Kengold wangekamia SBS, KMC au Kagera Sugar kama walivyomkamia Yanga wangevuna walau alama moja

MwananchiOG

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
1,970
Reaction score
4,037
GYU35S-bQAEFnvP.jpeg
Hizi timu za Ligi kuu zinasikitisha sana, kumfunga Yanga au kutoa sare haikufanyi upate alama tatu muhimu! Bali nguvu mbinu na mikakati mnayowekeza kukabiliana na Yanga mngewekeza kwenye vilabu vingine hakika mngevuna alama nyingi Sifahamu huwa wanafundishwa nini huko kambini, Ila laiti kama hivi vilabu vingine vidogo vingekuwa vinacheza michezo mingine kama jinsi inavyocheza na Yanga, hakika wangevuna alama za kutosha!

Kwa upande wa pili Yanga imeshajulikana ndiye bingwa inafahamika ni timu tishio hali inayopelekea vilabu vingine vidogo kama KMC, Simba, Azam n.k kuikakia mno! Hivyo angalizo kwa Yanga wanapaswa kuja na mkakati mbadala kukabiliana na hali hii.

PIA SOMA
- FT: Ken Gold 0-1 Yanga | NBC Premier League | Sokoine Stadium | 25.09.2024
 
Mnaendelea kutoa milio wazee wa machakani. Unasajili washambuiaji wote wale na viungo halafu unaishia kupata ushindi wa kagoli kamoja dhidi ya timu inayoshika mkia kalikofungwa na beki.

Ubaya Ubwelaaa....
Wanataka wasikamiwe kwani wako kwenye ligi ipi
 
Mnaendelea kutoa milio wazee wa machakani. Unasajili washambuiaji wote wale na viungo halafu unaishia kupata ushindi wa kagoli kamoja dhidi ya timu inayoshika mkia kalikofungwa na beki.

Ubaya Ubwelaaa....
Wewe huujui Mpira R.madrid bigwa wa Dunia ni hivi juzi tu kadraw na kitumu cha mkiani mwenye ligi ya laliga akina mbappe,Bellingham,Vini Jr wote walikuwepo ila Ngoma ililala.
 
Peleka huo Ubaya ubwege shirikisho😀
 
Wewe huujui Mpira R.madrid bigwa wa Dunia ni hivi juzi tu kadraw na kitumu cha mkiani mwenye ligi ya laliga akina mbappe,Bellingham,Vini Jr wote walikuwepo ila Ngoma ililala.
Si mnajitoaga ufahamu, leo ndiyo mnajua hilo wazee wa "no shot on target"?
 
Kuikamia Yanga nayo ni mkakati,ulitaka wajilegeze wapigwe tu? Kwani yanga haipo kwenye ligi,hii kauli kwamba timu inakamiwa ni upuuzi,kama hutaki kukamiwa si usiingie uwanjani tu
Sasa huo mkamio ulikuwa wapi wakati wanacheza na Singida?
 
Wewe huujui Mpira R.madrid bigwa wa Dunia ni hivi juzi tu kadraw na kitumu cha mkiani mwenye ligi ya laliga akina mbappe,Bellingham,Vini Jr wote walikuwepo ila Ngoma ililala.
Ndiyo ujinga wenyewe wa hivyo vitimu vidogo
 
Kuikamia Yanga nayo ni mkakati,ulitaka wajilegeze wapigwe tu? Kwani yanga haipo kwenye ligi,hii kauli kwamba timu inakamiwa ni upuuzi,kama hutaki kukamiwa si usiingie uwanjani tu
Hii nayo ni point
 
Madogo wanajitahidi, kama ukicheki mechi yao na Kmc utakubaliana nami.
Huenda mbinu za kocha zinawaangusha.

Hivi vipigo mfululu vinawatoa nje ya reli, wajitahidi mechi ijayo walau wavune alama tatu.
 
Hizi timu za Ligi kuu zinasikitisha sana, kumfunga Yanga au kutoa sare haikufanyi upate alama tatu muhimu! Bali nguvu mbinu na mikakati mnayowekeza kukabiliana na Yanga mngewekeza kwenye vilabu vingine hakika mngevuna alama nyingi Sifahamu huwa wanafundishwa nini huko kambini, Ila laiti kama hivi vilabu vingine vidogo vingekuwa vinacheza michezo mingine kama jinsi inavyocheza na Yanga, hakika wangevuna alama za kutosha!

Kwa upande wa pili Yanga imeshajulikana ndiye bingwa inafahamika ni timu tishio hali inayopelekea vilabu vingine vidogo kama KMC, Simba, Azam n.k kuikakia mno! Hivyo angalizo kwa Yanga wanapaswa kuja na mkakati mbadala kukabiliana na hali hii.

PIA SOMA
- FT: Ken Gold 0-1 Yanga | NBC Premier League | Sokoine Stadium | 25.09.2024
Wala sikuona kama walikamia. Siyo kweli.
 
Back
Top Bottom