Dume la Mbegu
Member
- Apr 16, 2008
- 31
- 1
Cha maana pasi yake ya kusafiria imeshawekwa kapuni..sasa sheria ifuate mkondo wake..na kibaya zaidi vyombo vya habari vishajua kuwa kuna kaharufu ka mchezo mchafu..stay tuned
It is a pity Mjadala huu sikuuona on time!
Inawezekana wachangiaji tukawa hatuwatendei haki watanzania wenzetu kwa kutokufahamu! Kwanza ikumbukwe kuwa huyu mtoto wa Keenja ameshitakiwa akiwa anatekeleza wajibu wake kwa mwajiri wake, National Housing Cooperation (NHC)! Kimsingi angetakiwa alindwe na ajira yake kwa vile walimuondoa mpangaji wa NHC akiwa kazini. Mchina aliondolewa kwenye nyumba ya NHC baada ya kukiuka taratibu za upangaji. Aliondolewa kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kuhusisha ofisi ya serikali za mitaa na kumpa taarifa ya kimaandishi. Yeye (mchina) aliandaa orodha kubwa ya vitu alivyodai kupotea kutokana na zoezi hilo ambayo ilikuwa tofauti kabisa na ile iliyosimamiwa na NHC, Dalali na ofisi ya serikali ya mitaa! Aidha Dalali ndiye aliyehusika moja kwa moja ktk kufunga milango.
Mchina alifungua kesi ya madai dhidi ya NHC na dalali. Katika hali inayoweza kuchukuliwa kama ni lengo la kuwakomoa watendaji waliohusika, alifungua kesi ya wizi dhidi ya mfanyakazi wa NHC (ambaye ni Eliaisa Keenja) na dalali wa NHC kama individuals.
Mimi sio mwanasheria lakini nimeifuatilia kesi hii kwa ukaribu sana na kushangazwa na taswira inayojengwa dhidi ya watu wasio na hatia. Waandishi wa habari walioko JF watanisamehe lakini Mchina amekuwa akiwapa waandishi "her side of story" na wao kukimbilia kuandika magazetini bila ya kujali athari zake.
Hebu tujenge picha kuwa wewe katika kutimiza majukumu yako ya kawaida ukafunguliwa mashtaka ya kuiba mamilioni ya shilingi na kuwekwa rumande (by the way Eliaisa alishalala rumande siku za njuma ktk mashtaka haya haya!), ufiwe na mume wako halafu hapohapo uwekwe ndani! kama hiyo haitoshi unahukumiwa na umma kupitia magazeti na mtandao kama mwizi!
Siyaandiki haya kwa vile Eliaisa ni rafiki yangu bali ni sehemu ya habari ambayo hatuisikii. Tunachokisikia ndicho kinachotufanya tuyaseme tunayoyasema humu!
Vyombo vya habari vingeweza kufanya kazi nzuri zaidi hata kama MCHINA ni mshikaji wao!