Kengold na Pamba zimepanda ligi kuu, Mbeya kwanza na Biashara kucheza playoff na vibonde wa ligi kuu

Kengold na Pamba zimepanda ligi kuu, Mbeya kwanza na Biashara kucheza playoff na vibonde wa ligi kuu

Kwa mtazamo wangu timu nayoona inaenda kuleta ushindani ni Pamba Fc tu, wanaujua uchungu wa kuwa nje ya ligi miaka 23,

Kengold wageni wa ligi wakileta mbwembwe kama Tabora united wanashuka tena
Kwani unadjani wachezaji wake ni walewale katika hiyo miaka 23? Hata viongozi ni tofauti.
 
Hazina ushindani wala hakuna iliyowahi kubeba ubingwa ligi kuu

Ni kawaida Mwanza kukaa miaka bila kuwa na timu ligi kuu

Mbeya hapo majuzi tu misimu ya 2021 na 2022 wameingiza timu nne
Kipindi pamba inabeba ubingwa ulikuwa unachezea kamasi!?
 
Kwani tatizo lipo wapi,

Timu dhaifu za ligi kuu zikiona zina uwezo kuzidi za championship wamepewa nafasi ya kujitetea kwenye playoffs.
Ndio jibu ambalo hutolewa Kila mara kujibu maoni kama hayo
 
Tatizo la Pamba lilikuwa Pesa..., baada ya ufadhili wa Bodi ya Pamba kutokuwepo tena..., Hivyo kwa sasa sababu wanapata pesa kutoka Jiji kama watachukua wachezaji kutoka Kanda ya ziwa (upcoming) basi kubaki kwenye ligi kuu ni rahisi..., Kuna kipindi Pamba ilikuwa ni mojawapo ya Timu ya kuleta Talent.....

Raphael Paul, George Masatu, Hussein Aman Masha, Nico Bambaga, Fumo Felician, Nteze John (to name just few)
 
Mi nadhani wa ligi kuu wacheze wenyewe atayefungwa ashuke .. na WA championship wacheze wenyewe atayeshinda apande..... Hii kuwapambanisha wa ligi kuu na championship sio sawa.
Tff sijui wanawaza nn
 
Mi nadhani wa ligi kuu wacheze wenyewe atayefungwa ashuke .. na WA championship wacheze wenyewe atayeshinda apande..... Hii kuwapambanisha wa ligi kuu na championship sio sawa.
Inaongeza amsha amsha ya timu za championship to have something to play for mpaka siku ya mwisho..., bila hivyo mtu akishaona hizo nafasi mbili ameshindwa ataanza tu kuuza mechi...

By the way kama unashindwa kuwafunga vibonde wa ligi kuu ambao wanashuka wewe ni kwamba hautaweza kumihili misuko suko ya huko bora hao vibonde hata wana uzoefu...
 
Hakuna ushindani mwanza wanapigana fitna za hovyo sana kwenye soka utaona wanatumia walikokuwa na wanapotea mazima
Sa Pamba inapoteaje mazima ndugu? Kwa sisi tunaoijua Pamba nadhani baada ya Simba na Yanga ndo timu inayofuatia Kwa kuwa na mashabiki wengi Tanzania.

Kwani unadjani wachezaji wake ni walewale katika hiyo miaka 23? Hata viongozi ni tofauti.
 
Hauko sahihi Pamba huwa ni Simba, Toto Africans ndio Yanga.
Hazina maisha hizo zinakwenda kusajili masalia ya yanga na kocha anakua minziro au fredy mbuna unategemea nini sio kurudi daraja la kwanza na point 12!
 
Kwan kanda ya kaskazin Arusha tumelaaniwa na mosh au shida nini mikoa
Hii miaka nenda rud hakuna team kabisa
Wachaga/wapare na mpira wapi na wapi? Yaani awe uwanjani anaumia kwa jasho halafu mtu mwingine yupo getini anakusanya hela? Mtu unaweza ku-concentrate uwanjani kweli?
 
Kengold kutoka Mbeya imetwaa Ubingwa wa Championship

Hatimaye baada ya miaka 23 timu ya Pamba Jiji FC ya Mwanza imefanikiwa kupanda ligi kuu

Bishara United Mara na Mbeya Kwanza watasubiri Playoff Kujaribu bahati yao

  1. KenGold FC
  2. Pamba FC
  3. Mbeya Kwanza FC
  4. Biashara United FC
  5. TMA FC
  6. Mbeya City FC
  7. Mbuni FC
  8. Polisi Tanzania FC
  9. Cosmopolitan FC
  10. FGA Talents FC
  11. Stand United FC
  12. Green Warriors FC
  13. Transit Camp FC
  14. Copco FC
  15. Pan Africans FC
  16. Ruvu Shooting FC
Tumkumbuke Amos Makala kwa Pamba kupanda Daraja hii ameacha legacy ninadhani na hili la ujenzi wa miundo mbinu uwanja wa ndege litawezekana.Hongera uliko mpambanaji
 
Pamba bingwa wa ligi kuu 1990
Pamba haikuwa kuchukua ligi ila ilikuwa ndio timu bora na consistent ukitoa simba na yanga..., Yanga alikuwa lazima apoteze kwa Pamba na Pamba ndio ilikuwa academy ya kutoa vipaji vingi ambavyo vilikuwa inaelekea Simba....
 
Hazina maisha hizo zinakwenda kusajili masalia ya yanga na kocha anakua minziro au fredy mbuna unategemea nini sio kurudi daraja la kwanza na point 12!
Pamba wacheze mpira waachane na usimba na yanga.
 
Back
Top Bottom