KERO Kelele usiku kucha Mbweni Mpiji-Ungindoni sababu ya vigodoro na pub tumezichoka, tumeripoti serikali za mtaa lakini kazi bure

KERO Kelele usiku kucha Mbweni Mpiji-Ungindoni sababu ya vigodoro na pub tumezichoka, tumeripoti serikali za mtaa lakini kazi bure

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mbweni ushuwani hakuna mambo haya...
Ukitaka kujenga au kufanya makazi inataka uangalifu sana

Ova
Na kweli
Ila mkuu kwanini suala la kelele hawalitilii maanani sana serikalini? Imekuwa kawaida sana

Ila umenifundisha kitu
 
Nakuuliza kama nilivyomuuliza Mkuu mwingine, kuna watu wana ruhusa ya kupiga kelele usiku kucha kwenye makazi ya watu? Pub inakesha usiku kucha kwamba nihame, kwanini? Dar karibu yote wazaramo na wanaofanana hawakosi kwahivyo wengine ambao hatuna tamaduni za kukesha tuondoke, kuwa serious Mkuu
Huwez kuja mgeni ukabadili mtindo wa watu kuishi kwasababu huupendi. Ndio maana manzese huko wazaramo ngoma kila siku na hakuna anaewagusa. Hiv kwa mfano ukiona pale kkoo watu wamefunga barabara wana sherehe yao utasema wanazuia watu kupita? Kuna maeneo serikali inakaa kimya sio kwasababu inakubaliana na watu ila kwasababu kuna kukubali kwa kutokukubaliana.
 
Njoo kiembeni huku mkuu mbele mbele kwa manyama unapita mbeeele huku
 
Wakuu

Huku Mbweni Mpiji maeneo ya Ungindoni wakiwa na sherehe zao za vigodoro ni kero kubwa, wanakesha usiku kucha na mziki ni mkubwa kiasi kwamba ni changamoto hata kupata usingizi. Mbali na hili ni hatari kwa watoto pia, ukienda kuchungulia mida ya saa tano sita usiku hukosi watoto, kwa watu wazima hamna tabu lakini hawa watoto wanakuwa exposed kwenye mambo ya ajabu sana, waliowahi kuona yanayofanyika huko wakati wa usiku wataelewa ninachosema.

Mbali na hilo, kuna pup ambayo ipo karibu na kanisa, jamani ni balaa, ni kero kwakweli. Kwenye pub wanasema wana kibali cha polisi kukesha. Polisi wanatoa vipi kibali cha watu kukesha kwenye makazi ya watu usiku kucha na hawana sound proof?

Nikaenda kupeleka malalamiko yangu katika ofisi ya serikali ya mtaa wakasema watalishughulikia lakini chochote walichofanya, weekend ni kama sikulala kwa makelele yale. Nadhani kuna rushwa inatolewa ili wafanye sherehe zao mpaka asubuhi, maana hatusikilizwi kabisa.

Soma Pia: Kelele usiku kucha Mtaa wa Alesika, Mbezi Beach kutoka Amigos Pub na Kanisa la Angels Ministry ni kero kubwa, tumechoka!

Sasa pata picha pub inapiga mziki, huku kigodoro kimechanganya, saa saba usiku kuna makelele utafikiri saa sabab mchana. NEMC mje mtupie jicho na huku na uongozi wa serikali ya mtaa uwajibike.
jisogeze mbweni teta mkuu uko mpiji ni changanyikeni hao wa swahili wata kuroga tu ukifanya move kuwashitaki.
 
Back
Top Bottom