Malcom wasanii wetu naweza sema hawajui kuvaa uhalisia au wanatufanya tusione uhalisia wa kitu wanachofanya!.. Hebu cheki ile nyimbo ya Harmonize ile matatizo anataka tuone kapigika lakini anavaa fashion ya wakati huo!..Huyo ni mfano tu sasa uje ukutane na wasanii wanaact kama choka mbaya lakini kichwani wana dreadlocks wana nguo zipo vizuri!..
Unajua kuna watu wengine huwa tunaangalia na mandhari iliyotumika ili kurelate kama kinachoimbwa kinalingana!..
Ukimcheki Kendrick Lamar kwenye video zake huwa yupo soo simple lakini anazipa uniqueness flani hasa kama kwenye All the Light, Alright, Humble, DNA na ile nyimbo na drake!..
Sasa ukija kwetu unaona kabisa huyu mtu either ushamba au hajiamini, hebu mcheki Diamond kwenye ile nyimbo na Ne-yo pale anashuka gari, anashangaa demu kwenye traffic lights, anaingia ndani.
Labda mie pekee ndio naziona hizi scene za kujishtukia wasanii wetu!..
-wick
Tuanze na Harmonize! Mosi, inaonekana umechanganya madesa kati ya wimbo wa Matatizo na Niambie!
Kwenye Matatizo sioni ambacho hakina uhalisia! Storyline inaonesha hustle za jamaa akiwa street... mara anatembeza biashara mikononi; sometimes anabeba zege, kisha unamkuta yupo na mkokoteni!
Kwahiyo kama kukosa uhalisia labda kuoga na kuonekana ametakata huku akiwa amevaa nguo za kawaida kabisa lakini zimefuliwa na zipo safi!
Sidhani kama kuna uhusiano kati ya matatizo na uchafu! Hata wale Machinga tunaokutana nao barabarani ni Matatizo tu ndo yanawafanya watembee Mbagala hadi Mwenge but still ni Wasafi!
Tafuta video ya Matatizo iangalie!
Or probably ulitaka kuzungumzia wimbo wa Niambie ambao Harmonize anaongelea asivyo na kitu lakini video inaonesha maisha ya kifahari... nyumba ya kifahari, magari ya kifahari, michezo ya kishua (tennis)
Hata hivyo wakosoaji wa video wamejikita kwenye umaskini wa Harmonize badala ya kuangalia context ya wimbo mzima!
Harmonize ni maskin lakini anashangaa na umaskini wake ule kupendwa! Na ukisikiliza kwenye verse, Harmonize anamuuliza mwanamke ni kipi kilichomfanya ampende!
Video inaonesha maisha ya kifahari lakini haya maisha sio ya Harmonize bali ya yule mwanamke... kwa maana nyingine Harmonize analelewa!
Tukirudi kwenye Marry You ya Diamond + NE Yo! Man ume-miss sanaa iliyotumika kwenye ile video!
Storyline ni kwamba Diamond akiwa na Ne-Yo kwenye gari, wakapishana na wale Warembo pia wakiwa kwenye gari.
Matukio mengi yaliyofuata, kv kushuka kwenye gari akiwa na yule mtoto kisha wanaingia kwenye mansion, harusi n.k.... matukio yote yale sio real bali ni imagination! Yaani baada ya kumuona yule demu, Diamond akawa ana flashfoward ya vile ATAKAVYOKUWA na yule demu... wanatembea wameongozana, wanaingia kwenye mansion, swimming pool, harusi ya haja; n.k... zote zile ndoto za alinanacha kwa sababu demu kapishana nae barabarani na kenda zake!
Na ndio maana ukiiangalia vizuri, mwisho mwisho Ne-Yo anamgutua Diamond kutoka kwenye hizo ndoto!