Meshe
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 386
- 479
Naziomba mamlaka ziliangalie na kulitafutia ufumbuzi suala la uchafuzi wa mazingira kwa makelele. Uchafuzi huu wa ajabu kabisa unaolelewa ni kero kubwa kwa raia na unaathiti sana utulivu wa moyo na akili.
Pengine mahospitalini tunatibiwa magonjwa sugu yanayotokana na adha ya makelele haya.
Kelele hizi zinatokana na matumizi ya vipaza sauti vinavyotumika hovyo bila utaalam.
Maeneo husika ni pamoja na:-
1. Wahubiri walioenea mitaani hasa nyumba za ibada zilizojengwa mitaani kwenye makazi ya watu wanatumia vipaza sauti muda wote.
2. Wahubiri hawa wanaweka vipaza sauti mitaani na katika vituo vya mabasi bila kudhibitiwa. Mfano ni stendi ya daladala ya Mbezi Luis. Tena wengine wanakusanya hela kwa kutishia abiria kuwa wasipotoa sadaka watawaombea wapate mabalaa huko mjini waendako.
3. Vipaza sauti vya wafanyabiashara wadogowadogo zilizotundikwa kila Kona. Mfano wanaosajili line za simu, wauza dawabza mende na kunguni, wauza madawa ya kuongezea nguvu za kiume,n.k.
Naziomba mamlaka zinazohusika wakiwemo Halmashauri ya Ubungo, Mkuu wa Mkoa na NEMC waingilie kati suala hili na kulipatia ufumbuzi wa kudumu. Pia waangalie huu uingizaji holela wa maspika.makubwa ya kichina ambayo watumiaji wengi wana abuse.
Tunayo haki ya kuishi mazingira salama na ya utulivu.
Mpango wa kuwapanga wamachinga uhusishe pia udhibiti wa sauti za makelele zilizoenea mitaani.
Miji safi na tulivu kwa ustawi wa wakaazi na wageni!
U