Livefire habari kwanza, kama ukisoma vizuri nimesema hivyo vi-drone vinasaidia kuangalia majeshi au terrorist wako wapi [recon/scouting] kama unavyo sema. Sasa tatizo liko wapi? Kwani nani kasema humu kwamba drone hizo ni kama Predator zinazo beba mabomu ya hellfire! Au nani kasema vi-drone hivyo ni tishio kwa nchi za Africa Mashariki au kufikili Tanzania inaweza kutishwa na vijindege ambavyo vinaweza kuwa-brought down by a mere stone age anti aircraft guns; nani kasema KAF/KDF aina haki ya ku-modernise jeshi lenu!
Wewe unazungumzia mambo ya capabilities za heron/predator hivi unaweza kweli kulinganisha Raven drones ambazo unaweza kuzinyanyua kwa mkono na hazibebi air to ground missile wala bomb la aina yoyote ile! Nimeona umekuja juu hapa kuhusu comment yangu juu ya drones zilizo pelekwa Uganda! Labda nikuhulize swali, Je wewe ni a five star General wa jeshi la Uncle SAM mpaka ukajua kwa uhakika kwamba drones zilizo pelekwa Uganda haziusiki katika utafutaji majeshi ya KONY; kwa nini upendi watu wengine watoe maoni yao? Kuna mwana JF aliuliza kuhusu drones zilizo tolewa na Merikani kwa jeshi la Uganda mimi nikatoa maoni yangu, sasa imekuwa nongwa TENA!
Mleta post hii alikuwa na maana gani kuileta humu jamvini-kuna mahali amesema eti "KDF sasa itakuwa TISHIO kwa nchi jirani" - je huyu mtu anajua anacho zumgumza humu - who is afraid of a paper TIGER? eti "stay out of KDF inventories!!" nani kawaulizeni inventories la jeshi lenu? Kukosa kwenu kutafakali mambo mnaeleza kila kitu kilicho jikoni mwenu vingine vya kubuni tu! Hivi kweli kuna Mtanzania yeyote ambaye amewahi kuwa concern na jeshi lenu au kujali silaha zenu au kutangaza silaha za TANZANIA zinazo tumiwa na majeshi yetu au kujitapa kwamba tumenunua silaha fulani majirani zetu sasa watatukoma? Usifikili Jane's Defence books vina Intelligence na Analysis ya kweli kuhusu silaha na uwezo wa majeshi yote hapa duniani, wanayo andika humo ni script za maigizo ya HOLLYWOOD.
We unajuwa wapi doctrine za jeshi letu, unaleta mambo ya kubuni na propagada za nchi za magharibi; unaleta utani na a battle hardened jeshi (JWTZ) - nyie mumewahi kupigana wapi? mnatolewa kamasi na a rag tag al-shabaab alafu msivyo na aibu mnaomba nchi za jirani ziwasaidie kupigana a proxy WAR! - Livefire si unasema jeshi lenu ni moto wa kuotea mbali mbona mlikosa ubavu wa kujaribu jeshi la Uganda mlipo kuwa mnagombea kisiwa katika ziwa Victoria, mgefanya kosa kuwachokoza Uganda mkidhani eti "wangetumia swam/mass deployment tactics" na sijuhi term hii umeipata wapi? sina shaka umeisoma kwenye vitabu vilivyo andikwa kutoka nchi za magharibi kuhusu jeshi la UCHINA kwenye miaka ya 1940s/50, ila unacho sahau ni kwamba jeshi hilo lilitwanga Merikani katika vita vya KOREAmpaka wakashika adabu, bila umoja wa mataifa kuingilia kati sijuhi kungetokea nini? - Jibu unalo.
Livefire, mshukuru sana busara za Rais Kibaki ni binadamu anaye tafakali mambo kwa kina na hana papala! Hana majigambo na majivuno yasio na tija kama baadhi yenu walivyo - kama angefanya kosa na kuwachokoza Waganda saa hizi mgekuwa wakimbizi Sudan ya Kusini au Tanzania - Nimeyasema haya kukumbusha kwamba usiwe na tabia ya KUDHALAU majeshi ya jirani zako kwa kuwapachika majina ya kishenzi.
Mwisho labda nikukumbushe kwamba ukitaka kujuwa umahili wa jeshi la TANZANIA nenda kawaulize ma General wa jeshi la makaburu kuhusu vita vya Angola: Menu ilikuwa kama ifuatavyo:-
1) Fighter Pilots- Cubans/ Tanzanians na Angolans - marubani wa makaburu walichanganyikiwa walikuwa hawajuhi ndege za MiG23 na MiG21 zilikuwa zinahibuka kutoka wapi, hakuna cha wingman au angalia 12,3,6,9 O'Clock au radar viliweza kufua dafu. Mark you muda umekwisha pita tangu vita hiyo ipiganwe na vilikuwa vita vya kisayansi.
(2) Infantry ambayo ili-involve vifaru, magari ya deraya na artillery wahusika wakuu walikuwa ni - Cubans, Tanzanians, Angolans na nchi marafiki; makaburu na Savimbi walivua viatu na kukimbia miguu pekupeku wakiogapa milio ya Stalin ORGANS wakasahau G-55 zao.
(3) Manning Air Defence System - Tanzanians/Cubans/Angola.
Ninacho eleza hapa ni too brief, nikiogezea vita vya Msumbiji majeshi ya RENAMO yaliyokuwa yanasaidiwa na makaburu na Kenya ilikuwa inaunga mkono RENAMO lakini jeshi letu liliwashinda huko Msumbiji, kuna sakata la Seycells ambalo makaburu walivamia kisiwa hicho wakitaka Macham arudi madarakani kutoka aliko kuwa amekimbilia uhamishoni Kenya, walipo sikia majeshi ya Tanzania yanakuja mbona makaburu walifunga virago wakaondoka bila kuhaga! Eh, Livefire bado unafikili jeshi la TANZANIA linatumia a stone age tactics - mimi nakupa ushauri wa bure siku moja nenda pale ARUSHA wakati wa Bunge la EA limekaa, basi omba kukutana na mtoto wa the late J.Nyerere walao akupe somo kuhusu Artillery Engineering nione kama utaendelea na kejeli zako za kusema eti JWTZ "wanatumia swam/mass deployment tactics" kwenye medani za VITA. What a HARAKIRI statement!!!!