Kenichi Shinoda: Mfalme wa Yakuza, uongozi na uhusiano na serikali ya Japan

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Katika historia ya uhalifu wa kisasa nchini Japani, jina la Kenichi Shinoda linatajwa kwa heshima ya kutisha na hofu isiyoelezeka. Huyu ndiyo kiongozi mkuu wa kundi kubwa la kihalifu la Yamaguchi-gumi ambalo ni mojawapo ya makundi makubwa zaidi ya Yakuza duniani. Maisha ya Shinoda yamejaa utata, nguvu kubwa sana ya uongozi wake, na siri nzito kuhusu uhusiano wake na baadhi ya viongozi wa serikali ya Japani.

Kenichi Shinoda, anayejulikana pia kwa jina la Shinobu Tsukasa, alizaliwa mwaka 1942 katika mji wa Ōita, kwenye kisiwa cha Kyushu ndani ya taifa la Japai. Alikulia na kuishi katika mazingira ya umaskini, lakini kutokana na nia na dhamira yake ya kutafuta maisha bora, alijiunga na dunia ya Yakuza mapema katika ujana wake.

Na kama vijana wengine Kenichi Shinoda alipitia utamaduni wa kawaida kwa kuingia Misu-gumi ama kwa lugha ya Kijapani wakisema Tekiya, yaani kipindi cha majaribio kwa vijana, ila pia kukiwa na suala la Sakazuki likiwa ni tambiko la kukaribisha vijana ndani ya familia wakiwa na cheo cha Kobun, na hupewa jina code name, majina kama Hebi, Tora, Katana, Tetsu, Kaji, Shunju, na Kobe huku wale vijana wanaotoka familia zenye ushawishi mkubwa wakipewa majina yenye hadhi kama Waka, Khai ama Koji.

Kenichi Shinoda alianza ngazi za chini kama wengine akiwa kama Kobun, baadaye kwenda Shatei kisha kupata nafasi ya kuwasimamia Yakuza ngazi za chini akiwa kama Shateigashira na kwenda kuwa Wakagashira-hosa na kupewa mafunzo ya kujiandaa kushika nafasi ya Wakagashira, na mwaka 2005 rasmi alichukua uongozi wa Yamaguchi-gumi kama Kumicho (bosi mkuu), akawa mtu wa kwanza kutoka nje ya mji wa Kobe kuongoza kundi hilo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1915.

Yaani katika Kumicho sita, ni Kumicho mmoja tu ndio mzaliwa wa Kyushu, akipokea madaraka kutoka kwa Yoshinori Watanabe,
Yamaguchi-gumi ni kundi la kihalifu lililoanzishwa na Harukichi Yamaguchi, likiwa na historia ya zaidi ya miaka 100.

Linaaminika kuwa na wanachama zaidi ya 12,000 hadi kufikia miaka ya 2020, likihusika katika shughuli mbalimbali za uhalifu kama biashara ya dawa za kulevya, wizi wa fedha, utapeli, kamari haramu, biashara ya silaha, na hata biashara ya binadamu. Ingawa baadhi ya wanachama wake wanajitambulisha kama “wasimamizi wa amani,”.

Yamaguchi-gumi ni kundi ambalo kwa miaka mingi limekuwa likitekeleza vitendo vya kikatili kwa kutumia mbinu za kisasa na za asili. Ni kitu rahisi sana kukuta silaha kama Tanto, Katana, ama bastola aina ya SIG Sauer ama Glock ndani ya magari ya vijana wa Yamaguchi-gumi.

Katika uongozi wake, Kenichi Shinoda alileta mabadiliko makubwa katika mikakati ya Yamaguchi-gumi. Alifahamika kwa kuwa na akili ya kijasusi na nidhamu kali, akihimiza wanachama wake kufuata kanuni za heshima na hofu. Alipanua shughuli za kundi hilo kutoka eneo la Kansai hadi maeneo mengine ya Japani, na hata kuvuka mipaka hadi nchi kama Marekani, China, na baadhi ya nchi za Ulaya kwa njia ya uhalifu wa kimataifa.

Kinachoshangaza watu zaidi ni madai kuwa baadhi ya viongozi wa serikali ya Japani wamekuwa wakitumia ushawishi wa Yamaguchi-gumi kwa faida zao binafsi.

Kwa mujibu wa ripoti ya jarida la The Diplomat la mwaka 2012, baadhi ya wanasiasa mashuhuri wamewahi kuhusishwa kwa njia zisizo za moja kwa moja na Yamaguchi-gumi, wakiwemo kwa kupokea msaada wa kifedha au kutumia wanachama wa kundi hilo kwa kufanikisha ajenda zao za kisiasa.

Mwaka 1992 Shirika la Habari la NHK lilitoa ripoti yao ambayo ilibaini uwepo wa “mtandao wa kimyakimya” baina ya baadhi ya wabunge na makundi ya Yakuza, jambo lililozua taharuki ya kitaifa.

Katika kitabu cha Tokyo Vice kilichoandikwa na Jake Adelstein — mwandishi wa kwanza wa Magharibi kufanya kazi katika gazeti la kihabari la polisi nchini Japani — anaeleza jinsi Shinoda alivyoweza kudhibiti taarifa na kupenyeza watu wake hadi kwenye taasisi za sheria kama Mahakama, polisi, na hata vyombo vya habari. Adelstein aliandika kuwa

“Shinoda hakuwa tu jambazi wa kawaida, bali alikuwa na akili ya kisiasa inayoweza kufananisha na viongozi wa kitaifa, ni mtu ambaye ana watu ndani ya kila sekta Japani.”

Ushahidi wa kuonesha nguvu za Shinoda ulidhihirika mwaka 2005 wakati alipokamatwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria. Ingawa alihukumiwa kifungo cha miaka sita, bado aliendelea kuendesha shughuli za Yamaguchi-gumi akiwa gerezani kama kawaida ndani ya vyumba vya gereza la Fuchu.

Aliweza hivyo kwa kuwatumia wawakilishi wake waliokuwa huru pamoja na maafisa wa magereza tena wale High Officials, hii inatosha kuonesha nguvu yake ya utawala. Mwaka 2011 aliachiwa huru kwa msamaha wa mapema, na kurudi moja kwa moja kwenye uongozi wa kundi hilo.

Yamaguchi-gumi ilikuwa salama na imara kwa sababu kuu moja, muundo wake ulikuwa ni imara sana, wasaidizi wa Oyabuni wale viongozi kama Wakagashira, Wakagashira-Hosa, Shateigashira, Shatei pamoja na Kobun walimsaidia sana Shinoda kuendesha shughuli zote pasipo tatizo.

Katika makala ya Shirika la Reuters ya mwaka 2015, waandishi walieleza namna Shinoda alivyoendesha kundi hilo kwa mkono wa chuma lakini kwa werevu, maarifa na ustadi mkubwa. Alikuwa na tabia ya kutoonekana hadharani kabsa, kutumia ujumbe kwa ishara za vidole na mdomo pamoja na kuzungumza na waandishi wake binafsi, na alizingatia maadili ya Kijapani ya ukimya na nidhamu hata katika uhalifu wake.

Serikali ya Japani imekuwa ikipambana na Yakuza kwa miaka mingi kwa kuweka sheria kali za kupunguza ushawishi wao, zikiwemo Sheria ya Kudhibiti Makundi ya Uhalifu maarufu kama Bōryokudan iliyopitishwa mwaka 1991.

Hata hivyo, Yamaguchi-gumi imeendelea kuwa imara chini ya uongozi wa Shinoda, na hata ikitokea kuna hatari ya mipasuko ama migawanyiko ya ndani, basi mzee baba hatosikia chochote kwani ndio majukumu na kazi za watu kama Wakagashira, Wakagashira-Hosa kumpunguzia kazi kiongozi mkuu.

Takwimu kutoka Edelman Trust Barometer za mwaka 2023 zinadai kuwa ni asilimia 40 pekee ya wajapani ndio wanaamini kuwa serikali yao haina mahusiano na kundi la Yamaguchi-gumi, huku asilimia 60 wakiamini kuwa serikali ya Japani inafanya kazi na Yamaguchi-gumi.

Kwa upande wa Italia wao wameonesha kuwa waitaliano zaidi ya asilimia 65 wamedai kuwa serikali zao zinafanya kazi na makundi ya Mafia, kwa upande wa Mexico wao wananchi zaidi ya asilimia 75 wana imani kubwa kuwa serikali yao inaunga mkono na kubariki kwa ukaribu kabsa shughuli za wauzaji wa sembe, Sinaloa Cartel, Jalisco Cartel, Los Zetas, na wengine wamekuwa wakidaiwa kufanya kazi na serikali ya Mexico.

Mwisho wa makala hii ndio mwanzo wa makala nyingine, usikae mbali, nipo napika makala kuhusu mwanamke pekee ambaye anaheshimika ndani ya Yamaguchi-gumi na mayakuza wote na wamempa heshima ya kipekee ya jina la Onna-Oyabun ama Godmother of the Yakuza, Bibie Fumiko Taoka, mke wa Shinobu Taoka, Shinobu wa tatu wa Yamaguchi-gumi. Utafahamu mengi kuhusu Fumiko Taoka na namna ambavyo atabakia kuwa na heshima kubwa ndani ya Japani mpaka kesho.
 
Umetisha sana man🫡🫡 vitu vyangu hivi.... hawa yakuza wa japan walinifanya nipende kutazama filamu za kijapani haswa zile za kimafia kama showdown in little Tokyo na naked weapon.......
 
Umetisha sana man🫡🫡 vitu vyangu hivi.... hawa yakuza wa japan walinifanya nipende kutazama filamu za kijapani haswa zile za kimafia kama showdown in little Tokyo na naked weapon.......
Kuna Makala moja nadhani ipo YouTube, inaitwa Yakuza: Japan’s Criminal Underworld ilisimamiwa na National Geographic ni ya mwaka 2012, ukitazama utacheka sana, wajomba wapo social balaa ila ukiingia kwenye 18 zao wanasema hata nusu saa haumalizia, ni aidha ujipige Sepuku mapema au waje wakunyooshe wewe na familia nzima. Nilishangaa eti wanatoa mpaka misaada kwenye tetemeko la Tōhoku. 😃 😀 😄
 
Hivi hiyo seppuku ndio ile mtu anajichoma kisu tumboni na kumwaga utumbo wote?
 
Sema wajapan wako aggressive sana ukiingia kwenye 18 zao
 
Kama ni kundi la kihalifu kwanini halivunjwi?ilikuaje huyu Shinoda akarudi huko baada ya kutoka kifungoni?
 
Mbona taarifa inasema lina wanachama 12,000 tu,mbona ni wachache sana kuwathibiti hao,
Ndani ya serikali wale viongozi top ranking officials inasemekana ni Yamaguchi-gumi kitambo! Ndio maana hata alivyokwenda jela bado Yamaguchi-gumi walikuwa imara zaidi
 
Ndani ya serikali wale viongozi top ranking officials inasemekana ni Yamaguchi-gumi kitambo! Ndio maana hata alivyokwenda jela bado Yamaguchi-gumi walikuwa imara zaidi
Kama ni hivyo kazi ipo
 
Mbona wamekatwa vidole vya mwisho?
Vipi wanawake wapo humo?ukiacha huyo mmoja uliyemdokeza?
Umetisha Mkuu!
Hiyo kitu inaitwa Yubitsume
Ambapo ni suala linalofanywa na mtu endapo akikosea misingi na makosa madogo madogo, zamani samurai ndio walianzisha Yubitsume na kwa kuwa mila na desturi za Yakuza huendana na Samurai hivyo na Yamaguchi-gumi pia hufuata jambo hilo.

Mfano, Kobun* ama **Shetai endapo atafanya kitu tofauti na maelezo ya Shateigashira ama Wakagashira-hosa namna ya kukubaliwa msamaha wako ni kukata sehemu ya kidole chake.

Ukiachana na Fumiko Taoka ni vigumu kwa watoto wa kike kupata nafasi ndani ya Yamaguchi-gumi, ingawa baadhi wamekuwa wakihusika na operesheni wakiwa kama consultants pekee.
 
Du!hao ni hatari sana,kama anaweza kukata kidole chake vipi akitumwa kukushughulikia maana yake hakuna huruma hapo
 
Du!hao ni hatari sana,kama anaweza kukata kidole chake vipi akitumwa kukushughulikia maana yake hakuna huruma hapo
Seppuku pekee ndo itaokoa familia yako 😃 kuna Wakagashira-hosa wameshakuwa vilema, hawana visehemu za vidole vyao 😃
 
Ukosefu wa ajira ndio chanzo Cha kuibuka kwa makundi ya uhalifu kama YAKUZA na PANYAROAD!
 
Remeber The Name Shinoda namfananisha na Mafia mmoja hivi kwenye Picha la Kutisha yaani hilo lidude nili Monster haswaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…