Kelvin Kiptum ashika rekodi mpya ya dunia katika marathon huko Chicago (2:00:35). Kipchoge kwisha habari yake!

Kelvin Kiptum ashika rekodi mpya ya dunia katika marathon huko Chicago (2:00:35). Kipchoge kwisha habari yake!

Leo jumapili October 8, tumemuona KELVIN KIPTUM akivunja record ya dunia ya Marathon hapo Chicago nchini Marekani kwa muda wa saa 2 na sekunde 35, akiizidi record ya KIPCHOGE aliyoweka Berlin Marathon(saa 2:01:09)...Hivyo bingwa mpya wa marathon ni KELVIN KIPTUM..
Duh maana yake anaweza kimbia dar mnazi mmoja to msavu morogoro kwa masaa 9 kasoro tu.

Sasa hilo si gari kabisa hawa watu wanakimbia isee
 
Eliud Kipchoge 2019 amkimbia marathon kwa muda wa 1hr 59min.
 
Eliud Kipchoge 2019 amkimbia marathon kwa muda wa 1hr 59min.
Hiyo ni UNOFFICIAL ilikua ni project ya NIKE breaking two...ilikua na vitu ambavyo haviruhusiwi... kama pace makers walikaa MONZA FORMATION umbo kama la pembe tatu hivi ili wamkingie upepo, pia walifuata LASER BEAM za kijani zilikua projected kutoka kwenye gari lililokua mbele, pia alipewa maji na electrolytes na watu wa baiskeli badala ya kuchukua mezani, pia kuna madawa alitumia(DOPPING) kama huamini angalia Berlin ya mwaka huu nini kilikua kinatoka puani kwake kwanzia km 35 sio kamasi angalia vizuri...
 
Hiyo ni UNOFFICIAL ilikua ni project ya NIKE breaking two...ilikua na vitu ambavyo haviruhusiwi... kama pace makers walikaa MONZA FORMATION umbo kama la pembe tatu hivi ili wamkingie upepo, pia walifuata LASER BEAM za kijani zilikua projected kutoka kwenye gari lililokua mbele, pia alipewa maji na electrolytes na watu wa baiskeli badala ya kuchukua mezani, pia kuna madawa alitumia(DOPPING) kama huamini angalia Berlin ya mwaka huu nini kilikua kinatoka puani kwake kwanzia km 35 sio kamasi angalia vizuri...
uongo mtupu
 
CREDIT: BBC

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon za wanaume, Mkenya Kelvin Kiptum, 24, amefariki dunia katika ajali ya barabarani nchini mwake.

Alifariki pamoja na kocha wake, Gervais Hakizimana wa Rwanda, kwenye gari kwenye barabara magharibi mwa Kenya siku ya Jumapili.

Kiptum aliandikisha mafanikio mnamo 2023 kama mpinzani wa mwenzake Eliud Kipchoge - mmoja wa wanariadha wakuu wa marathon.

Na ilikuwa Chicago Oktoba mwaka jana ambapo Kiptum aliboresha mafanikio ya Kipchoge,akimaliza umbali wa maili 26.1 (42km) kwa saa mbili na sekunde 35.

Wanariadha hao wawili walikuwa wametajwa katika timu ya Kenya ya marathon kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Paris baadaye mwaka huu.

Akitoa risala zake kwa Kiptum, Waziri wa Michezo wa Kenya Ababu Namwamba aliandika kwenye X: "Inasikitisha sana!! Kenya imepoteza vito maalum. Sina la kusema."

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya na waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga, alisema nchi hiyo imepoteza "shujaa wa kweli" na inaomboleza "mtu wa ajabu... na kinara wa riadha wa Kenya".

Sebastian Coe, rais wa Riadha Duniani, alisema Kiptum "ni mwanariadha wa ajabu aliyeacha historia ya ajabu, tutamkosa sana".

Ajali hiyo ya barabarani ilitokea mwendo wa saa 23:00 kwa saa za huko (20:00 GMT) siku ya Jumapili, polisi walinukuliwa wakisema na shirika la habari la AFP.

Wakitoa maelezo zaidi kuhusu ajali hiyo, polisi walisema Kiptum ndiye aliyekuwa dereva, na gari "lilipoteza mwelekeo na kubingiria na kuwaua wawili hao papo hapo".

Msemaji aliyenukuliwa na AFP aliongeza kuwa abiria wa tatu - ambaye alikuwa mwanamke - amejeruhiwa na "kukimbizwa hospitali".

Wiki iliyopita tu, timu yake ilitangaza kwamba angejaribu kukimbia umbali wa chini ya saa mbili katika mbio za marathon za Rotterdam - hatua ambayo haijawahi kuafikiwa katika mashindano ya wazi.

Ukuaji wa umaarufu wa baba huyo wa watoto wawili ulikuwa wa haraka - alikimbia marathon yake ya kwanza kamili mnamo 2022.

Alishiriki katika shindano lake kuu la kwanza miaka minne iliyopita akikimbia kwa viatu vya kuazima kwani hakuweza kumudu jozi yake mwenyewe.

Alikuwa miongoni mwa wanariadha wapya wa Kenya ambao walianza uchezaji wao ugenini, wakiachana na tamaduni ya zamani ya wanariadha kuanza kwenye mbio kabla ya kuhamia masafa marefu.

Kiptum aliiambia BBC mwaka jana kwamba chaguo lake lisilo la kawaida liliamuliwa tu na ukosefu wa rasilimali.

“Sikuwa na pesa za kusafiri kufuatilia vikao,” alieleza.

Kocha wake, Hakizimana, 36, alikuwa mwanariadha mstaafu wa Rwanda. Mwaka jana, alitumia miezi kadhaa kumsaidia Kiptum kulenga rekodi ya dunia.

Uhusiano wao kama kocha na mwanariadha ulianza mnamo 2018, lakini wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza wakati mshikilizi huyo wa rekodi ya ulimwengu alipokuwa mchanga zaidi.

"Nilimfahamu alipokuwa mvulana mdogo, akichunga mifugo bila viatu," Hakizimana alikumbuka mwaka jana. "Ilikuwa mwaka wa 2009, nilikuwa nikifanya mazoezi karibu na shamba la baba yake, alikuja kunipiga teke na nikamfukuza.

"Sasa, ninamshukuru kwa mafanikio yake.
 
MAY HIS SOUL REST IN PEACE...BABU KIPCHOGE KAACHIWA UWANJA SASA
 
Too Bad huyu dogo ametutoka kwa ajali!!... dahh. Very painful.... mimi naanza kuhisi ni fitna hizi
Dunia uwanja wa vita ..mtu anajiandaa kvnja rekod ya dunia, ghafla anapiga mzinga wa ajali..
 
Back
Top Bottom