Snowden E
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 1,668
- 2,908
Ajali: Watu zaidi ya 50 wafariki katika ajali ya basi Kenya wakielekea Kisumu
Haki miliki ya pichaAFP
Watu 50 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu ya Nairobi-Kisumu.
Walioshuhudia wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea leo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.
Vyombo vya Habari nchini Kenya vinaripoti Kuwa ajali hiyo mbaya ilitokea katika eneo la Fort Ternan Kaunti ya Kericho.
Kwa mjibu wa kamanda wa polisi Kaunti ya Kericho, James Mogera, basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 67, lilitoka barabarani baada ya dereva kushindwa kulimudu kisha kugonga vizuizi vilivyokuwa kando ya barabara na kubiringia mita 20 kwenye bonde.
Kwa mjibu wa Gazeti la Daily Nation, miongoni waliofariki ni watoto wanane wa chini ya umri wa miaka mitano.
Awali idadi ya waliofarini ilikuwa 40 lakini polisi walielezae hofu yao juu ya vifo kuongezeka kutokana na hali ya baadhi ya majeruhi kuwa mbaya.
"Bahati mbaya sana tumepoteza watu 51," Mkuu wa Polisi Kenya Joseph Boinnet ameiambia redio ya Capital FM.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionPaa la gari hiyo lilifumuka baada ya kupinduka na kubiringia mara kadhaa.
Shuhuda mmoja anasema alisikia honi, ikifuatwa na mlio mkubwa wa breki, kisha akawasikia abiria wakipiga kelele.
Baadhi ya majeruhi wanatibiwa katika Zahanati ya Fort Ternan, huku wengine wakikimbizwa hadi kwenye Hospitali ya Kaunti mjini Muhoroni kwa matibabu.
Taarifa zaidi zinasema miili ya baadhi ya watu waliofariki ingali imekwama ndani ya mabaki ya basi hilo.
Source: BBCswahili