia! Kuna wanaosema kuwa "mahakamani za Tanzania kuna SHERIA na sio HAKI"! Mimi ni mmoja wa memba ya klabu inayokubaliana na usemi huu. Karibu Kuhani kwenye klabu.
 
Dume la Mbegu

Ninakushukuru kwa kuweka mwanga katika hili suala kwa vile wengi tulishaanza kuwa na mawazo mbalimbali!

Natoa pole zangu kwa Bi. Elisha kwa yaliyomkuta lakini ndio dunia, sio!

Mzee Keenja jina lake nalo limeburuzwa vilivyo kwenye vyombo vya habari utafikiri ameua! Lets give huyu mzee a break! Ametumikia taifa vya kutosha katika ngazi mbalimbali na hastahili haya tunayoyaona! Sisi tuliobahatika kufanya nae kazi tunamwelewa vema utendaji na uadilifu wake. Nani asiyekumbuka hali ya jiji letu miaka ileee mpaka tukafikiri limelaaniwa! Naambiwa alifanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji ndani ya wizara ya kilimo iliyomfanya kuchukiwa na baadhi ya vigogo waliozoea kuchota fedha za mifuko kama IMPORT SUPPORT na AGRICULTURE INPUT SUPPORT.

Namuheshimu sana mzee huyu kwa vile huwa tunaona matokeo ya kazi zake bila ya yeye kuweka utaratibu ya kujikosha kwenye vyombo vya habari kama wanasiasa wengi wanavyofanya!
 
hiii yote ni jitihada za akina kundi la lowasa na wenzake kuwachafua wenzao ili tusahau ya richmond
 
Watanzania tuwe na la kusema, habari ya kusoma au kula maisha ni jambo la lake binafsi,jambo la msingi ni kwanini Keenja ailazimishe mahakama impe dhamana? au ni kwa sababu baba yake amewahi kuwa waziri? sasa sisi watoto wa walala hoi twende wapi?
 
Utafiti kabla ya kusema ni kitu kizuri sana,otherwise ni rahisi mno kuharibu haiba ya JF mbele ya jamii kama kutaletwa habari ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha...wana JF tujitahidi kuandika hoja zilizotafitiwa vema tusiwe na haraka....Mfano ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuthibitisha kuwa uamuzi wa jaji ulitokana na shinikizo la Keenja na si mtazamo wa Jaji ?
 

Jaji hakutakiwa kabisa kujadili na baba mtu kuhusu kesi ya mtoto. Ilibidi baba asubiri nje ya ofisi, wakili ndio aingie.

Tena ni kwa sababu nchi yetu nayo masikini katika misingi ya sheria. Vinginevyo, hata huyo wakili nae hakutakiwa kuwasiliana na Jaji kienyeji. Unaongea na Jaji ndani ya koti, tena una file a motion rasmi, sio kwa mazungumzo ya faragha.

Hatujui kama baba mtu alishinikiza. Lakini sababu ya kuwepo ustaarabu wa kukutana na Jaji mahakamani - na wakili sio Baba - ni kuepuka shuku shuku za yasiyo stahili (appearance of impropriety) kama haya.

Moja ya milingoti ya maadili ya maofisa wote wa sheria, ni kwamba wanatakiwa wawe juu ya hata 'appearance of impropriety.' Na Jaji ndie kinara wa hao maofisa wa sheria.

Jaji Kaijage analijua hili vizuri tu. Ni kwa sababu anajua watu hawafuatilii vitu kama hivi ndio maana wanapeta na mikorogo kama hii.
 

Nashukuru Dume la Mbegu kwa ufahamisho wako wa kina. Inaelekea unaijua vyema kesi hii ilivyo na umetumia busara na ujuzi wako kuelimisha wana JF vizuri. Ninavyoifahamu kesi hiyo ilivyo, hakuna ukweli zaidi ya ule uliotolewa nawe mkuu.
 
Nashukuru Dume la Mbegu kwa ufahamisho wako wa kina. Inaelekea unaijua vyema kesi hii ilivyo na umetumia busara na ujuzi wako kuelimisha wana JF vizuri. Ninavyoifahamu kesi hiyo ilivyo, hakuna ukweli zaidi ya ule uliotolewa nawe mkuu.


Amani Keenja, karibu tena JF. Wewe unaweza kutupa undani zaidi kuhusu kesi inayomkabili dada yako

PM
 
Amani Keenja, karibu tena JF. Wewe unaweza kutupa undani zaidi kuhusu kesi inayomkabili dada yako

PM

Ahsante kwa kujitokeza AmaniK naamini kulikuwa na upotoshaji wa ukweli wa kesi hii.Naomba wape mwanga wale waliokuwa wanaopotosha ukweli.Kenny
 
Kwa mtu yeyote kuona mwanao anawekwa ndani ni lazima uhangaike. hata kama huna jinsi ya kuwaona hao majaji ni lazima utaangaika kwa namna yako utakayoweza kwana uchungu wa mwana aujua mzani. sioni kama kitu alichofanya Keenja ni cha ajabu, labda kama mtu hana uchungu na mtoto wake na huyo atakuwa abnormal
 

Nakuunga mkono, Mkuu, siamini kuwa majaji waliohusika na maamuzi hayo walishinikizwa ktk kutoa maamuzi yaliyotolewa.

Binafsi naona hii sio NEWS yakupoteza muda wetu! Kuna mambo makubwa sana ya kujadili kwa mstakabali wa maendeleo ya nchi yetu.
 
...siamini kuwa majaji waliohusika na maamuzi hayo walishinikizwa ktk kutoa maamuzi yaliyotolewa.

Binafsi naona hii sio NEWS yakupoteza muda wetu! Kuna mambo makubwa sana ya kujadili kwa mstakabali wa maendeleo ya nchi yetu.

Dume La Mbegu, heshima mbele.

Hii ishu inaenda kwenye kiini cha vizingiti vikubwa vya huo mustakabali wa maendeleo unao uongelea.

Uozo wa utawala wa sheria, na watu kutokuwa sawa mbele ya haki pamoja na influence peddling ya wakubwa ni mbegu ya matatizo mengi ya nchi zetu kama ufisadi usio na mithili.

Kwa sababu hili la utawala wa sheria ni yai la matatizo ya maendeleo, unaweza kusema mijadala moto moto kama kutaka Mafisadi washitakiwe inawezekana ni ndio kupoteza muda zaidi kuliko kutaka jamii, na hasa majaji, waheshimu haki na usawa wa watu mbele ya sheria. Wizi wa mchana mchana wa mahela ya wananchi, na baadae kukebehi uliowaibia, unashamiri pale ambapo watu hawaogopi sheria. Ndio maana mtu anajiamini kutamka kifidhuli kwamba dola milioni moja ni senti tu. Nani atamtisha?

Huo ndio mzizi wa fitina. Jamii za watu wenye utawala wa sheria hili la Binti Keenja lingekuwa dhoruba kubwa mno, kwa sababu linahusu Jaji wa Mahakama Kuu ya nchi kushawishi pembeni pembeni maamuzi ya hakimu, baada ya kukutana na mkubwa, Mbunge ambae ni baba wa mtuhumiwa, na mpaka hakimu akasusia kesi. Hili ni vunjo la nguzo ya msingi ya maadili ya maofisa wa sheria.

Wakili Chuwa na Jaji Kaijage wanaelewa vizuri sana travesty iliyotokea hapa. Na wanajua wamepeta kwa sababu hakuna atakae 'poteza muda' na mambo haya. Tuache kufuatilia 'mustakabali' na 'uhafidhina na 'ufisadi'? Haya ndio mavazi mapya mjini.
 

Kuhani Mkuu, nakubaliana sana na hoja hiyo (niliyoi-quote)!
 
Ahsante kwa kujitokeza AmaniK naamini kulikuwa na upotoshaji wa ukweli wa kesi hii.Naomba wape mwanga wale waliokuwa wanaopotosha ukweli.Kenny

Lesiriamu, Salaam.

Ukweli umeshaanza kuongelewa hapa. Naona kuna wengi wanojua mambo yanavyokwenda. Ila ninachoweza kusema ni kwamba, hakuna nguvu iliyotumika kuomba marudio ya kuondolewa kwa dhamana. Ilitumika busara na uaminifu zaidi. Nadhani wote mtakubaliana nami kuwa si tija kwa yeyote mtu anaponyimwa dhamana ana kuwekwa ndani bila kuwa hatari kwa jamii. Naomba tuachie wanaohusika kuishughulikia kesi hii, ili haki ya kweli ipatikane kwa wote kadri inavyowezekana.
 
Lesiriamu, Salaam.
... ninachoweza kusema ni kwamba, hakuna nguvu iliyotumika kuomba marudio ya kuondolewa kwa dhamana. Ilitumika busara na uaminifu zaidi.

Unajuaje? Sitakiwi kumwamini hata Rais wangu, kwa nini nikuamini wewe? Ili kuondoa mimi kukuamini wewe na wewe kuniamini mimi ndio ukatengenezwa utaratibu kwamba Jaji akutane na mtuhimiwa na mwakilishi wake kwenye mahakama ya wazi sio na Baba ndani Ofisi. Ili mimi na wewe tuone na tusikie Jaji kamwambia nini mtuhumiwa, na kampa au kamnyima dhamana kwa nini. Na Jaji anacho mwagiza hakimu kiwe kwenye rekodi, sio kwenye faragha za simu. Ili kesho na kesho kutwa mtoto wa Chumvi na Nyonzo, na mtoto Yatima wakija kuomba dhamana kwa kigezo hicho hicho cha kufiwa nao wapewe. Ni haki msingi. Jaji Kaijage analijua vizuri hili. Anaiita Stare Decisis.
Nadhani wote mtakubaliana nami kuwa si tija kwa yeyote mtu anaponyimwa dhamana ana kuwekwa ndani bila kuwa hatari kwa jamii.
Ndio. Ni kweli kabisa.
Naomba tuachie wanaohusika kuishughulikia kesi hii, ili haki ya kweli ipatikane kwa wote kadri inavyowezekana.

Nooooooooh! That is treason! Abdication of your public duty to watch the government is as bad as espionage! Do not pick sides here, pick the country. Look at the mockery of justice that happened here!
 
Nooooooooh! That is treason! Abdication of your public duty to watch the government is as bad as espionage! Do not pick sides here, pick the country. Look at the mockery of justice that happened here!

Heshima mbele, Kuhani Mkuu
Sijui comment hii imetokana na nini? Naona haijibu comment iliyotolewa mwanzo na mchangiaji.

Naomba mwongozo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…