Kendrick Lamar & SZA- all the stars: Wasanii wetu mna nini cha kujifunza?

Kendrick Lamar & SZA- all the stars: Wasanii wetu mna nini cha kujifunza?

Wanasema huyu ni another 2Pac...lakini kipindi fulani tena walitaka kutukaririsha kuwa T.I was another 2pac...ohhh Mara Jay-Z ni another Frank White Big...Kendrick yuko vizuri na ameweza kukaa hapo muda mrefu.
Alinipa radha flan ktk nyimbo ya RED ya The Game
 
Malcom wasanii wetu naweza sema hawajui kuvaa uhalisia au wanatufanya tusione uhalisia wa kitu wanachofanya!.. Hebu cheki ile nyimbo ya Harmonize ile matatizo anataka tuone kapigika lakini anavaa fashion ya wakati huo!..Huyo ni mfano tu sasa uje ukutane na wasanii wanaact kama choka mbaya lakini kichwani wana dreadlocks wana nguo zipo vizuri!..
Unajua kuna watu wengine huwa tunaangalia na mandhari iliyotumika ili kurelate kama kinachoimbwa kinalingana!..
Ukimcheki Kendrick Lamar kwenye video zake huwa yupo soo simple lakini anazipa uniqueness flani hasa kama kwenye All the Light, Alright, Humble, DNA na ile nyimbo na drake!..
Sasa ukija kwetu unaona kabisa huyu mtu either ushamba au hajiamini, hebu mcheki Diamond kwenye ile nyimbo na Ne-yo pale anashuka gari, anashangaa demu kwenye traffic lights, anaingia ndani.
Labda mie pekee ndio naziona hizi scene za kujishtukia wasanii wetu!..
-wick
Tuanze na Harmonize! Mosi, inaonekana umechanganya madesa kati ya wimbo wa Matatizo na Niambie!

Kwenye Matatizo sioni ambacho hakina uhalisia! Storyline inaonesha hustle za jamaa akiwa street... mara anatembeza biashara mikononi; sometimes anabeba zege, kisha unamkuta yupo na mkokoteni!

Kwahiyo kama kukosa uhalisia labda kuoga na kuonekana ametakata huku akiwa amevaa nguo za kawaida kabisa lakini zimefuliwa na zipo safi!

Sidhani kama kuna uhusiano kati ya matatizo na uchafu! Hata wale Machinga tunaokutana nao barabarani ni Matatizo tu ndo yanawafanya watembee Mbagala hadi Mwenge but still ni Wasafi!

Tafuta video ya Matatizo iangalie!

Or probably ulitaka kuzungumzia wimbo wa Niambie ambao Harmonize anaongelea asivyo na kitu lakini video inaonesha maisha ya kifahari... nyumba ya kifahari, magari ya kifahari, michezo ya kishua (tennis)

Hata hivyo wakosoaji wa video wamejikita kwenye umaskini wa Harmonize badala ya kuangalia context ya wimbo mzima!

Harmonize ni maskin lakini anashangaa na umaskini wake ule kupendwa! Na ukisikiliza kwenye verse, Harmonize anamuuliza mwanamke ni kipi kilichomfanya ampende!

Video inaonesha maisha ya kifahari lakini haya maisha sio ya Harmonize bali ya yule mwanamke... kwa maana nyingine Harmonize analelewa!

Tukirudi kwenye Marry You ya Diamond + NE Yo! Man ume-miss sanaa iliyotumika kwenye ile video!

Storyline ni kwamba Diamond akiwa na Ne-Yo kwenye gari, wakapishana na wale Warembo pia wakiwa kwenye gari.

Matukio mengi yaliyofuata, kv kushuka kwenye gari akiwa na yule mtoto kisha wanaingia kwenye mansion, harusi n.k.... matukio yote yale sio real bali ni imagination! Yaani baada ya kumuona yule demu, Diamond akawa ana flashfoward ya vile ATAKAVYOKUWA na yule demu... wanatembea wameongozana, wanaingia kwenye mansion, swimming pool, harusi ya haja; n.k... zote zile ndoto za alinanacha kwa sababu demu kapishana nae barabarani na kenda zake!

Na ndio maana ukiiangalia vizuri, mwisho mwisho Ne-Yo anamgutua Diamond kutoka kwenye hizo ndoto!
 
Tuanze na Harmonize! Mosi, inaonekana umechanganya madesa kati ya wimbo wa Matatizo na Niambie!
Na ndio maana ukiiangalia vizuri, mwisho mwisho Ne-Yo anamgutua Diamond kutoka kwenye hizo ndoto!
Kifupi Hujaelewa content niliyoiongelea, rudia kuisoma!..
 
Kifupi Hujaelewa content niliyoiongelea, rudia kuisoma!..
Sijaelewa wapi?!
Umesema kwa mfano Harmonize na Matatizo yake anataka tumuone amepigika wakati anavaa fashion ya wakati huo...

Sasa hiyo fashion unayosema haiendani na uhalisia ni ipi? Ndo maana nikahoji labda issue iwe kuonekana msafi lakini video inaonesha hustles...


Kuhusu Diamond, umesema anaonekana anashuka kwenye gari anashangaa demu kwenye traffic kisha anaingia ndani!

Hapa nasisitiza... hakuna scenes za namna hiyo! Scene zinaonesha wanapishana na scenes ulizoona anaingia kwenye nyumba ni imagination/flash-forward scenes!

Sasa ni kipi ambacho sijaelewa?! Inawezekana ukawa na hoja lakini mifano uliyotoa sio sahii! Nyimbo zote mbili full uhalisia na yale maisha ya kifahari uliyoona kwenye Marry You sio real but just imagination!
 
Jana nlishangaa kuna watu wanamfananisha Kendrick Lamar na vitu vya kijinga....
 
Huyu jamaa kiukwel mwache achukue grammys tuu,daah,ujue nilikua sjaona hii video,wala kuskia huu mwimbo,kwel Tz ya sasa si ile,mi si wakutokuona hii video kwakwel.daah,

Vyuma achia kidogo bas
 
Huyu jamaa kiukwel mwache achukue grammys tuu,daah,ujue nilikua sjaona hii video,wala kuskia huu mwimbo,kwel Tz ya sasa si ile,mi si wakutokuona hii video kwakwel.daah,

Vyuma achia kidogo bas
Hahahahahahahahaha!
 
Hii video ilivyotengenezwa imeniacha mdomo wazi na wala sichoki kuiangalia,
Wanasema kuna vitu ameiba lakini niseme tu kwamba ubunifu uliotumika hapa ni wa kiwango cha hali ya juu sanaa. Ameitengenezea katika mazingira ya Kiafrika na bado umebamba sana: Hasashasa ukiongezea kile alichoimba na beat iliyotumika ndiyo hatari kabisaa.


NB: Hakika wasanii wetu wana kitu cha kujifunza hapa,
Siyo lazima kila video iwe na Lamborghini, Ferrari, Chevy Impala, Majumba ya kifahari au ifanyiwe nje ya nchi ili iwe nzuri. Japo naomba nieleweke kwamba sisemi kufanya hivi ni vibaya kabisa, lakini mara nyingine tunahitaji kujaribu vitu vya kitofauti ambavyo vitafanya muziki wetu uwe wa kipekee. Magari ya kifahari na majumba wasanii karibia dunia nzima ndiyo wanayatumia, sasa ni wakati tufanye kama Wahindi na nyimbo zao ambazo zinawapa Utofauti sanaaa na watu wengine.

CC: Red Giant , Benny , wick, travis 1

Naunga mkono hoja, huu ni bonge la wimbo sema K kaharibu sehem mmoja tu. Kaimba beti moja tu hafu huyu dada kaimba pakubwa
 
Wenzetu wanajipanga,wanajiamini,wanajua kwenda na wakati,na huyu Kendrick si wa nchi hii
 
Waafrika wabaguzi sana ila tunawasingizia wazungu wanatubagua, Mara watengeneze muvi ya mablack tupu Mara waunde TV ya mablack tupu 'bet', miafrika ni mibaguzi sana


Inawezekana hujui unachoongea kuhusu huu ubaguzi.5
 
Back
Top Bottom