Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Siku hizi kila muda ni maadili! maadili! lakini wengine hawajui kuwa wanapiga kelele tu zisizo na tija. hebu hizo juhudi za kujenga maadili mema changanyieni na hizi
1.Azam achieni ile chaneli ya ZBC2 iruke watu waangalie bure hata bila kulipia. kama nakosea mtanirekebisha lakini nijuavyo ile ni kama tbc ya upande wa pili sasa iweje tbc tuangalie halafu zbc2 mpaka kifurushi. mbaya zaidi ni kwamba kukiwa na mpira wanaiachia muangalie mpira lakini ukiisha wanakata fasta, ina maana mpira ndiyo unawafaa watu kuliko vipindi vya kimaadili?
2.Zuieni wasanii kufanya matamasha shuleni. wasanii na watu maarufu (mf waigizaji na watangazaji) wana tabia ya kwenda mashuleni halafu ukifuatilia hata kilichowapeleka hukielewi vizuri halafu wao ndiyo namba moja kwa kuporomosha maadili ya jamii kupitia vaa yao, ongea yao, imba yao, cheza yao, nk. afadhali yule jamaa wa skonga kidogo anaeleweka japo naye kuna baadhi ya mapungufu
3.Wapeni wananchi uhuru kamili katika imani zao. hii namaanisha kama mtu kazini akathibitika kwa vigezo vyote vinavyotakiwa basi acheni imamu aamuru yuule mtu apigwe bakora 100 zake msiingize huruma. sasa serikali yetu inasema kila mtu yupo huru ilimradi uhuru wake usivunje sheria za nchi ila wanasahau kuwa raha za mtu yeyote yule lazima zitakuwa zinaingilia raha za mtu mwingine yaani raha za huyu ni taabu kwa yule na hiyo ni nature huwezi kwepa. kwahiyo waumini wakimtenga mtu akaenda kushitaki serikalini isionekane mtumishi wa kanisa amefanya uonevu/ubaguzi mpaka kufikia serikali kupangua yale aliyoyaamuru kiongozi huyo bali
4.Chukueni maoni kwa viongozi wa dini kwa baadhi ya mambo ambayo ni pasua kichwa . msiwafanye wao kazi yao ni kuwafungulia kwa dua tu mikusanyiko yenu
5.Na nyinyi viongozi wa dini nanyi toeni hoja/suluhisho kwa mujibu wa dini zenu juu ya maswala muhimu mbalimbali ili serikali ione kama yafaa kuingiza hoja zenu katika mambo yake na zikafaa. dini ni mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu maana yake kila linalohitajia ufumbuzi linapatiwa (yaani kila linaloonekana kutatiza basi solution yake ipo kwenye mfumo huo wa maisha ambao mtu ameshikamana nao)
Kuna maswala mengi tu unakuta serikali na vyombo vyakke inahangaika kupata solution wakati wangeshirikisha watu wa dini ni mambo madogo tu. kwa mfano nenda mahakamani makesi ya mirathi, ubakaji, wizi, nk yamejaa kibao. mambo kama hayo ya malezi na maadili, unakuta kiongozi wa dini yeye kaitwa kwenye kongamano eti akafungue tu kwa dua basi hallafu wanaojadili maswala hayo ni vijana tu ambao hawajaoa hata kuoa, mapungufu kibao!
6.Msiwaalike wakata viuno kwenye mikusanyiko ya viongozi (najua hili ni gumu sana)
7.Fanyeni allocation kwa uwiano wa watumishi kati ya ke na me katika sehemu hizi; mashuleni, hospitalini, polisi, nk
8. Tukirudi hoja namba 3 najua ni ngumu kwa baadhi ya mambo lakini basi mambo madogo madogo acheni yaamriwe kwenye dini na mila za watu wenyewe. nyinyi serikali mbaki na yale makubwa tu ambayo huko kwenye mamlaka za kimila maamuzi yake ni makubwa na magumu kutekelezeka kwa nchi yetu
9.Wapeni nafasi watoto ya kujifunza mila na dini zao. siyo kweli kwamba vyote atafundishwa shuleni, kuna vingine itabidi akafundishwe nje na skuli. pigeni marufuku watu wa elimu ambao wanang'ang'ania walimu wakae na watoto muda wote wa mwanga wa jua kasoro siku moja tu katika wiki
10.Masomo ya dini yasiwe ya option wala yasiachwe tu kama sasa ambapo mtu akisoma faida ipo kwenye dini yake tu lakini serikalini hayatambuliki