Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Ndugu Kenani Kihongosi (Katibu Mkuu UVCCM) amuwakilisha Ndugu Daniel Chongolo (Katibu Mkuu CCM) Msiba wa Mke wa RC Morogoro, Mhe Martine Shigela.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Cde Kenani Kihongosi akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo; aungana na viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi kwenye mazishi ya mke wa Mhe Martin Shigela Mkuu wa Mkoa wa Morogoro marehemu Bi. Magdalena Layda Anney Shigela Mkoani Shinyanga
Viongozi waliohudhuria ni Pamoja na mawaziri, makatibu wakuu wa wizara, wakuu wa wilaya; wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mke wa Shigela alifariki dunia Alhamis tarehe 19 Januari, 2022 Dar Es Salaam na kupumzishwa nyumbani kwake mkoani Shinyanga 24- Januari 2022.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.