Kenchi ikikaa muda gani bila bati inaharibika

Kenchi ikikaa muda gani bila bati inaharibika

Hapana siyo kweli
Uiumia agent kuna probability ya kupata bati mapema sababu agent ana kuwa na order. Ya mzigo mkubwa sasa hawawezi jukuanza kukusaidia ww mwenye order ndogo lzm wana anza na mwenye order kubwa

Mimi nina ushahidi kabisa site kwangu kuna jumba moja likipigwa kenchi 3 weeks kabla boma langu sijapiga kenchi lkn sasa mm nikaenda kuweka order fundi wangu akanishauti tutumie agent huwezi amini boma langu nimeshalipiga bati hii ni wiki ya pili sasa lkn lile jumba kubwa mpaka leo hawajapata mzigo wao wana almost 2 month

Maanna Alaf kuamzia tareh 28 august walifanya stock take so walisitisha uzalishaji kwa siku kama 5 ivi acxording to yule agent so ilipo pinduka Sept tu wakaamza uzalishaji so wana order nyingi mnoo hata mie zile bati zangu zilifika site saa saba uaiku ..pale kiwandani kwao kulikuwa na foleni hatarii
 
Unakuwa sio muelewa, makadirio yanayofanyika kabla ya ujenzi ni ya size standard ya mabati. Mfano kama makadirio ni bati 70 maana yake ni bati 70 za meter 3. Ila hizi za kupima baada ya kupiga kenchi huwa zinapimwa bati za urefu tofauti pungufu au zaidi ya meter 3. Hivyo vipimo unapeleka alaf na bati zako zikija wewe ni kugonga tu hakuna hata kukata ili kupunguza urefu etc.
Kwani bati za kupima zina advantage gani? Hiyo square meter inapimwa sawasawa kwa urefu na upana? Maana naona bei yake ukilinganisha na bati zao ni kubwa mno . Lengo ni kujifunza
 
Kwani bati za kupima zina advantage gani? Hiyo square meter inapimwa sawasawa kwa urefu na upana? Maana naona bei yake ukilinganisha na bati zao ni kubwa mno . Lengo ni kujifunza
Urefu tu ndio unatofautiana. Upana wa mabati nisawa. Hii inapunguza adha ya kukata kata mabati, kupata mabati kiasi kile tu unachohitaji bila kuzidisha au kupungua, bei ya kiwandani etc
 
Mkuu

Sunshare mimi nilipaulia bati zao huko zamani. Dar. Baada ya miaka kama mitano hivi zilipauka na kupoteza rangi ya awali.

Labda kama wamejiboresha!
Hakuna bati isiyopauka! Take it from me, hata Alaf hawezi kukupa gerentii kuwa bati zake hazipauki. Kinachotofautisha ubora wa kampuni moja na nyingine ni time ya kupauka. Takribani bati kutoka kampuni yote lazima utaanza kuona dalili za kupauka baada ya mwaka wa kumi. Zipo kampuni zinazopauka mapema na nyingine zinachelewa lkn hatimaye zote zitapauka
 
Salama wanajamvi?

Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza. Wiki nne zilizopita Nilifunga mbao za kench ktk site yangu na kuoda bati alaf ila bati bado hazijatoka nimeambiwa nitegemee zitatoka ndani ya wiki tatu zijazo.

Na mvua za masika ndio naona zimeanza hapa Dar. Sasa naingia wasiwasi kama kenchi zinaweza kuharibika. Naombeni ushauri wadau kama kweli zinaharibika zikikaa sana na je nifanye nini kuzuia uharibifu.

Nyumba iko Dar na nimetumia mbao zenye dawa. Ila ni mbao za dawa ya kuchovya sio zile za kuchemsha

Wasalaam
ina tegemeana na aina ya mbao nyumba ya Mzee alitumia mbao za mniga mpaka Leo zipo vizur tokea mwaka 1974 na madirsha mbao ya mninga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ina tegemeana na aina ya mbao nyumba ya Mzee alitumia mbao za mniga mpaka Leo zipo vizur tokea mwaka 1974 na madirsha mbao ya mninga

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kwa mwaka 1974 huo mninga ulikuwepo kwa wingi...sasa hivi kupata mninga kwa ajili ma milango tu ni shida.na bei ni juu sana.
 
Back
Top Bottom